Waziri Lawrence Masha hana uwezo

Punda kiongwe na Punda milia wote punda tu, wanatofautiana mistari, lakini mwendo, mikogo na matendo ni yale yale tu.
 
Mkuu FMES,
Tulipoliongelea hili la Masha + Imma + Deepgreen + Ridhiwani Kikwete, ulijitokeza kumtetea kijana Masha kuwa ni safi, je huu msimamo bado unao au kuna mabadiliko??

Mkuu heshima mbele, bado ninaifuatilia kwa makini sana hii ishu sofa bado ninampa the benefit of the doubt,

Lakini kama kawaida huwa inadai ukweli au dataz, kama sio facts, hapa ni lazima niwe mkweli wa Mungu, habari chache za dataz nilizonazo kutoka huko ndani zinanipa wasi wasi sana kwani kuna ambayo nimeyasikia ambayo sijayathibitisha ila lakini ninaamini kuwa ni the matter of time tu ukweli utatoka wazi,

Ikifahamika kuwa ana mkono kwenye ufisadi badi nitakuwa wa kwanza kusema wazi, lakini so far bado sijaona ushahidi wa kutosha kumhukumu kuwa ni fisadi, na niamini kuwa nimegusa kila mahali so far na bado ninaendelea kutafuta ukweli.
 
Mkuu Mmongoiwe

Kasome Gazeti La Mwananchi!!!!!!au Kama Uko Mbali Fungua Website
Ukupenda Zaidi Naomba Ulete Kilichoandikwa Kikiwa Tofauti Na Haya
Jf Si Ushabiki Tupo Kurekebisha Na Si Kutetea Uchafu.......mkuu

"""""""""ujumbe Waambie Muda Umefika Hukumu Ile Ile........"""""""""""
 
Nilivyoona Hiki Kwa Pdidy Ikabiid Nkanunue Magazeti Kuangalia Kama Ni Kweli...na Huo Ndio Ukweli Halisi Kaka ..usittete Ushabiki Kumbuka Familia Na Kizazi Chako Cha Baadae!!!!!kama Na Wewe Uko Kwenye System Kumradhi
Tusaidiane Kurekebisha Uozo!!!!!!!!!!!!!!
 
:confused:Najiuliza wakati fulani, hivi watu wanaotuhumiwa kufurahia Ufisadi huwa wanajifikiria nini! Jumamosi katika harakati za kusaka Mlimbwende wa Kanda ya Ziwa, baada ya Mshindi kutangazwa na kukabidhiwa zawadi, Mheshimiwa sana Masha, waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Muungwana, alimua naye kutoa zawadi za kwake kwa washindi na washiriki wote.

Sijui alikuwa akitafuta nini kwa hawa warembo, lakini pia sijui alikuwa akitafuta nini katika mashindano haya ya kikanda, ingekuwa ni shughuli ya jimboni kwake Nyamagana au angalau Mkoa wake angeeleweka.

Lakini wakati akifanya hivi, sijui kama alikuwa amelewa sana ama namna gani kuna watu ambao walikuwa wakishangilia -- fisadi fisadi fisadi -----katika ukumbi ule.

Lakini hii ilikuwa ni saa chache tu tangu atoke kwenye mkutano wake wa hadhara na wapiga kura wake ambako aliulizwa mengi likiwemo la hali ngumu ya maisha kusababishwa na Ufisadi na kwamba kampuni yake ya kisheria kuhusishwa na ufisadi baada ya kusaidia kusajiri kampuni ya Deep Green. Akajibu kwa kubabaisha na wasaidizi wake kuwashawishi waandishi wa habari wasindike haya kwa mshiko kama wanavyosema wao wa shilingi 20,000.

Nimeona kama gazeti la Mwananchi ndilo lililoandika habari hii kwa stahili yake mengine naona yamempunga upepo Mhe saana.

Nafikria enzi ya Nyerere ingekuwaje kuwa na kiongozi wa namna hii, nafikiria pia Muungwana anafikiria nini wakati anateua viongozi wake, au hana ushauri wa akina Kingunge?
 
:confused:najiuliza Wakati Fulani, Hivi Watu Wanaotuhumiwa Kufurahia Ufisadi Huwa Wanajifikiria Nini! Jumamosi Katika Harakati Za Kusaka Mlimbwende Wa Kanda Ya Ziwa, Baada Ya Mshindi Kutangazwa Na Kukabidhiwa Zawadi, Mheshimiwa Sana Masha, Waziri Wa Mambo Ya Ndani Katika Serikali Ya Muungwana, Alimua Naye Kutoa Zawadi Za Kwake Kwa Washindi Na Washiriki Wote.

Sijui Alikuwa Akitafuta Nini Kwa Hawa Warembo, Lakini Pia Sijui Alikuwa Akitafuta Nini Katika Mashindano Haya Ya Kikanda, Ingekuwa Ni Shughuli Ya Jimboni Kwake Nyamagana Au Angalau Mkoa Wake Angeeleweka.

Lakini Wakati Akifanya Hivi, Sijui Kama Alikuwa Amelewa Sana Ama Namna Gani Kuna Watu Ambao Walikuwa Wakishangilia -- Fisadi Fisadi Fisadi -----katika Ukumbi Ule.

Tusipoangalia, Kila Kiongozi Tanzania Ataitwa Fisadi Halafu Na Maana Halisi Ya Ufisadi Itamomonyoka Na Kuwa Kama Yale Yaliyopita Mf. Tapeli, Kihiyo (ambao Wapo Wengi Sana Sasa) Nk.
 
Gembe,

Hata mwandishi mwenyewe kaiandika habari hii kiudaku udaku, ndo maana bado unauliza maswali. Kwani kuna taabu gani mi nikiamua kugawa zawadi kwa warembo?

Ongeleeni issues acheni udaku.

FairPlayer
 
Gembe,

Hata mwandishi mwenyewe kaiandika habari hii kiudaku udaku, ndo maana bado unauliza maswali. Kwani kuna taabu gani mi nikiamua kugawa zawadi kwa warembo?

Ongeleeni issues acheni udaku.

FairPlayer
Kuna haja ya kujua katoa shillingi ngapi?Tunamfahamu Masha kwa undani na tabia zake hasa akishapata Ulabu.Tunahitaji kujua na ndiyo maana ya Fair Play
 
Iachwe hapa hapa,wewe Umetumwa ili uje Umtetee huyu kijana?FMES nawewe umo katika muongo wa kusema kwamba Masha hajadiliki?
 
Tusipoangalia, Kila Kiongozi Tanzania Ataitwa Fisadi Halafu Na Maana Halisi Ya Ufisadi Itamomonyoka Na Kuwa Kama Yale Yaliyopita Mf. Tapeli, Kihiyo (ambao Wapo Wengi Sana Sasa) Nk.

Katika lugha ya kisiasa FISADI sio jina ama sifa moja. UFISADI ni mfumo unaohusisha washika dau wengi wa madaraja na majukumu tofauti. Wapo mafisadi wa kisiasa, kijamii na kiuchumi. Na hawa wapo wanastrategia, wapo watekelezaji, wapo wafaidikaji, wapo wa kula masaza (watoto, ndugu, jamaa na wapambe wa mafisadi), wapo watetezi na wapo walinzi (wanasiasa kama kina chitalilo, waandishi, wanausalama, makada chongo etc). Vilevile hata wale wanaonyamaza kuacha ufisadi ukitendeka pia ni mafisadi. Kwa kifupi tupo wengi lakini focus kubwa ipo kwa wale mafisadi wa kiuchumi na kisiasa ambao wameunda mtandao wao wa kufanikisha na kulinda nafasi yao ndani ya mfumo fisadi.

Tanzanianjema
 
iachwe Hapa Hapa,wewe Umetumwa Ili Uje Umtetee Huyu Kijana?fmes Nawewe Umo Katika Muongo Wa Kusema Kwamba Masha Hajadiliki?
Kwa Kweli Hii Taarifa Inahitaji Uchambuzi Wa Kina,maana Sijajua Kama Mwandishi Anapinga Mashindano Ya Urembo Au Anapinga Masha Kuwa Mgeni Rasmi Au Anapinga Masha Kuwaonga Waandishi Au Anapinga Masha Kutoa Zawadi Binafsi....kama Ni Mashindano Ya Urembo Basi Anapaswakujua Kuwa Yapo Kitaratibu Zinazokubalika,kama Ni Kuwa Mgeni Rasmi Anapaswa Kujua Kuwa Nafasi Ya Ugeni Rasmi Huwa Haiombwi Bali Unaombwa,kama Ni Kweli Aliwaonga Waandishi Wasitoe Taarifa Nadhani Ungetekeleza Wewe,magazeti Yote Yana Contacts Ungeandika Then Utume Wewe Mwenyewe Na Naamini Wahariri Wangeitumia.na Kama Zawadi Binafsi Hapo Sina La Kusema Maana Ni Yake Na Si Ya Wizara Au Ya Serikali,na Pia Ni Zawadi Gani Na Kama Ni Peni Zenye Nembo Ya Saidia Polisi Kupambana Na Wahalifu????
 
Sijaona lolote la kumtuhumu Masha. Jibu swali langu, kutoa zawadi kwa warembo ni kosa?

Yaani bongo hii balaaa kabisa.
 
Sijaona lolote la kumtuhumu Masha. Jibu swali langu, kutoa zawadi kwa warembo ni kosa?

Yaani bongo hii balaaa kabisa.
kaka msamehe bure nadhani hakuwa ata anajua kuwa alikuwa anataka kuanduka nini haoa kabla ya kutuandikia....safari bado ni ndefu kama huu nao ni ufisadi wa kujadili humu ndani.
 
Kuna haja ya kujua katoa shillingi ngapi?Tunamfahamu Masha kwa undani na tabia zake hasa akishapata Ulabu.Tunahitaji kujua na ndiyo maana ya Fair Play
__________________
Mgoyangi lete za leoleo, je hakubeba mmoja wao?
 
Tuambie alligawa shilingi ngapi kwa kila Mlimbwende?

Sijui inawezekana kuwa na viongozi wa namna hii ni maendeleo, na huenda alichokifanya kinastahili kuungwa mkono kwa mtazamo wa wengine. Lakini kamwe zawadi binafsi kutoka kwa Masha kama , shilingi 150,000 na Seti ya Tv, shilingi laki moja kwa mshindi wa Urembo wa Pili na Laki Moja kwa mshindi wa Tatu, na shilingi 50 kwa kila mmoja kati wengine tisa waliobakia, na hapo hapo kuna zawadi tayari zilikuwa zimetolewa na muaandaaji, lakini pia kuna wahitaji wengi wenye shida katika jimbo lake, hili haliingii akilini.

Lakini Pia tuangalia aina ya viongozi ambao tunawatarajia linapokuja suala la vitendo, mienendo na yale ambayo jamii inatarajia iwafanyie.
 
Sijui inawezekana kuwa na viongozi wa namna hii ni maendeleo, na huenda alichokifanya kinastahili kuungwa mkono kwa mtazamo wa wengine. Lakini kamwe zawadi binafsi kutoka kwa Masha kama , shilingi 150,000 na Seti ya Tv, shilingi laki moja kwa mshindi wa Urembo wa Pili na Laki Moja kwa mshindi wa Tatu, na shilingi 50 kwa kila mmoja kati wengine tisa waliobakia, na hapo hapo kuna zawadi tayari zilikuwa zimetolewa na muaandaaji, lakini pia kuna wahitaji wengi wenye shida katika jimbo lake, hili haliingii akilini.

Lakini Pia tuangalia aina ya viongozi ambao tunawatarajia linapokuja suala la vitendo, mienendo na yale ambayo jamii inatarajia iwafanyie.
Atakuwa anamuwinda kati ya hao mabinti,myaniambia baadaye
 
Kuna haja ya kujua katoa shillingi ngapi?Tunamfahamu Masha kwa undani na tabia zake hasa akishapata Ulabu.Tunahitaji kujua na ndiyo maana ya Fair Play
__________________
Mgoyangi lete za leoleo, je hakubeba mmoja wao?

????????????
our future.........
 
Naona si vyema kumshambulia mleta mada, badala yake tumuombe atupe data zaidi ili tumkome nyani vizuri. kwamfano katika mada yake kuna issue kuu mbili na mawili yatokanayo:

1) -Waandishi walikatiwa mshiko wa alfu 20 ili wasiandike maswali ya wapiga kura wake ya kwanini aliisajiri Deep Green? je aliwajibu majibu ya kutosheleza?
---Je waandishi kwa kupokea hiyo alfu 20 mkaacha kuandika habari nzito namna hii mnatutendea haki watanzania wenzenu?

2)-Jambo la pili ndo hilo la kutoa zawadi binafsi kwa ma miss, je ni jambo jema kwa waziri mwenye dhamana kufanya hivo? je anapo toa pesa hiyo kwa shughuli kama hiyo wakati wapiga kura wake kuna watoto wana shindwa kwenda shule kwa kukosa uniform ya alfu 5 ni sawa?

----Jambo la mwisho linatokana na baadhi ya wachangiaji wanao uliza kwamba alitoa sh ngapi na kama alikuwa kaisha onja mbili tatu kwani wanamjua tabia yake, wasi wasi wangu ni je, waziri mwenye dhamana hatakiwi kuwa na maadili fulani ya kulinda heshima yake na pengine kuwa katika mazingira na hali ambayo haihatarishi maslahi ya taifa?, mfano kama akionja anakuwa 'out of himself' hawezi kuliingiza Taifa mkenge kwakutoboa siri, ama kufanya maafikiano fulani ambayo hayana tija kwa Taifa?
 
Back
Top Bottom