Waziri Mkuu awaamuru Madaktari kuripoti kazini Kesho!

Kwani hata akija kiongozi mkuu wa imani nyingine atafanya nini?

Angalia kiuchumi zaidi kujiona mfumo wenu upo vipi na mwelekeo wenu ni upi kiuchumi.

Kama mchumi kitaalamu nakwmbia mchana kweupeeeeeee hakuna jipya zaidi ya kujiongezea matatizo zaidi.

Issue ni kuangalia nani anaweza siyo imani yake. Mkuu uchumi wako ni wa 'kughushi'. Kwani hao waliofanikiwa walifanyaje mpaka wakaendelea?
 
PM acha ubabe, ma Daktari wanapotafuta haki zao, vitisho vya kuwafukuza kazi sio suluhisho, inachotakiwa serikali yako na chama chako kuyafanyia kazi madai yao, siku zote hutakiwi kukimbia changamoto bali ni ku deal nazo sambamba.
 
Ama kweli naanza kuamini ile kauli ya bora uwe mtupu mwilini kuliko kuwa mtupu kichwani... Siamini nikisomacho. Hivi watu wengine wamezaliwa na wanawake au ?
Faiza Fox ni mwendawazimu hivyo usipoteze muda wako, ni afadhali ukaongea na mbuzi unawezakupata la maana kuliko mtu huyo.
 
Mkwara hausaidii lolote. Solution ni kuwalipa madaktari stahili zao, mengine manjonjo tu.
 
Duuh! Cheap Politics Mtoto wa Mkulima! Madaktari ni rare profession not only in Africa but all over. sasa akijidai anawatimua ndo mwanzo wa maandamano ya kuutoa utawala wa JK madarakani. Waziri Mkuu usitumie ubavu tumia busara na uhalisia Jifunze kitu kutoka kwa majirani zetu Kenya nao pia waligoma December,2011 serikali ikaleta mkwara kama wako mwishowe serikali ilifyata mkia
 
haya majina ya humu ndani kumbe yanaendana na bongo za mtu uliona wapi mama porojo akawa na uwezo wa kufikiri. wewe umemsomesha nani, kwani mama ntilie pia siku hizi mnalipa kodi.

Mkuu, kama huna cha kuandika ni bora unyamaze. Hujui hata wananchi tunalipa vipi kodi sasa utakuwa unachangia nini hapa kama siyo mashudu tuuu? Unajaza post za kipuuzi hapa watu tunashindwa kusoma post za maana. Bibi yako kule kijijini analipa kodi ndo itakuwa mama ntilie? Na kwa taarifa yako kitu kisicholipiwa kodi hapa duniani ni pumzi pekee. Acha kudandia mambo usiyoyajua. Kama hujui kitu, pitia tuu post za wengine kama mimi ninavyoozipitia. UMENIHARIBIA SIKU YANGU.
 
Ama kweli naanza kuamini ile kauli ya bora uwe mtupu mwilini kuliko kuwa mtupu kichwani... Siamini nikisomacho. Hivi watu wengine wamezaliwa na wanawake au ?
Just regard that as a motivation to take action...
 
Nimeangalia jana hotubu ya Mhe Waziri Mkuu. Pamoja na nia nzuri ya kuona huduma za afya zinarejea kwa watanzania kuna mapungufu nimeona. Hawa madaktari wanaonekana tayari wamechukia na hawako katika hali yao ya kawaida ndio maana wanashinda katika kumbi za mikutano badala ya mawodini. Mioo yao tayari imechafuka kwa shida na maneno mbali mbali wanayosemezana. Sasa mhe unapotaka kutaua shida hii uwe mwangalifu sana. Matumizi ya nguvu ndiyo hasa wanayo taka. Wanataka kupima nguvu yao kwa serkali. Na wanatangaza kugoma kwa sababu wao wanaamini wataishinda serkali. Serkali iliyo na busara isiwape wanachotaka ili kujipima nguvu. Serkali ikijibu kwa mabavu ndicho hasa wanachotaka madaktari ili wajihakikishe kuwa wanaweza kuishinda au kuitingisha serkali. Mimi nafikiri Mhe PM hapa kinachotakiwa ni kumtuliza mwenye hasira. Si lazima kuwapa madai wanayotaka lakini yafuatayo yanaweza kufanyika:

1. Serkali ikubali kukaa na kuongea hata kama ni kukubali maongezi hayo yafanyike katika terms za madaktari kama venue na lini.

2. Serkali iwaruhusu madaktrai waseme kinachowauma na wapewe nafasi ndefu wajieleze. (Katika mtu kujieleza na akigundua unamsikiliza machungu ya moyo wake hupungua)

3. Majibu ya serkali yasiwe ya jazba bali madaktari waeleweshwe jinsi serkali inavyotambua na kuheshimu mchango wao katika taifa na kisha inavyojaribu kuwahudumia madaktari.

4. Waonyeshwe vikwazo vinavyozuia serkali kutimiza yote ambayo ingependa kuwafanyia madaktari na kisha madaktari waombwe wachangie mawazo ni ninii kifanyike na kwa njia zipi.

5. Kama madaktrari wanayo mawazo ambayo serkali inaweza kuyatumia kutatua shida zao mf namana ya kupata hizi fesha kwa muda mfupi kama wanaotaka na kwa viwango wanavyotaka basi si vibaya wakatekelezewa, la si vyo basi watiwe moyo kuendelea na kazi wakisubiiri uwezekano utakao kuja.

6. Sioni ubaya hata kama wanaweza kukaribishwa kushauri mambo fulani fulani yanayoweza kusaidia kukusanya mapato ya nchi, maana kabla ya kutumia unakusanya mapato. (Nafikiri madaktari ni inteliligent na wanaweza kuja na mawazo ya kuboresha) Kwa niia hii watajiona wana thamani na mmichango yao ya mawazo inaheshimiwa. Kama serkali ikikwama itakuwa si serkali pekee bali na madaktari watakuwemo.

Huu ni mchango wangu wa mawazo kwa PM tunaendelea kukuombea Mungu akusaidie katika kutatua suala hili.
 
Back
Top Bottom