Waziri Lukuvi shughulikia uzembe mkubwa idara ya ardhi kanda ya Moshi

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,801
18,527
Idara nzima ya ardhi kanda ya Kaskazini yenye makao makuu Moshi imegubikwa na rushwa na uzembe mkubwa mno!

Huwezi kusaidiwa bila kutoa rushwa

Kupata cheti cha usajili wa ardhi huchukua mwaka mmoja au zaidi.

Kamishna wa ardhi ndio tatizo kubwa. Amelundika lundo la maombi na hafanyii kazi maombi hayo hadi apate chochote

Tunamwomba waziri Lukuvi kumwajibisha Kamishna wa ardhi kanda ya Kaskazini pamoja na watendaji wengine wazembe katika ofisi za ardhi Moshi kwani utendaji wao mbovu unachelewesha maendeleo ya nchi
 
Back
Top Bottom