Elections 2010 Waziri Mkuu atamka: Kugawa kanga kwenye kampeni ni rushwa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Tanzania, aka mtoto wa mkulima huko Sumbawanga alipokuwa analiomba radhi kanisa kuhusu kashfa ya udhalilishaji wa imani, ametamka wazi kuwa kugawa kanga kipindi cha kugombea nafasi za uongozi ni rushwa. Alitamka hivyo alipogusia suala la rushwa katika uchaguzi ambao chama cha CCM kiliibuka na kashfa kubwa ya kutumia rushwa tangu kura za maoni. Amewaasa wanaccm kubadilika ingawa ni kazi ngumu alisema.
:target:
 
Wakati zinagawiwa aliona akakaa kimya. Baada ya uchaguzi ndiyo amefahamu kuwa ni rushwa?
 
Sina imani na Pinda tena.................................... ameshakuwa pombe ya kijani na njano.
 
Wakati zinagawiwa aliona akakaa kimya. Baada ya uchaguzi ndiyo amefahamu kuwa ni rushwa?

mambo yaleyale ya VX V8 kasusa eti hataki gari la gharama anabana matumizi, wakati limenunuliwa tayari, hapo hapo alisema mpeni waziri
mwingine, yaani nachoka asubuhiii, Pinda....!!!!:nono::nono:
 
Sina imani na Pinda tena.................................... ameshakuwa pombe ya kijani na njano.

Miye nilishapoteza imani naye toka alipotamka kwamba wale mafisadi wa EPA ni matajiri wakubwa nchini na kama wakikamatwa basi nchi ingewaka moto.

 
hawa CHAMA CHA MAJAMBAZI, ni lazima waondoke madarakani, leo hii wewe PINDA kwa kuwa uko kanisani ndo unajua kugawa kanga ni RUSHWA.......? maisha yanazidi kuwa magumu kila kukicha kwa ajili ya kuwakamua wafanyabiashara mpate hela za kuhonga ili mrejee madarakani. uchaguzi ukiisha nao wanapandisha bidhaa bei kufidia pengo la hela mlizochukua(UKUTAKA KUFANYA BIASHARA TZ HII KUWA MWANA CCM, mhe f sumaye)
 
Du! kasheshe!!! Lakini is unakumbuka aliwahisema watumishi wasivae suti? Na akasema Ma- VX na Ma V8 ni anasa? Jiulize yeye havai suti? hapandi ma VX na Ma V8? this is stupidity.
 
Pinda ni Mgonjwa anahitaji maombi mazito!

Pinda was hope within the government, but he is increasingly becoming something else. Naona ameamua kufuata nadharia ya "if you can not beat them, join them". Lakini tunaopotea ni watanzania.
 
Back
Top Bottom