Waziri Kombani Ndani Ya Sakata La Jerry Muro

ndio hivyo manake hata mkuu wao naye ni hivyo hivyo tu.
watanzania---endeleeni kucheka na nyani ili hali tayari mmeshaanza kuvuna mabua..itafikia staji hata mabua yatakuwa hamna..nayo yataliwa na nyani..
 
Kombani130508.JPG


Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Waziri mpya wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani leo Ikulu Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo. (Picha na Mroki Mroki).

Source: http://kennedytz.blogspot.com/2008/05/blog-post_8198.html
 
Duh sasa dhamana ya nchi yetu tumpe nani kama mawaziri pia wanahusika katika kuhujumu nyanja mbalimbali za kuleta maendeleo nchini? Hii ni hatari kubwa, watanzania tunakoelekea ni kubaya sana!
 
Tumeyasema sana humu. Sema huu ni mfumo uliokomaa sana. Ulianzishwa na CCM kuchangiwa na taasisi za UMMA. Hamjawahi kushtukia utajiri mawaziri wetu unatokana na nini muda mfupi baada kushika nyadhifa hizi? Mchezo huu pia unazikumba PCCB, TISS ndio maana ni vigumu mno kuudhibiti.

Mkuu,

Bahati mbaya sana ni wachache wanaoona tatizo lilipo. SIASA na MFUMO batili wa kujitawala.

Naamini kama tungeweka SIASA pembeni na kueka mfumo thabiti wa kujitawala, mambo kama haya yasingejitokeza.

Hao law enforcers wenyewe ni waganga njaa na slaves wa genge la watawala. They are not autonomous kwa sababu MFUMO wenyewe umeegemea kwenye maamuzi ya wanasiasa.

Tuendelee kuugulia maumivu mpaka kitakapokuja kizazi chenye daring power.
 
I wish viongozi wote wanaokuwa na tuhuma za ufisadi wakae kando ya nyadhifa zao kupisha uchunguzi.
 
Halafu kuna taasisi inasema imefanya tafiti zake na kuwa zaidi ya 70% ya waliotoa maoni wanasema wanaimani na serikali ya CCM ambayo inaongozwa na mawaziri wa aina hii. Mirembe Hospital ipanuliwe maana wengi tunahitaji kupelekwa huko kupimwa.
 
Mkuu una hisa nae nn?


Sina hisa naye Fidel80 lakini mnamuonea tu . . . . LOL

Hata mahakama haijasema, mnamuonea tu Mkuu, hata Chenge, Lowassa, Rostam nk. wote mnawaonea . . . mahakama hazijawahukumu ati . . . .

Hata hoja ya mgombea binafsi pia mnalazimisha . . . Mahakama ya Rufaa bado haijaamua . . . . . haaa haaa . . .

Tanzania zaidi ya uijuavyo . . . . lakini mambo ni shwari tu, AMANI, MSHIKAMANO NA UTULIVU . . . . Karibuni Wawekezaji.
 
Back
Top Bottom