Waziri Mkuu anatoka chama gani?

masaiti

Senior Member
Jun 16, 2008
196
22
Wana JF, napenda kupata ufanuzi kuwa je waziri mkuu wa Tanzania anatoka katika chama chenye wabunge wengi bungeni au? Je Dr Slaa akishinda urais na ccm ikawa na wabunge wengi, je itamlazimu ateue waziri mkuu toka ccm ? Ambalo baadaye itamlazimu kuwa na serikali ya mseto kwani waziri mkuu naye anahusika kupanga baraza la mawaziri. Naomba ufafanuzi wa suala hilo.
 
Kwa sasa katiba ya nchi inasema chama kinachoshinda ndio kinaunda serikali, so waziri mkuu atatoka chama kitakachoshinda!
 
Waziri mkuu hutoka chama chenye wabunge wengi bungeni na kama Chadema itakuwa na wabung wengo basi Chadema itatoa PM pia
 
Kwa sasa katiba ya nchi inasema chama kinachoshinda ndio kinaunda serikali, so waziri mkuu atatoka chama kitakachoshinda!

SEHEMU YA TATU

WAZIRI MKUU, BARAZA LA MAWAZIRI

NA SERIKALI

Waziri Mkuu

51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano

atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na

ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais

kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa

na Bunge.

(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku

kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua

Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi

anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi

Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge

wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio

wengi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika

madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa

na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge

walio wengi.

(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri

Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi(

a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake;

au

(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au

(c) siku atakapojiuzulu; au

(d) siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwa

Waziri Mkuu; au

(e) atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibu

wa masharti mengineyo ya Katiba hii.
 
Mkumbuke kuwa waliotunga katiba hii, walijua kuwa CCM itaendelea kushika madaraka wakati wote. Ni katiba ambayo inalenga kumpa nguvu anayekuwa mshsindi wa urais. Bado imekaa kwa mtindo wa "winner takes all", lakini opposition wakiwa na zaidi ya wabunge nusu bungeni kivitendo wao ndio watakuwa serikali na Rais atakuwa msindikizaji tu. Tusiishie kuangalia PM tu, tuiangalia katiba kwa ujumla wake.
 
SEHEMU YA TATU

WAZIRI MKUU, BARAZA LA MAWAZIRI

NA SERIKALI

Waziri Mkuu

51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano

atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na

ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais

kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa

na Bunge.

(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku

kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua

Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi

anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi

Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge

wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio

wengi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika

madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa

na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge

walio wengi.

(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri

Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi(

a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake;

au

(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au

(c) siku atakapojiuzulu; au

(d) siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwa

Waziri Mkuu; au

(e) atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibu

wa masharti mengineyo ya Katiba hii.

Nakushuku sana Miruko kwa ufafanuzi wa kikatiba uliotupa.
Hivyo kuna uwezekano wa serikali ya mseto kuundwa iwapo Dr Slaa akishinda urais na ccm ikawa na wabunge wengi, kwani kulingana na katiba waziri mkuu inatakiwa atoke chama chenye wabunge wengi (ccm), au JK akishinda urais na chadema ikawa na wabunge wengi, basi waziri mkuu ni lazima atoke chadema.
 
Mnayabeza maoni Synovate, REDET, vyombo vya DOLA na Daily News? Uchaguzi TZ ni kama vile umeshaisha! WM ni Pinda, Spika ni Lowasa, SS ni waziri wa KATIBA na Sheria. Wanasubiri kuapa tu.
 
Wildcard!unashangaza sana,siku hizi mnapanga tuu matokeo mezani?au hakuna uchaguzi?nguvu hiyo umeipata wapi?Au ndiyo ule mpango wa CCM na NEC kuchakacua matokeo?
 
Nashukuru kwa swali la kisayansi. Uteuzi wa Waziri mkuu utakuwa mgumu kama chadema ikipata wabunge wengi na rais akatoka chama tofauti. Ila kwa msimamo wa chadema kutoa katibatmpya ili alitakuwa tatizo tena. Rais mpya dr.SLAA ameliona sana suala ilo ndo kaamua kuaidi katiba mpya kuwakomboa maskini. Mbowe au Zitto kama si waziri mkuu wa kwanza m/mke dada Halima Mdee atafaa kukaa pale, mama Kaiula awe Tamisemi, Tundu lisu waziri wa sheria, Mnyika Mambo ya nje, ndesamburo Waziri wa fedha,Marando chief Justice, ulinzi chibuda, maliasili Ana komu,...CHADEMA IKO kamili asikwambie mtu. Wito kwa dr. SLAA japo umemtaja dr. Jakaya kikwete kwenye first 11 ya mafisadi,nakuomba uingiapo ikulu umwache huru aweze kukuonesha maficho ya majasusi wa rasilimali za Taifa. Ikumbukwe kuwa kuna kinga kwa rais kikatiba, awapo na anapomaliza muda wake. Mola aingoze nuru ya chadema,akina Sheikh yayah washindwe kwa nguvu zao za giza.
 
Zito waziri wa nishati na madini
 
Back
Top Bottom