WAZIRI MASELE ananikosha..

theHAVARD_product

JF-Expert Member
May 4, 2012
289
191
Wakuu nimekuwa nikifuatilia mtiririko wa huyu jamaa ,na siku hadi siku anzidi kuonesha Kile kitu ambacho hakijafanywa miaka mini cheki hii ya KARIBUNI.


NAIBU Waziri wa Nishati na Madini,Stephen Masele ameiamuru kampuni ya TanzaniteOne kuacha kumwaga maji kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.


Akizungumza jana na uongozi wa kampuni hiyo,Masele ambaye ni Naibu Waziri anayeshughulikia madini aligeuka na kuwa mkali mithili ya mbogo wakati akizungumzia suala hilo kwa viongozi wa kampuni hiyo.​



Naibu waziri alitoa amri hiyo baada ya kuelezwa na wachimbaji wadogo alipofanya ziara ya kutembelea migodi yao kuwa kampuni hiyo inawamwagia maji mgodini na alipotoa amri hiyo gari lake lilisukumwa na wachimbaji hao.


“Sawa ninyi ni wawekezaji lakini Serikali haipo tayari kuona wachimbaji wadogo wananyanyaswa katika nchi yao hivyo niwaamuru kusitisha mara moja kumwaga maji hayo kwenye migodi ya wachimbaji wadogo,” alisema Masele.




Hata hivyo,Mwenyekiti wa kampuni ya TanzaniteOne,Ammi Mpungwe alimthibitishia Masele kuwa kampuni yake haimwagi maji kwenye migodi ya wachimbaji wadogo ila maji hayo yanatoka yenyewe kwenye mgodi wa TanzaniteOne.


Mpungwe alisema maji hayo hutoka nyenyewe kutokana na jiolojia ya miamba ilivyo kwenye mgodi wao wa Bravo ambao haufanyiwi kazi lakini kampuni hiyo haijawahi kumwaga maji kwenye migodi ya wachimbaji wadogo.


“Mheshimiwa waziri mimi nilikuwa balozi na nikastaafu kwa heshima zote,sasa siwezi kwenda jela leo kwa kosa la kukiuka sheria za nchi,mimi ni mzalendo sitakubali kuruhusu kampuni yetu imwage maji migodini,” alisema Mpungwe.


Pia,Naibu Waziri huyo aliitaka kampuni hiyo kusaidia huduma za jamii kama madawati shuleni,afya na maji kwenye kata zote nne za tarafa ya Moipo zilizopo pembezoni mwa migodi hiyo kuliko kuisaidia kata moja ya Naisinyai.


“Watanzania hawatatuelewa ikiwa kampuni hii inachimba madini ya Tanzanite yenye utajiri mkubwa wakati kata za jirani wanafunzi wanakaa sakafuni,huduma za afya duni na barabara ya Kia-Mirerani ni ya vumbi,” alisema Masele.



Akizungumzia kuhusu hilo,Mpungwe alisema watajipanga kulitekeleza ila alisikitishwa na kitendo cha viongozi wa kilichokuwa kijiji cha Mirerani kukataa msaada wa zaidi ya sh12 milioni walizotoa kama msaada wa maendeleo mwaka 2000.
 

Attachments

  • uncle.jpg
    uncle.jpg
    18.8 KB · Views: 241
Wanachukua tanzanite kwa kuchangia madawati shuleni maskini tanzania shamba la bibi
 
Tanzanite ni Madini Pekee yanayopatikana Tanzania tu!!! Kuna haja Gani ya kuwashirikisha Wazungu?... Of all the People unamzungumzia Massele? ameifanyia nini Taifa hili? Muulize Petradiamond wataanza lini kulipa stahili za Watanzania? Kwenye Dhahabu mrabaha wa 1.2% unakaguliwa na nani?..
 
Mleta mada. Yaani wewe ni bonge LA mzembe. Anachofanya Masele ni kutimiza wajibu wake, sasa nashangaa anachokukoshea sijui nini. Wewe ni kama wale walioukataa utumwa , wakajikuta hawana uhuru
 
Acha ushabiki wew, hayo ni majukumu yake ni si swala gen alilofanya na isitoshe hata utekelezaji haujafanyika unaanza kutokwa na bofuu. Hayo ni maneno ya kujikosha aonekana ni mtu mwema kwa wanaume ila hapo kinachofanyika ni kiin macho maana bahasha ina mhusu na hata hana muda wa kufanya ufuatiliaji tena!!!
 
Back
Top Bottom