Waziri Mkuu anapopingana na Rais

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,875
2,739
Juzi hapa ndani ya Bunge la Jamhuri tulishuhudia Waziri Mkuu Mizengo Pinda akinasa kwenye mtego wa swali lililoulizwa na mh Wenje kuhusu madaraka na mamlaka ya watumishi wa umma kwa wananchi dhidi ya utumishi kwa chama kilichopo madarakani. Tulishuhudia Pinda akisema kuwa hao watumishi wa umma wakiwa ni pamoja na wakuu wa mikoa na wilaya wana haki ya kufanya kazi za chama ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa ccm kinaendelea kutawala...

Kabla yake, Rais alishawahi kutamka na kkuonya juu ya hao hao watumishi wa umma ambao walishasahau majukumu yao na kujiingiza kwenye siasa za ccm. Ndipo wakati wa kuteua wakuu wa wilaya na mikoa, Rais akawaonya na kuwaasa na kuwakaripia kuwa wasiende kufanya siasa bali kutumikia wananchi! Na yeyote atakayekwenda kinyume na hayo maagizo atatoswa! Sasa leo tena tunasikia eti wao ni ruksa kufanya kazi za chama ili kutekeleza ilani ya chama ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ccm hakitoki madarakani.

Waziri Mkuu anapingana na Rais. Huu ni udhaifu wa taasisi ya urais au ni athari za uropokaji za PM, au ni mkakati wa ccm uliojificha ambao wenyewe wanaufichua bila kujua?
 
Ni kawaida mno na sana kwa Pinda kuropoka hata Sensa walibofoa pia huyu kasema lile huyu hili!!always inaonekana hakuna coordination
 
Ni kawaida mno na sana kwa Pinda kuropoka hata Sensa walibofoa pia huyu kasema lile huyu hili!!always inaonekana hakuna coordination

Ni kweli hakuna coordination maana matamko yanayokinzana ndani ya ccm si haba
 
Inawezekana vilevile akawa sahihi kutekeleza maelekezo ya chama/mkuu wake. Je uliyaamini maneno ya Mh. JK aliyoyatamka adharani?? Wakuu wa mikoa na wilaya wanatekeleza majukumu yapi kikatiba? Zaidi huwa wanatekeleza majukumu yao kutokana na semina elekezi.
 
Huwa Pinda ni Bulicheka ila kuna muda ukikaa ukatulia unaweza ukaona labda Pinda ananyoosha maelezo(anaongea ukweli) ya kile kilichosemekana kwenye vikao vyao vya chama ingawa hakutakiwa kuja kusema hadharani.

Hii inatokana na laana ambayo tayari inatembea nao sawa na mtu aliyekwishauwa binadamu mwenzake kuna kipindi kikifika anaanza kuongea mwenyewe niliua fulani nikamuuwa na fulani ila anakuwa anaropoka bila kujitambua. Pinda huyo
 
Basi tuamini tu kuwa tulidanganywa na jk. Na Tanzania ijue sasa ya kuwa watumishi wa umma waliopo na kwa kiasi kikubwa walioteuliwa na Rais wako kwa maslahi ya chama na si Taifa
 
Sijaona wanapopinga hayo ni mawazo yako umeamua kutumia uhuru wako wa kikatiba kuwakilisha mawazo yako hiyo ndio demokrasia.
 
Kukataza watumishi wa umma wasisiriki siasa na kuunga mkono watumishi wa umma kusaidia chama tawala si kupingana? Ritz just be honest
 
Hata mkulu Dhaifu nae ni kigeu geu!mbona lile tamko la kutenganisha siasa na biashara hadi leo halieleweki?
Huyu mtoto wa fiswadi ni kama bata tu nae huwa ana penda kuhara anapo jisikia!hana lolote!
 
Huwa Pinda ni Bulicheka ila kuna muda ukikaa ukatulia unaweza ukaona labda Pinda ananyoosha maelezo(anaongea ukweli) ya kile kilichosemekana kwenye vikao vyao vya chama ingawa hakutakiwa kuja kusema hadharani.

Hii inatokana na laana ambayo tayari inatembea nao sawa na mtu aliyekwishauwa binadamu mwenzake kuna kipindi kikifika anaanza kuongea mwenyewe niliua fulani nikamuuwa na fulani ila anakuwa anaropoka bila kujitambua. Pinda huyo
hapa umesema kweli mkuu. Pinda sio mwanasisasa, inajulikana kuwa hawa wakuu wa mikoana na wilaya sio watumishi wa umma bali ni makada wa chama, lakini ili wapate mishahara ni lazima watumie mgongo wa Serikali. kwa hiyo kazi yao hasa ni kuhakikisha uhai wa ccm. lakini wanadanganya umma kuwa ni watumishi wa seikali, kwa mkritu safi ambaye anazitii amri za Mungu hawezi kuwa mwanasiasa, hasa wa ccm kwa kuwa katika manemo mia utakayoonge sio zaidi ya mawili ya ukweli.
 
Mkuu wa mkoa yuko pale kushuhulikia maswala ya mji na wananchi wote bila kujali ni wa chama gani so kama pinda kasema hivo kweli ndio muone tofauti ya huyu bwana na lowasa.. Mlifanya kosa sana kutaka lowasa ajiuzulu mliruka mkojo mmekanyaga mavi tena ya kijani
 
hapa umesema kweli mkuu. Pinda sio mwanasisasa, inajulikana kuwa hawa wakuu wa mikoana na wilaya sio watumishi wa umma bali ni makada wa chama, lakini ili wapate mishahara ni lazima watumie mgongo wa Serikali. kwa hiyo kazi yao hasa ni kuhakikisha uhai wa ccm. lakini wanadanganya umma kuwa ni watumishi wa seikali, kwa mkritu safi ambaye anazitii amri za Mungu hawezi kuwa mwanasiasa, hasa wa ccm kwa kuwa katika manemo mia utakayoonge sio zaidi ya mawili ya ukweli.

Sasa ndugu, kwa kuwa umesema kuwa Pinda si mwanasiasa. Na kwa kuwa umesema kuwa mkristu safi hawezi kuwa mwanasiasa. Unamaanisha kuwa Pinda ni mkrisu safi?
 
Namuamini pinda ndio aliyesema ukweli kwani ndio agenda za chama JK aliongea propaganda ila ni upepo tuu....
 
Hawajapingana ila wapo kazini,hakuna kuingiliana katika majukum kila mtu anatekeleza ya kwake.
 
Ni kweli kuna muda nimefikiria, iwapo cdm wamekamata Dola, haya hayatajitokeza?
 
Back
Top Bottom