Waziri Menejimenti ya Utumishi wa Umma: Lugha ya malkia Elizabeth, mhhhhh!

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Kwa wale walioangalia maadhimisho ya miaka 50 ya Utumishi wa umma mtakubaliana na mimi mh. waziri wa wizara hiyo lugha gongana. Mimi niliyekuwa namsikiliza hadi niliona aibu jinsi alivyotuaibisha tena mbele ya wenye lugha yao. Na hapo alikuwa akisoma kwenye makaratasi. Angekuwa anazungumza moja kwa moja sijui ingekuwaje. Ni bora angeongea katika lugha anayoijua. Yaani ilikuwa balaa.
 
Kwani hao kina malkia wanaongea lugha ngapi?

Sijui ila mh. waziri alikuwa anajitutumua kuongea kiingereza matokeo yake ikawa ametengeneza lugha yake nyingine kabisa ambayo bado haijatambulika kwa sasa.
 
nami niliona pia, angefanya kwa Kiswahili ingeeleweka zaidi! ...lakini, hivi wengi wetu tunajua kuwa Kingereza ndiyo lugha ya taifa hili (official language)?
 
Kwani hao kina malkia wanaongea lugha ngapi?

Malkia na senior members wengi wa royal family wanaongea english, french & german.

Kwenye hii ya waziri Ghasia, kwangu mimi shida si kuongea kiingereza, ila ni kung'ang'ania kuongea kiingereza huku mambo ni upside down. Kwa nini asiongee kiswahili na wakatela mkalimani? au aanza darasa hapo British council.
 
nami niliona pia, angefanya kwa Kiswahili ingeeleweka zaidi! ...lakini, hivi wengi wetu tunajua kuwa Kingereza ndiyo lugha ya taifa hili (official language)?
Kiswahili ndo lugha ya Taifa, ila Kiingereza na Kiswahili zote ni lugha rasmi Tanzania.
 
nami niliona pia, angefanya kwa Kiswahili ingeeleweka zaidi! ...lakini, hivi wengi wetu tunajua kuwa Kingereza ndiyo lugha ya taifa hili (official language)?

Hapo kwenye red: Hivi ni kweli mkuu?
Sasa mbona mfumo wetu wa elimu hauoneshi kuendana na hilo?
Yote kwa yote, mh. waziri jana katuangusha. Mbona nchi za wenzetu viongozi huongea kwa lugha zao, ni jukumu la wale wanaosikiliza kutafuta wakalimani.
Hata hivyo ile risala alikuwa akiwahutubia wazungu au watanzania?
 
Kwenye kiingereza ndio mawaziri na viongozi wetu wengi sana wanapoonyesha unyonge wao ndio maana hata wakienda nje mijadala ya maana huwa wanaishia kuwa wajumbe sio wachangiaji!!wanasinzia wakitoka wanawahi shopping tu!
 
Kwa wale walioangalia maadhimisho ya miaka 50 ya Utumishi wa umma mtakubaliana na mimi mh. waziri wa wizara hiyo lugha gongana. Mimi niliyekuwa namsikiliza hadi niliona aibu jinsi alivyotuaibisha tena mbele ya wenye lugha yao. Na hapo alikuwa akisoma kwenye makaratasi. Angekuwa anazungumza moja kwa moja sijui ingekuwaje. Ni bora angeongea katika lugha anayoijua. Yaani ilikuwa balaa.

Lugha ni tatizo la kitaifa huko Tanzania. Tuulize sisi waalimu tutakwambia.

Hata Viongozi wenu woooote hakuna hata mmoja anayeweza kutoa hotba kwa lugha ya kimombo bila kushika karatasi na kusoma kama risala..

Angalia hotba za JK Nyerere kama alikuwa anashika karatasi na kusoma.??
 
Malkia na senior members wengi wa royal family wanaongea english, french & german.

Kwenye hii ya waziri Ghasia, kwangu mimi shida si kuongea kiingereza, ila ni kung'ang'ania kuongea kiingereza huku mambo ni upside down. Kwa nini asiongee kiswahili na wakatela mkalimani? au aanza darasa hapo British council.

Kwa nini viongozi wa Tanzania wanapenda kujitutumua kuongea kiingereza huku hali ni ngumu. Mbaya zaidi wanatumia lugha hiyo hata pale wanapotaka kueleweka na wananchi wao. Ni aibu kuiga lakini ni aibu zaidi kuiga kitu kimakosa.
 
Nilimuona mwanamke aliyejigubika Ushungi akijikanyaga mbele ya Kadamnasi akiwemo PM Pinda,sikujua ni nani... Kumbe ndiye Hawa Ghasia??? Ama kweli tuna safari ndefu sana Wa-Tz...
 
Jana nilikuwapo na mke wangu nilimjuza hili jambo wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili Usiku. nakamuuliza hivi ni kwelin huyu mama anaweza kuhutubia kwa Kingereza bila kusoma, maana hata uwezo wake wa kusoma uko chini sana.
Ushauri wangu katika hilo, ikiwa ni lazima sana kutumia Kingereza, ni vyema wakatumia Kiswahili na wakaweka wakalimani wao, maana ni aibu sana.
 
Kwa nini viongozi wetu hawaenzi lugha yao? Ufaransa, China, Urusi, Ujerumani, Uholanzi, Sweden, Norway, etc wanatumia lugha zao! Nenda Japan, Korea, Misri, Ethiopia,UAE etc wote wanatumia lugha zao!! Hata Rwanda, japo wanazungumza Kifaransa matumizi makubwa ni Kinyarwanda....sijui sis tatizo letu ni nini!!
 
Ulimbukeni
 
Back
Top Bottom