Maarifa
JF-Expert Member
- Nov 23, 2006
- 4,568
- 2,911
Hili swala la viongozi wenye Shahada za kusuka liliwahi kujadiliwa hadi bungeni; Kama sikosei mheshimiwa Shelukindo ndiye aliyeanzisha mjadala huo na waziri Msola akaahidi kulishuhulikia lakini mpaka leo kimya!! Inaelekea wanamtandao ndio wengi wenye vyeti feki ndio maana hatua hazichukuliwi ipasavyo ukianzia na Nchimbi, Lukuvi, Makongoro. David Mattayo, Mzindakaya , Masaburi , Nangale etc. Jambo la kusikitisha ni kwamba usanii wetu tumeupeleka mpaka kwenye E.A. legislative assembly ambako wabunge wa wenzetu ni wasomi kweli kweli na ndio maana wanasema ukihiyo wetu ndio unatufanya tuogope soko la ajira Afrika Mashariki lisiwe huru !! Hii ni aibu, ni vizuri vyeti vya waomba uongozi mwaka 2010 vikahakikiwa na competent authority kabla ya kuruhusiwa kugombea ili tuondokane na aibu hii.
Lukivi wakati fulani alialikwa mahala fulani na watu fulani(watasha) alijikanyaga kutoa just speech ya vote of thanks. Akanirushia wakati huo mie nikiwa undergraduate pale mlimani Dr Huyo.