Kichankuli
JF-Expert Member
- Dec 18, 2008
- 887
- 189
Waziri, wa Masuala ya Muungano, amejiandaa kuongea na vyombo vya habari kwaajili ya kuhimiza Taasisi na Makampuni mbalimbali kuchangia katika sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Cha kushangaza ni pale ombi lake la kwanza kwa makampuni ya simu linaangukia kwenye kampuni ya simu ya Mobitel ambayo haipo tena katika ulimwengu wa biashara ya simu. Lakini kibaya zaidi ni kwa Waandishi aliokuwa akiongea nao kushindwa kumsahihisha, sijui na wao hawakugundua au la, kosa hilo na kwenda kurusha habari hiyo hivyohivyo kwa wananchi.
Hapa ndipo linapojitokeza suala la kutokuwa na umakini kwa vyombo vyetu vya habari. Inakuwa ni kama wanakopi na kupesti. Tofauti na wenzetu wa nchi za magharibi, mathalani, kumbuka namna Wanahabari wa Marekali walipoujulisha umma wa Wamarekani juu ya Hilary Clinton alivyoshindwa kukumbuka jinsi alivyotembeleaBosnia; walimpa fact na kumaliza uzia.