Waziri Maghembe avikoroga vyuo vikuu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WANAFUNZI wa vyuo vya elimu ya juu nchini wamemcharukia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Jumanne Maghembe kutokana na agizo lake la kufuta mfumo uliopo wa serikali za wanafunzi katika vyuo hivyo.
Kutokana na agizo hilo lililochapishwa kwenye Gazeti la Serikali Juni 12, 2009, marais wa Umoja wa Serikali za Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO), wamekuwa wakikutana na kutoa maamuzi kuhusu agizo la Waziri Maghembe.

Katika hicho inachokiita waraka, serikali kupitia Waziri Maghembe ilitoa mwongozo ikitaka serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu kuwa chini ya utawala na mwongozo wa mshauri wa wanafunzi huku rais wa chuo akiitwa, mwenyekiti badala ya rais.

Kutokana na hali hiyo, marais hao wametoa wito kwa Waziri Maghembe kubatilisha haraka uamuzi huo, vinginevyo suala hilo lingefikishwa kwenye mabunge ya serikali zao na mikutano mikuu ya vyuo kwa uamuzi wa mwisho.

Aidha, walisema endapo Maghembe hatabadili msimamo huo, wako tayari kufanya lolote ikiwa ni pamoja na kuendesha kampeni za kumpinga kisiasa hadi jimboni kwake.

Katika vikao vyao vya Februari 20 hadi 23, 2010, katika Taasisi ya Uhasibu ya Arusha na Chuo cha KCMC, marais hao (Maseneta) waliamua kumwandikia Waziri Maghembe na kumpa msimamo wao ikiwa ni pamoja na kutokuwa tayari kufanya mabadiliko huku wakimtaka asitishe waraka huo haraka.

Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa TAHLI SO, Katongo Noel, na nakala yake kutumwa kwa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), NACTE, COSTEC, Makamu wa Wakuu wa Vyuo Vikuu, marais wa serikali za wanafunzi na wanafunzi wote, maseneta hao wamehoji mambo mbalimbali juu ya uamuzi wa Waziri Maghembe.

“Kwani kuwapo mabadiliko hayo na vyeo vya watendaji wa ofisi za serikali za wanafunzi na jina linaathiri nini? Vipi kuhusu gharama za kubadili katiba, sheria ndogondogo, mwongozo wa shughuli za chuo (Prospectus), nani atabeba gharama hizo? Mbona katika miaka ya nyuma majina ya viongozi hao hayakuwa na madhara yoyote kwa serikali?

“Hivi ni kweli tunaandaa viongozi imara wa sasa na wa baadaye wa kitaifa na kimataifa kama hata katika ngazi ya vyuo vikuu tunachukuliwa kama watoto wadogo. Hivi katika ngazi hii tunapaswa kuwa watazamaji huku mtu mwingine akifikiri, kuamua na kutufanyia?” Noeli alihoji kwa niaba ya wenzake.

Katika mahojiano na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki, baadhi ya marais na wawakilishi wa vyuo vikuu mbalimbali walisema hawako tayari kufanya mabadiliko hayo kwa kuwa yanakwenda kinyume na sheria za vyuo vikuu na zile zinazoanzisha serikali ya vyuo vikuu.

Kwa upande wake, Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISWOSO), Emmanuel Mwasota, alisema, “Agizo la Waziri Maghembe halikufanywa kwa umakini kwani katiba za vyuo vyetu, hazimtambui Mwenyekiti zinamtambua Rais.

Lawrance Mwantimwa ambaye ni rais katika Chuo Kikuu cha Tumaini upande wa Dar es Salaam (TUDACO), alisema anashangazwa kwani haoni mamlaka ya jina Rais katika serikali ya wanafunzi pia anashangaa kwa vipi yanamuumiza Waziri Maghembe.
 
hawa wanazuoni wetu nawashauri kuwa hii misimamo yao isiishie tu kulinda maslahi yao, wakitoa misimamo kama hiyo dhidi ya mafisadi pia itasaidia jamii.
 
Back
Top Bottom