Waziri Menejimenti ya Utumishi wa Umma: Lugha ya malkia Elizabeth, mhhhhh!

Sijawahi kumsikia akiongea kiingereza tupu zaidi ya kumsikia akiongea kiswanglishi.

Jamani twende mbele turudi nyuma hii lugha inatutesa sana watanzania. Afadhali FL yeye hata akiwa nyuuyoku huwa anatwanga kiswahili tu badala ya kujitutumua kwa kiingereza. Na huyu mama si ashauriwe tu awe ananena kwa Kiswahili. Nadhani hii si mara ya kwanza kuharibu kuna wakati nadhani pia aliharibu.
 
ndio ni kweli. Mwanzoni sikujua hilo lakini aliniambia mgeni mmoja. Akasema ndio maana pesa zetu zimendikwa Kiingereza na nyaraka zote za muhimu ni kwa Kiingereza lakini kubwa kabisa hukumu (katika mahakama za juu) zinatolewa kwa Kiingereza pia. Kwa hiyo promotion ya Kiswahili ni kama unafiki tu ambao nao 'wanaouendesha' unawatafuna kama tulivyomuona mama Ghasia jana.
Naomba mwenye mawazo zaidi atusaidie hapa.
Hapo kwenye red: Hivi ni kweli mkuu?
Sasa mbona mfumo wetu wa elimu hauoneshi kuendana na hilo?
Yote kwa yote, mh. waziri jana katuangusha. Mbona nchi za wenzetu viongozi huongea kwa lugha zao, ni jukumu la wale wanaosikiliza kutafuta wakalimani.
Hata hivyo ile risala alikuwa akiwahutubia wazungu au watanzania?
 
Sijui ila mh. waziri alikuwa anajitutumua kuongea kiingereza matokeo yake ikawa ametengeneza lugha yake nyingine kabisa ambayo bado haijatambulika kwa sasa.
English was born in England, modified in America, destroyed in Africa and died in India.
 
tanzania hata bila ki-ingereza inawezekana.!

Kwa nini viongozi wetu wanalazimisha kuongea kitu wasichokijua. Mbaya zaidi wanapenda kujinadi mbele ya wenyewe wenye lugha yao. Wanaaibisha kwa kweli.
 
Kwa wale walioangalia maadhimisho ya miaka 50 ya Utumishi wa umma mtakubaliana na mimi mh. waziri wa wizara hiyo lugha gongana. Mimi niliyekuwa namsikiliza hadi niliona aibu jinsi alivyotuaibisha tena mbele ya wenye lugha yao. Na hapo alikuwa akisoma kwenye makaratasi. Angekuwa anazungumza moja kwa moja sijui ingekuwaje. Ni bora angeongea katika lugha anayoijua. Yaani ilikuwa balaa.

Hata mimi niliona aibu sana, kitu kinachonisikitisha ni kuwa Waziri wetu nafikiri hajui shida yake kuwa anatatizo la namna ya kuongea lugha ya kiingereza kwa ufasaha, huenda ni baadhi ya wale ambao wanaamini kuwa unaweza kuongea lugha hii ya kigeni"automatic". Viongozi wetu wanapopewa nyadhifa lazima waainishe matatizo yao hasa ya kimawasiliano ili angalau kwa kuweza kuzungumza hii lugha ya Kiingereza kwa ufanisi ili ikitokea ulazima wa kutakiwa upande hewani isiwe aibu kama hii ilivyotokea maana kuanzia utamkaji wa maneno n.k utagundua kuwa Bi. Mkubwa yamemkuta.
 
Yametukuta wote mkuu, maana alikuwa anatuwakilisha.
 
Ukimsikikiliza yule aliyekuwa Waziri wa Africa Mashariki ,KAMALA unaweza ukazimia. Tena anaji-address kama PhD, sijui aliipataje hiyo doctorate.
 
Huyo ni Ghasia, hujabahatika kumsikiliza Lukuvi....utajuta kumsikiiza

Mmmhh MK mimi sikuwa najua hili mkuu. Anyway wakati nadhani Lukuvi naye anapaswa kukijua kimalkia angalau kwa elimu yake Diploma ya ualimu ninaweza kumsamehe kidogo. Tatizo langu kubwa kwa huyo waziri mwenye nyodo Ghasia, CV yake insema amesoma MSc ya Rural Development SUA kama sikosei sasa hata hiyo dissertation alidefend vipi? Lakini pia kwa nyodo alizonazo hata kama mfumo wetu hautuandai vizuri kwenye lugha ya Malkia ningekuwa yeye ningetumia juhudi binafsi kuijua lugha hii muhimu. Hivi hawa watu hata kiingereza hawawezi kujifunza (sijasema kwamba English ndio kila kitu) wanawezaje kutuongoza kwani I'm sure wanafahamu fika kuwa English ni muhimu sana sana.
 
Kwa wale walioangalia maadhimisho ya miaka 50 ya Utumishi wa umma mtakubaliana na mimi mh. waziri wa wizara hiyo lugha gongana. Mimi niliyekuwa namsikiliza hadi niliona aibu jinsi alivyotuaibisha tena mbele ya wenye lugha yao. Na hapo alikuwa akisoma kwenye makaratasi. Angekuwa anazungumza moja kwa moja sijui ingekuwaje. Ni bora angeongea katika lugha anayoijua. Yaani ilikuwa balaa.

Hii kazi kapewa na shemeji yake JK hivi hujui wana uhusiano wa karibu sana na mama Salma. huyu mama hii ndo post yake ya juu sana kutoka msaidizi wa DED hadi full minister. Na ujue ana uzoefu kuliko Aggrey Mwandry na Balozi Kagasheki amabo wameendelea kuwa manaibu mawaziri kwa vipindi viwili mfululizo kwa sababu uzoefu wao wao mdogo kuwa full ministers.

Huyu dada amesoma MSC. Rural Development pale SUA miaka ya 1998-2000. Kiingereza kizuri cha hitaji juhudi binafsi za kujisomea vitabu n.k. sas huyu huo muda hana atajulia wapi kiingereza dada wa watu wa kimakonde kama siyo wa kiyao?

Ghasia kila mtu anajua ni incompetent na kama unakumbuka alivyoanza alijidai ku-adapt system ya Mary Nagu ya System ya performance measurement ya kila mfanyakazi wa umma. Hii ingesaidia kila mtu kuwa na work plan yake ambayo mwisho wa siku watafanya self assessment na kama plan versus actual work ni less than 50% basi huna kazi au unashushwa cheo. Hii haiku take off kwa sababu siasa iliingia na mpango mzima kutupwa baada ya wanasiasa kugundua kwamba vilaza wengi wangemwaga unga.

Mkorogo anaoufanya Ghasia unatokana na kubweteka kwa sababu hakuna wa kumyooshea kidole wal kumchapa kiboko.
 
Mi naona huu ni mwendelezo wa madudu ya huyu bibie. Nakumbuka kuna wakati alishawahi kulalamika kwa rais eti kwenye wizara yake kuna maelfu ya wafanyakazi hewa ambao wanasababisha upotevu wa mabilioni ya pesa za walalahoi. Si masihara haya!
 
Hivi ile tuition ya kiingereza almaarufu kama Maimuna si ingemsaidia sana huyu mama.
 
Back
Top Bottom