Nkoboiboi
JF-Expert Member
- Oct 9, 2010
- 243
- 63
"Haumwi kama watu wanavyodhani, ni kwamba amejiskia vibaya kama watu wengine wanavyoweza kujiskia na hivyo amekwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi" hii ni kauli ya Naibu Waziri Kijana wa viwanda na biashara ndg Razaro Nyarandu alipoulizwa juu ya afya ya Bosi wake Dr Chami.
Hapa ninajiuliza maswali kadhaa!
Mosi, hivi Nyarandu anaposema anajiskia kama wanaweza kujiskia watu wengine, je hao watu wengine wakijiskia nao waende India?
Pili, hapa kwetu hakuna madaktari wa kufanya uchunguzi wa mtu akijiskia kawaida?
Tatu, anataka kutuambia kodi zetu zimewafanya wajisahau namna hiyo hata kama mtu akijiskia ugonjwa wa kawaida akafanye vipimo nje ya nchi?
Nne, inamaana viongozi wa nchi hii wanajua udhaifu wa hospitali zetu na hivyo hawaamini kuzitumia hata pale wanapojiskia kuumwa kawaida tu?
Kwa mbwembwe hizi za wabunge wetu.....!!!!! Naomba wataalamu wa mahesabu wanijuze ni lini kikao cha ngapi cha Bunge la Tanganyika kitafanyika 'hospitalini' India.....!!!!!!