WAZIRI Kivuli Azuia uchimbaji wa almasi eneo la shule, zahanati zinafanya na diwani CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
WAZIRI Kivuli wa Ujenzi Salvatory Machemli (Chadema), amepiga marufuku uchimbaji wa madini ya almasi katika eneo la shule ya msingi na zahanati ya Maganzo, kata ya Songwa, wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, unaodaiwa kufanywa na diwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kuanzia sasa mtu atakayebainika kuchimba madini katika maeneo ya shule na zahanati hiyo, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kukamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yake bila kujali cheo alichonacho.
Machemli ambaye pia ni mbunge wa Ukerewe, aliyasema hayo hivi karibuni wakati alipokuwa akihutubia wakazi wa Maganzo, kwenye mkutano uliotanguliwa na maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika katika mji wa Maganzo.
Waziri kivuli huyo amelazimika kupiga marufuku uchimbaji huo wa madini katika maeneo ya taasisi za umma baada ya wakazi wa Maganzo kulalamikia kitendo hicho kwenye mkutano huo wa hadhara.
"Huyu diwani anayechimba madini eneo la shule na zahanati aache mara moja kuchimba maeneo hayo, na akiendelea tutamkamata na kumshtaki mahakamani.
"…Hatutaki kuona tena kero kama hii; aende kule Mwadui akachimbe almasi na si maeneo ya shule na zahanati, ole wake akiendelea kuchimba ataiona nguvu ya umma," alisema Machemli.
Awali alihoji sababu ya diwani huyo ambaye hakutajwa jina kuendesha uchimbaji huo wa madini kwenye maeneo ya zahanati na shule ya msingi wakati viongozi wapo na hawachukui hatua; na kusema, "Huu ni udhaifu wa serikali ya Kikwete." Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum Rebecca Mngodo (Chadema), aliwataka wananchi hao kumkamata diwani ama mtu yeyote atakayeonekana akichimba almasi maeneo ya shule na zahanati, kwani maeneo hayo yanapaswa kulindwa na si kuharibiwa kwa lengo la mtu kujipatia manufaa binafsi. Mbunge huyo wa viti maalumu, Rebecca, alikwenda mbali zaidi na kusema, "Umaskini unaowakabili wakazi wa Maganzo na Tanzania kwa ujumla unasababishwa na uongozi mbovu wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete."
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom