Waziri Kigoda na kutetea ubinafsishaji mbovu wa viwanda Tanzania

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,087
450
kwenye majumusiho ya bajeti ya viwanda na biashara, waziri kigoda , nimemwona akitoa majumuisho ametetea wawekezaji waliobinafishiwa, kuwa viwanda vya korosho tanzania vimeshindwa kuendelezwa kwa sababu ya mitaji midogo na tekinolojia kubadilika.swali, je wakati wa kubinafisha, serikali haikuwa na uchambuzi wa mwekezaji kama ana uwezo wa mtaji?ikumbukwe karibu 3/4 ya viwanda vya korosho, vimebinsfishwa kwa wawekezaji wa ndani , na miongoni mwao ni vigogo kama mke wa BEN MKAPA, je hoja hii ya mitaji midogo ina mashiko?
 
Na ndiyo makosa tutakayofanya 2015 kurudisha sura zile zile!! Hakutakuwa na jipya zaidi ya kuendelea na kulalamika hadi tutakapoanza kutumia nguvu. Hawa jamaa wamejipanga, sisi tunataka mabadiliko lakini hatujajipanga!!
 
Huyu bwana ndo alikuwa kinara wa kuvibinafsisha usitegemee tofauti na hayo aliyosema.
 
wakati wa ubinafsishaji yeye ndo alikuwa waziri,sasa leo hii ajikaange mwenyewe?
 
Huyu fisadi mzoefu tu na sasa amerudi tena baada ya kuona yale mafungu ya rushwa alizotunukiwa wakati wa ubinafsishaji yameisha,akamuomba bwana mdogo ampe shavu tena.
 
Back
Top Bottom