Waziri Maige mfupi mno, azuia wawekezaji kutumia mitambo katika uzalishaji

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
IMG_0246.JPG
IMG_0135.JPG

WAZIRI MAIGE AWAPIGA 'STOP' WAWEKEZAJI KUWANYIMA AJIRA WATANZANIA

WAZIRI wa maliasili na utalii Ezekiel Maige amewataka wawekezaji wa makampuni na viwanda katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kuendesha viwanda hivyo kwa kuzingatia mahitaji ya nchi ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa vijana nchini badala ya kutumia mashine kufanya kazi ambazo vijana wangeweza kuzifanya.

Waziri Maige ametoa kauli hiyo jana wilayani Mufindi wakati kikao chake na wawekezaji wakubwa katika msitu wa hifadhi ya Taifa wa Sao Hill Mufindi .

Amesema kuwa hatua ya wawekezaji kutumia mashine na wageni kutoka nchi kwa kazi ambazo watanzania wanaziweza ni kutowatendea haki watanzania ambao walitegemea uwekezaji huo kuwawezesha kupata ajira zaidi.
 
Suala la ajira kwa vijana haina maana tuendelee na mfumo wa utendaji wa karne iliyopita kwa kutumia guvu za watu badala ya kuongeza vitendea kazi vya kurahizisha na hivyo kuongeza uzalishaji.

Huyu waziri anaturudisha nyuma, badala ya kutumia mitambo ya kisasa katika upasuaji mbao, sasa turudi nyuma enzi za kuchimba shimo na kuweka boriti huku wapasuaji wawili wanaotumia msumeno mkubwa mmoja akiwa shimoni na mwingine juu huku wako vifua wazi wapasue mbalo.

Huyu waziri hana ubunifu wa njia za kuwapatia ajira vijana na sasa anawalazimisha wawekezaji wasitumie mitambo kitu ambacho kitapunguza uzalishaji na kuwatia hasara.
 
Dah,ajira kwa wazalendo...Bado sijaona kama ataokoa tatizo la ajira kwa kusisitiza njia za miaka 50 iliyopita.Kinachatokiwa ni kuboresha nguvu kazi kwanza ili iendane na teknolojia inayokua,si kufanya kuwanufarahisha wengi kwa mafanikio kiduchu kamwe hatutoendelea kwa mtindo huu
 
Huyu ni mmoja kati ya mawaziri vijana tunaotegemea kuwa na mawazo mapya ya kubuni njia za ajira kwa vijana, sasa anakuja na hii ya mwaka 1947 katika kizazi cha leo kinachoendesha biashara na uwekezaji kiushindani nadhani ni mtumwa wa fikra fulani, sitegemei kama ni kitu kutoka kichwani mwake. Hili ndilo tatizo la viongozi wa CCM.
 
If we really want to do good for the young citizens of this country, we should educate them and assist them to become players in the global business dynamics. Hii ya kuwa labors akaifanye kwenye mji wake...anawalostisha hao vijana
 
Mimi nakerwa sana ziara za serikali zinapochanganywa na itikadi.......huyo gamba na hizo kijani-manjano ametia dosari hii ziara

IMG_0135.JPG
 
jamaa mambo yamemzidi. watu wanafikiria kuhusu efficiency and productivity kama binadamu hawezi fanya kazi kwa haraka na kuna machine inayoweza fanya kazi kwa haraka why not using the machine. ndo maana tunashauri tuweke elimu mbele na sio ufisadi mbele
 
Huko ughaibuni nilipokuwa mwanafunzi niliwahi kufanya kazi kwenye kampuni moja ya uchapishaji majarida ya matangazo ya makampuni ya biashara kama Sears, Walmat nk kila mtambo ulikuwa unazaliwa majarida milioni moja ndani ya 24 hour, Maana yake hapo ni uendeshaji ulikuwa wa robotical system na binadamu ni kutouch screen tu, vinginevyo kasi yake katu binadamu huwezi kabisa. Sasa huyu Maige yuko wa kizazi kipi? Aibu tupu mawaziri wa Kikwete.
 
nilichoelewa ni kwamba maige ana hofu isiyokuwa ya lazima na zaidi anahofia chama cha ccm kuendela kutawala....wawekezaji wa huko mufindi hasa wa Green resources/ Saohill industries wamefunga mitambo ya kisasa ya kupasua mbao ambapo mtambo mmoja ulizinduliwa na makamu wa raisi hivi majuzi....yeye maige anataka kila kitu kifanywe na vibarua ili kuwapa ajira wazawa....nimemsikia katika report hii mkurugenz wa Green resources alimjibu waziri kuwa wanatumia mitambo hiyo ya kisasa ili kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa maana wavunapo mti toka shambni ni asilimia 30 tu ndiyo wanayoitumia na hiyo huwapa hasara kubwa na kwa hivyo wanafunga mitambo hiyo ili kuweza kuutumia mti kwa asilimia 100......

ukisikiliza taarifa hiyo ya maige ni hofu tu maana nimesikia pia anasema kuwa wawekezaji wasinunue ardhi kwa wakulima maana huko mbele chama tawala kikiondoka madarakani basi kuna hatari ardhi watayokayokuwa wamenunua watanyang'anywa na itarudishwa kwa wananchi...na ametumia neno ''natabiri'' kuwa huko mbele hii ardhi itarudishwa kwa wananchi na hivyo kama wawekezaji wanataka ardhi basi wasinunue ardhi ya wananchi masikini ila waongee nao na ikiwezekana wapande miti kwenye ardhi ya hao wananchi, miti ikokmaa wavune lakini ardhi ibaki mikononi mwa wananchi...
 
Pamoja na maelezo yako mazuri, ukweli unabaki kuwa kiongozi aliye na dhamana serikali na kujali ukuaji wa uchumi asingeweza kuonge alichoongea huyu waziri, ni alama wazi ya mtazamo wa kizamani na usio wa kiuchumi. Kuna kila dalili ya viongozi wetu kujifikira binafsi bila kuangalia maslahi ya uchumi wa taifa. Au alitaka watoe rushwa ili awasifie kutumia mitambo kuongeza uzalishaji?
 
mkuu kama umenielwa vizuri ni kwamba HOFU ndiyo inamsumbua...bomu la kutokuwa na ajira kwa vijana wengi na hivyo kupoteza imani na ccm inamsumbua.....kama ungepata riport hiyo ungemsikia mkurugenzi wa mufundi paper mill bwana chondri na mkurugenzi wa Greenresources bwana mwaniki walivyosaidia kunyoosha mind set ya waziri maige....
 
Maige kwa hili kaniangusha.. ingawaje ni katika hazina Tanzania iliyokuwa nayo. Ukimfuatlia kwa makini yupo tofauti sana na wenzake katika baraza la Kikwete
 
Huyu ni mmoja kati ya mawaziri vijana tunaotegemea kuwa na mawazo mapya ya kubuni njia za ajira kwa vijana, sasa anakuja na hii ya mwaka 1947 katika kizazi cha leo kinachoendesha biashara na uwekezaji kiushindani nadhani ni mtumwa wa fikra fulani, sitegemei kama ni kitu kutoka kichwani mwake. Hili ndilo tatizo la viongozi wa CCM.

ni kweli tatizo ni kwamba wakati anapanga safari ya kwenda hapo hakujua anaenda kufanya nini aliwaza safari tu na posho ndio mmaana kaongea tu bila kufikiri mradi siku ipite we mtu kaleta mitambo we unaangalia tu imefika inafanya kazi we upo tu leo ghafla unasema usiitumie

Back
Top Bottom