Waziri Mbarawa awafunda DIT

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, ameutaka uongozi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), kupunguza mlundikano wa kozi kwa lengo la kuleta ufanisi.
Kwa mara ya kwanza, alipotembelea taasisi hiyo tangu kuteuliwa kwake kuwa waziri hivi karibuni, Waziri Mbarawa alizungumza na uongozi, wahadhili, wafanyakazi na wanafunzi wa taasisi hiyo jana, kwa lengo la kutaka kujionea mwenyewe utendaji kazi na matatizo yaliyopo.

Akizungumza na wahadhiri akiwemo Mkurugenzi wa Mafunzo, Profesa Christian Nyahumwa, Waziri Mbarawa aliuonya uongozi wa taasisi hiyo kupunguza mlundikano wa kozi ambao unasababisha kupungua kwa ufanisi na gharama kuwa kubwa.

Katika suala la mawasiliano, Waziri Mbarawa aliutaka uongozi huo kuwa na mawasiliano kati ya menejimenti, wafanyakazzi, wanafunzi na wizara ili kupunguza mingongano isiyo ya lazima kutokea kama ilivyo sehemu nyingi za kazi.

“Nimesoma jana mahali fulani, nimeona kuwa mna kozi nyingi sana, naona ingekuwa vyema kuzipunguza ili kuleta ufanisi kwa wanafunzi na walimu, lakini pia kupunguza gharama kubwa ikiwemo vifaa na wafanyakazi,” aliongeza.

“… Huwezi kuibuka tu ukajiamulia leo kukatiza masomo au somo bila kuwashirikisha wanafunzi, ukafanya maamuzi makubwa bila kuwashirikisha wafanyakazi, haya yote husababisha migongano na migomo kwa wanafunzi au wafanyakazi, ni lazima kuepuka matatizo kama haya,” alionya waziri huyo.

Akitoa taarifa kwa waziri, Mkurugenzi wa Mafunzo katika taasisi hiyo, Profesa Christian Nyahumwa, alisema tayari taasisi imeanza mikakati ya matumizi ya vitendea kazi vipya vilivyopo ili kuboresha ufundishaji.
 
WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, ameutaka uongozi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), kupunguza mlundikano wa kozi kwa lengo la kuleta ufanisi.
Kwa mara ya kwanza, alipotembelea taasisi hiyo tangu kuteuliwa kwake kuwa waziri hivi karibuni, Waziri Mbarawa alizungumza na uongozi, wahadhili, wafanyakazi na wanafunzi wa taasisi hiyo jana, kwa lengo la kutaka kujionea mwenyewe utendaji kazi na matatizo yaliyopo.

Akizungumza na wahadhiri akiwemo Mkurugenzi wa Mafunzo, Profesa Christian Nyahumwa, Waziri Mbarawa aliuonya uongozi wa taasisi hiyo kupunguza mlundikano wa kozi ambao unasababisha kupungua kwa ufanisi na gharama kuwa kubwa.

Katika suala la mawasiliano, Waziri Mbarawa aliutaka uongozi huo kuwa na mawasiliano kati ya menejimenti, wafanyakazzi, wanafunzi na wizara ili kupunguza mingongano isiyo ya lazima kutokea kama ilivyo sehemu nyingi za kazi.

"Nimesoma jana mahali fulani, nimeona kuwa mna kozi nyingi sana, naona ingekuwa vyema kuzipunguza ili kuleta ufanisi kwa wanafunzi na walimu, lakini pia kupunguza gharama kubwa ikiwemo vifaa na wafanyakazi," aliongeza.

"… Huwezi kuibuka tu ukajiamulia leo kukatiza masomo au somo bila kuwashirikisha wanafunzi, ukafanya maamuzi makubwa bila kuwashirikisha wafanyakazi, haya yote husababisha migongano na migomo kwa wanafunzi au wafanyakazi, ni lazima kuepuka matatizo kama haya," alionya waziri huyo.

Akitoa taarifa kwa waziri, Mkurugenzi wa Mafunzo katika taasisi hiyo, Profesa Christian Nyahumwa, alisema tayari taasisi imeanza mikakati ya matumizi ya vitendea kazi vipya vilivyopo ili kuboresha ufundishaji.

Hivi Profesa wa nyuklia John Aron Kondoro bado yupo^ manake yule mzee ni mtu wa shari sana, si kwa wanafunzi wahadhiri wala wafanyakazi wengine.

Anyway hilo la kupunguza kozi sio issue, cha msingi serikali iongeze mafungu wananchi wake wapate taalum. Muhimu ni taaluma inayotolewa ikidhi mahitaji, hizo kozi zinaanzishwa kutokana na mahitaji.
 
Back
Top Bottom