Waziri Lawrence Masha hana uwezo

nop

mimi nsina muda wa mambo haya lakini hali ikiwa ngumu si unajua tean sie wengine tunahama mabaraza ..ukitoka Mtaa wa msimbazi unahamia pale mtaa wa udoe kwa shekh Nurudini,siku nyingine unapitia Pale klabu ya PAN AFRICA au ukichoka unaenda Makao ya zamani ya YANGA ...kisha SAIGONI nk

lakini Mwanasiasa unajua mambo ya humu yananikumbusha ETHINTANK kue yahoo
 
serikali ya kikwete haina watendaji. ukihesabu wakufukuzwa, nafikiri tunafaa kuanza na yeye rais mwenyewe, maana miaka miwili imepita na hatuoni mafaniko hata kidogo.

huyo magufuli aweza kuwa anafanya haki kwa upande mmoja, ila humo humo watu wasio na hatia wanapokonywa viwanja vyao kwa kuwa hawana pesa ya kuviendeleza!

isitoshe, kama waziri hakupaswa kumtaja naibu wake bungeni kuwa kakiruka kiwanja chake. hiyo ni kutaka sifa zisizo maana.
 
Rufiji na wakandamizaji wengine acha tu, Hahaaaaaaaaaaa
Kazi ipo ,kumnywesha mbuzi dawa malaria ipo kazi
 
Watanzania mnaniacha hoi!! Yaani kama tunaona Magufuli hafai basi nadhani akina Karamagi ndo saizi yetu!Magufuli hayuko 100% perfect lakini anawajibika 95% anajua matatizo ya sehemu anayopewa na anajua namna ya kuyamaliza.Sasa isiwe ikawa baadhi mikakati yake inatugusa baadhi then ndo ubaya wake unakuja.
 
Nyangumi mi nakubaliana nawewe katika hili,
Yes Magufuri anamapungufu yake kama wengine wote, but kwa kazi yake ya kujenga barabara kipindi cha BM hata kama alikuwa akichukua cha juu walau kazi ilifanyika na tuliiona, na hata sasa huko ardhi pamoja na Lawama lakini ule uzungushwaji usio kuwa wa msingi wa kwa wananchi wa kawaida umepungua sana! Ofcourse wafanyakazi wenzie hawampendi kwani kawazibia ulaji! but all in all Myonyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, jamaa ni mchapakazi!

Basi tu mchezo wa siasa ndo unao mgharimu kutaka kumpunguzia umaarufu lakini kazi anafanya bwana!
 
Habarini za Baraza jipya wanaJF,leo nataka niwaletee habari ya Masha na watoto wa Lowassa waliandaa sherehe ya kumuaga au kama sio kupongeza mzee wao mpendwa na fisadi. Majuzi sherehe hiyo iliandaliwa mahususi kumpongeza kwa kufisadi watz for two years!! Ilikuwa kama ni kulipiza mapigo ya ile ya watu wa sumaye!lakini cha ajabu JK anaye tena masha. Jamani hatutoki ktk ufisadi,masha anaweza kufunga lowasssa????
 
Ndugu zangu Watanzania !
Mara ya mwisho kuwaandikia kuhusu lile sakata lilopelekea kifo cha Dr, Omary Alli Juma ,nimefurahi kuwa jamaa wengi na hasa wasomi tu wazuri wame jibu kwa kukurupuka kwani kama wangekuwa ni wafuatiliaji wazuri wa mada husika wangeunda kile kitu kiitwacho Facts Finding Mind katika vichwa vyao na sio kulalama oooh jamaa hayuko seriously kwani wanataka umakini gani tena kunako hili !

Sasa hili la Waziri masha nalo nadhani kuna mamluki wameingilia hii fani ili kujaribu kupotosha ukweli na hawa ni wale wasio na akili either wanafanya kwa makusudi ama kwa kutumwa na makubwa wao kuwa nendeni mkatibue mada ili tu kupotosha ukweli na vitu kama vile sasa sijui hapa kwa Masha watasemaje ?

Masha ile kampuni yake ilitumiwa tu na CCM ili kuchota yale Mabilioni ya BOT kusema kuwa alitumiwa na CCM namaanisha kuwa ile DEEP GREEN FINANCE LTD ni kampuni ya CCM amabyo ndio iliyopewa tenda tena na serikali eti kupeleka bomba la mafuta kule Mwanza hebu niambie Serikali ya CCM na kampuni ya CCM ila sasa lengo halikuwa kupeleka Bomba la mafuta ila ni kuchota yale Mafedha ya BOT kwa ajili ya kampeni ambazo ndio zilichangia kumweka JK katika madaraka ambayo ndio hiyo hiyo Serikali yake eti inaambiwa kuchunguza mafisadi wa BOT hivi hapa unategemea nini sasa ndio maana unaona vijana na watoto wote wa wakubwa wanaitumia ile kampuni kama njia yao ya ajira lakini ukweli ni kwamba ni ili wale kile ambacho wazazi wao wamewatengenezea !

Masha ni mtu wa kulipa fadhila tu kwani anatumiwa na wakubwa ndio katika kula huko mahela ya BOT akampa hata sehemu ya fedha kwa Mtangazaji wa Redio na Mchora katuni Masoud Kipanya ili afungue lile duka lake la nguo pale Milenium Tower na kama mtakuwa mnakumbuka ndiye yeye aliyefungua eti yale mavazi ya KP wear na kuwasifu wale vijana ambao wanajiairi eti ni wajasiria mali wa kuigwa na kupigiwa mfano hivi anadhani kuwa Watanzania ni wajinga sana eeenhh ! Ngoja tu tunyamaze ila iko siku Bubu ataongea na Kenya ya pili italipukia Kinondoni !
Endeleeni kudanganyika tu !
 
Ujumbe huu ni mzito sana .Nautafakari maana JF bwana ina mambo mazito na utulivu unatakiwa sana.
 
mugishagwe wakati mwingine ukisubiri utulivu utakuta
ukenya ushaingia kwenye damu na kuchukua muda kutoka na hivyo
kuathiri jamii hivyo angalia pia na ukimya wako muda ni mzuri sana
 
jamani Members ..hivi Watu Wengine Mkoje ..inakuwaje Unaazisha Thread Mpya Wakati Haya Unayoyasema Yapo Tayari Kwenye Thread Ya Rizwan/masha...au Mnaona Sifa Tu Kuanzisha Thread...mbona Kuna Mengi Ya Kuongelea.....nashauri Kabla Ya Kuanzisha Thread Tuangalie..

Mods

Mnaonaje Hii Ikiunganishwa Na Ile Ya Kwanza...?
 
Jamani, hata Kipanya naye ameshaingia kwenye list ya benefactors wa ufisadi? Kabaki nani sasa!
 
Kipanya Masoud? How? Im lost pls help me...

Masatu umepotea ? Njoo nikushike mkono .Kipanga kaingizwa ki aina sasa tumia muda kusoma utaona madai ya mkuu ambayo ni connection ya Masha na jamaa ambaye alimwita mjasiriamali
 
My mind iko convinced kabisa kwamba Masha ameshiriki in a way or another kufacilitate ufisadi. Sina uhakika kama alifanya huku akiwa anajua au hajui. Lakini amabayo hainiingi akilini ni kale kaduka ka kipanya,KP kwamba eti masha alichomoa fweza ya ufisadi kumsaidia KP kuanzisha. Vp kuna evidence zaidi ya kupiga mkasi siku ya ufunguzi.

Maana kama ni hiyo tu basi hata mzee wa mikasi (MS) inabidi tuanze kuwa na wasiwasi naye!!!!!!!!!
 
Masatu umepotea ? Njoo nikushike mkono .Kipanga kaingizwa ki aina sasa tumia muda kusoma utaona madai ya mkuu ambayo ni connection ya Masha na jamaa ambaye alimwita mjasiriamali

Uzee unanijia haraka nipo kama sipo....
 
Ndugu zangu Watanzania !
Mara ya mwisho kuwaandikia kuhusu lile sakata lilopelekea kifo cha Dr, Omary Alli Juma ,nimefurahi kuwa jamaa wengi na hasa wasomi tu wazuri wame jibu kwa kukurupuka kwani kama wangekuwa ni wafuatiliaji wazuri wa mada husika wangeunda kile kitu kiitwacho Facts Finding Mind katika vichwa vyao na sio kulalama oooh jamaa hayuko seriously kwani wanataka umakini gani tena kunako hili !

Sasa hili la Waziri masha nalo nadhani kuna mamluki wameingilia hii fani ili kujaribu kupotosha ukweli na hawa ni wale wasio na akili either wanafanya kwa makusudi ama kwa kutumwa na makubwa wao kuwa nendeni mkatibue mada ili tu kupotosha ukweli na vitu kama vile sasa sijui hapa kwa Masha watasemaje ?

Masha ile kampuni yake ilitumiwa tu na CCM ili kuchota yale Mabilioni ya BOT kusema kuwa alitumiwa na CCM namaanisha kuwa ile DEEP GREEN FINANCE LTD ni kampuni ya CCM amabyo ndio iliyopewa tenda tena na serikali eti kupeleka bomba la mafuta kule Mwanza hebu niambie Serikali ya CCM na kampuni ya CCM ila sasa lengo halikuwa kupeleka Bomba la mafuta ila ni kuchota yale Mafedha ya BOT kwa ajili ya kampeni ambazo ndio zilichangia kumweka JK katika madaraka ambayo ndio hiyo hiyo Serikali yake eti inaambiwa kuchunguza mafisadi wa BOT hivi hapa unategemea nini sasa ndio maana unaona vijana na watoto wote wa wakubwa wanaitumia ile kampuni kama njia yao ya ajira lakini ukweli ni kwamba ni ili wale kile ambacho wazazi wao wamewatengenezea !

Masha ni mtu wa kulipa fadhila tu kwani anatumiwa na wakubwa ndio katika kula huko mahela ya BOT akampa hata sehemu ya fedha kwa Mtangazaji wa Redio na Mchora katuni Masoud Kipanya ili afungue lile duka lake la nguo pale Milenium Tower na kama mtakuwa mnakumbuka ndiye yeye aliyefungua eti yale mavazi ya KP wear na kuwasifu wale vijana ambao wanajiairi eti ni wajasiria mali wa kuigwa na kupigiwa mfano hivi anadhani kuwa Watanzania ni wajinga sana eeenhh ! Ngoja tu tunyamaze ila iko siku Bubu ataongea na Kenya ya pili italipukia Kinondoni !
Endeleeni kudanganyika tu !

Duuh!

:confused:
 
Waziri azomewa na wasomi

2008-03-17 08:55:43
Na Juma Ng\'oko, PST, Mwanza

Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Lawrence Masha, ameonja joto ya jiwe baada ya kuzomewa na baadhi ya wahadhiri pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) cha jijini Mwanza.

Alizomewa baada ya kujikanganya kuitetea serikali kufuatia hoja iliyotolewa na mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) Bw. Zitto Kabwe, iliyozungumzia usiri kwenye mikataba ya madini na namna ambavyo wananchi hawafahamu juu ya ukweli wa madini yao.

Mada iliyowasilishwa na Bw. Kabwe ilielezea mafanikio pamoja na matatizo mbalimbali yanayoikabili sekta ya uchimbaji madini.

Bw. Kabwe tofauti na Waziri Masha, aliingia ukumbini saa 6:41 mchana na kushangiliwa, alisema pamoja na mapungufu mengine serikali haiko wazi katika kutoa taarifa zinazohusu pato wala mikataba ya madini.

Waziri Masha alizomewa hadharani kwenye mjadala aliposema serikali iko wazi katika kutangaza masuala mbalimbali yahusuyo madini.

Alisema Watanzania wasioelewa kuhusiana na mikataba hiyo ya madini ni wale wenye uelewa mdogo na ama hawasomi magazeti au hawasikilizi redio.

Alitoa maelezo kwenye kongamano ambalo alikuwa mgeni rasmi lililoandaliwa na SAUT ambapo pamoja na mambo mengine, alishiriki kwenye mdahalo kuhusu uimarishwaji sera ya madini, kilimo na uvuvi kuelekea katika uboreshaji wa mali asili nchini.

``Kama nilivyotangulia kusema, Mheshimiwa Kabwe ni rafiki yangu. Ila ninachotaka kusema ni kwamba siyo kweli kwamba watu hawasomi magazeti na hawasikilizi redio wakati serikali inapokuwa inatangaza masuala mbalimbali yanayohusu mikataba,`` alisema Bw. Masha na kuanza kuzomewa.

PST ilikuwepo na ilishuhudia Bw. Masha akizomewa mchana saa 7:52 wakati akijaribu kufafanua mada hiyo.

Mbunge huyo alisema kuwa karibu Watanzania wote wanaamini kwamba pato la taifa kutokana na sekta ya madini ni asilimia tatu kwa mwaka lakini bila kuwa na ufafanuzi wowote.

Bw.Kabwe ambaye pia alikuwa mgeni mwalikwa kwenye mdahalo huo alisema kuwa hali hiyo imesababisha wananchi washindwe kuamini kwamba taifa linafaidika na sekta ya madini, kwa vile mikataba na pato litokanalo na madini ni siri ya viongozi wa juu serikalini pamoja na wawekezaji wenyewe.

Alisema wananchi wanaoishi jirani na migodi hiyo hawafaidiki na madini hayo na kwamba wengi wao wanaishi chini ya pato la Sh. 1,000 kwa siku.

Alitoa mfano kwamba tafiti zinaonesha kwamba Wilaya ya Geita mkoani humu, ndiyo ilikuwa ya mwisho mwaka 2005 kwa umasikini wa kipato kitaifa.

`` Kwa mfano, takwimu zinaonyesha kwamba mwaka 2005 Geita ndiyo ilikuwa wilaya ya mwisho kwa umasikini miongoni mwa wilaya zenye madini ambapo asilimia 62 ya wakazi wake waliishi chini ya Sh.1,000 kwa siku,`` alisema Bw. Kabwe.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom