Waziri kivuli wa Afya yuko likizo?

wimbi la mbele

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
647
266
Hivi waziri kivuli wa Afya wa Tanzania yuko vakesheni?

haya mambo yanayoendelea ya madaktari na Ulimboka nilitegemea wangekuwa wanatoa taarifa mbali mbali na misimamo lakini wako kimya

Hivi kweli hawa CHADEMA kama wana behave kama CCM kweli tutafika?

Tofauti ya hawa CHADEMA ni nini?
 
Wakuu huyu Waziri kivuli yupo kazini. Ukiisoma taarifa ya Zitto aliyoitoa leo, amemuagiza aende na afatailie hili swala kwa ukaribu na arudishe taarifa rasmi ndani ya chama. Ngoja niitafute ile taarifa nikuwekee mkuu.

Zitto na Demokrasia
Dr. Ulimboka kutekwa, kupigwa na kuumizwa: Serikali inawajibika kutueleza

Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI
‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous’

Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.

Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.

Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa ‘agente provocateure‘ kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.

Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.
Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all’
Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.

Written by zittokabwe
June 27, 2012 at 12:12 PM
 
Mnataka naye wamuulimboke? Subiri ripoti toka kwa kova atakapokuja na majibu mepesi tu kwamba Dr alitekwa na KIKUNDI CHA WAHUNI WACHACHE WALIOKUWA na lengo la kumdhuru
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom