Waziri Mkuu atoa masaa 48 Wafanyakazi 89 wafukuzwe kazi halmashauri ya manispaa Temeke

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa saa 48 kwa Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuwa amewaondoa kazini watumishi 89 wanaofanya kazi katika halmashauri hiyo kwa Mikataba.

Amewatahadharisha pia watendaji wa halmashauri zote nchini kutotumia fedha za miradi zinazopelekwa na serikali kinyume na malengo kutokana na kuimarishwa kwa mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi yake na thamani ya miradi itakayojengwa.

Aliyasema hayo alipozungumza na watumishi na watendaji wa manispaa hiyo, huku akiweka bayana kwamba halmashauri hiyo inaongoza kwa kuwa na watumishi wa Mikataba, jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za utumishi.

Akiendelea na mkutano huo, ghafla Waziri Mkuu alimsimamisha Kaimu Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Zaituni Hassan na kumuuliza idadi ya watumishi wa Mikataba katika halmashauri hiyo ambapo ofisa huyo alijibu kuwepo kwa watumishi 89.

Jibu hilo lilimfanya Waziri Mkuu kuhoji sababu ya kuwepo kwa idadi kubwa hiyo na kujibiwa kuwa hatua hiyo ilitokana na wengi wao kukosa sifa za kuajiriwa huku akisema wengi wao ni madereva.

Zaituni aliendelea kumwambia Waziri Mkuu kwamba mwaka jana Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitangaza nafasi za kazi na kuwataka watumishi hao kuomba lakini walishindwa kufikia vigezo vilivyowekwa na kusababisha halmashauri kuendelea kuwatumia bila kuwaajiri.

Pamoja na maelezo hayo, Waziri Mkuu alieleza kushangazwa na hatua ya kutokuwepo kwa madereva waliohitimu Kidato cha Nne ambao wangeweza kuajiriwa, hata hivyo Ofisa Utumishi huyo alimwambia waliopo wana elimu ya Kidato cha Nne lakini hawana vyeti vya mafunzo ya udereva kutoka Chuo cha Elimu na Mafunzo Stadi (VETA).

Majaliwa alieleza kuwa wanaotakiwa kuajiriwa kwa Mikataba ni walimu wa Masomo ya Sayansi na watendaji wa mitaa hivyo kama madereva hao hawana sifa ni vyema wakaondolewa kwa vile wanaziba nafasi za watu wenye sifa za kuajiriwa.

Alisema kutokuajiriwa ni moja ya sababu za kuwepo watumishi hewa hivyo alisema hadi kufikia Julai 30, mwaka huu, Ofisa Utumishi huyo awe amejiridhisha kuhusiana na sifa za watumishi hao ili wasio na sifa waondolewe na wenye sifa waajiriwe huku akisema zoezi hilo lifanyike katika idara zote.

Alimtaka kuanza taratibu za kumuomba Katibu Mkuu wa Utumishi kibali cha kuwaajiri watumishi hao na kusema ametoa nafasi hiyo kwa kuwa watumishi wengi katika halmashauri hawana mwelekeo mzuri kutokana na kutoajiriwa, hivyo wasio na sifa waondoke ili watafutwe wenye nazo.

Akizungumzia fedha zinazopelekwa katika halmashauri, Waziri Mkuu alisema kila fedha inayoingia katika halmashauri itakuwa na maelekezo ya matumizi na Mkurugenzi atalazimika kutoa nakala ya maelezo hayo na kumpatia Mkuu wa Wilaya ili ajue matumizi ya kila shilingi na thamani ya miradi.

Alisema baada ya kumaliza uteuzi wa viongozi mbalimbali, sasa Serikali inaanza kupeleka fedha za maendeleo katika halmashauri zote ili utekelezaji wa shughuli za maendeleo uendelee.
 
Hivi hao madereva wanashindwaje kusoma kozi za mwezi mmoja mmoja za umahiri pale VETA na NIT wanapokuwa likizo? Bora wafukuzwe kazi tu.
 
Kwa hiyo kaamua kupingana na boss wake? Walisema serikali imesimamisha ajira zote imekuwaje?
 
Sasa watatangazaje Ajira wakati ajira zimesimamishwa?

Pili kama hawa watu hawana sifa lakini wameonyesha Utendaji mzuri kwa nini serikali isiwape Ultimatum ya kuzisaka hizo sifa ndani ya muda fulani?

Mheshimiwa Waziri Mkuu, haya ni maisha ya watu, hawa watu wana familia wana watoto. Tuwape muda wazisake hizo sifa!
 
Hoja yako ina mashiko, lakini Mie nalia na hao madereva. Kozi za umahiri zinatolewa na VETA na NIT kuanzia wiki mbili na kuendelea, kuna ugumu gani kwao kuomba likizo fupi ama kutumia likizo zao ndefu kujiendeleza kitaaluma kwenye taasisi tajwa hapo juu na kupata astashahada? Ni makusudi ujue!
 
Sasa watatangazaje Ajira wakati ajira zimesimamishwa?

Pili kama hawa watu hawana sifa lakini wameonyesha Utendaji mzuri kwa nini serikali isiwape Ultimatum ya kuzisaka hizo sifa ndani ya muda fulani?

Mheshimiwa Waziri Mkuu, haya ni maisha ya watu, hawa watu wana familia wana watoto. Tuwape muda wazisake hizo sifa!
Walikua wapi muda wote huo kujiendeleza kama sio wazembe hao?
 
Mh sijaona mahali amesema watangaze ajira bali nimeona sehemu ikisema waanze mchakato wa kuomba kibari cha kuajili, maana yake serikali itakapotangaza ajira Temeke nao wawemo kwa nafasi za madereva!
 
Kama huna mkataba ni ngumu kupewa likizo hiyo kwenda kupata cheti.Hakuna sababu ya kuwaacha,wapewe muda kutafuta sifa.
 
Uko NIT kama kuna mtu aliyewai kusoma huko paka upate chet lazma uwandae milion ya kuhonga bila ivyo kwenye test utafelishwa ukienda kwa maveko utapewa alama za barabarani za uturuki ujibu maswali lazma uchemke tu siwalaumu sana hawa madereva tatizo ni majipu kila sehemu
 
Kama huna mkataba ni ngumu kupewa likizo hiyo kwenda kupata cheti.Hakuna sababu ya kuwaacha,wapewe muda kutafuta sifa.
elimu huna basi hata certificate ya driving nayo ni shida?

Hawa wengi wao ndio wale wenye matumbo makubwa wakiwaleta mabosi zao kwenye tafrija yanapenda kufakamia msosi utadhani ndio mwisho wa maisha, majitu ya namna hii hayawezi kuwa na akili.
 
Hivi hao madereva wanashindwaje kusoma kozi za mwezi mmoja mmoja za umahiri pale VETA na NIT wanapokuwa likizo? Bora wafukuzwe kazi tu.

Ni kweli mkuu hata mimi nimeshangaa kama ni kweli wanashindwa tuu kusoma vile vikoz VETA hawapendi kazi
 
Back
Top Bottom