Waziri Chami nae kalazwa India

Status
Not open for further replies.
It is very cheap but with excellent matibabu.
"It is very cheap" ndio nini, kwa elfu hamsini nitapata safari ya "uchunguzi zaidi"?

Malyamungu, kwa Mtanzania wa kawaida huwezi kumwambia kwenda India ni "it is very cheap." Kuna watu vijijini ambao ukiwaambia waje Dar kutibiwa watasema sina nauli! Nauli ya Dar Express hana unamwambia kwenda India "it is very cheap"? Stop being ridiculous.
 
Serikali inatakiwa kujiuliza ni kwa nini watu wengi especially viongozi wa serikali wanakwenda India aidha kwa matibabu au uchunguzi wa afya. Wakishapata majibu wanatakiwa kuyafanyia kazi, kama ni kununua vifaa zaidi, kusomesha watu kutumia hivyo vifaa badla ya kutumia fedha za walipa kodi ambao hata hawapati huduma nzuri pale Muhimbili wakati wakubwa wanaenda nje ya nchi.
 
get well soon abc.jpg

Kila la kheri Mkuu.
 
Kwa hivyo siku akijisikia vizuri ndiyo ataenda Muhimbili. Waboreshe hospitali za hapa nchini kila mtu atibiwe hapa hapa Bongo.
 
duh, hii kali sasa! India, Jamani India, Kunani kulee eh ., India, India, Kunani kulee eeh! India india
 
Mi wasi wasi wangu kuhusu wagonjwa walioko huko muda mrefu, inabidi wakae mkao wa kujilinda zaidi maana huwezi kujua hawa wagonjwa wapya ni kweli wagonjwa au wanaenda kwa kazi maalumu.

Nchi inahitaji mabadiliko ya lazima hakuna options!! we need the changes, na wazungu walishaona kipindi hiki ndo watuvune haswa mpaka tutoboke mifuko. Utasikia serikali imekopa, mara dharura, mara kampuni la kimarekani mara NGOs hadi machozi ya damu yatutoke.

Kwenye red hapo! It is a very good observation, ukizingatia Dr Mwakyembe ameahidi kuweka kila kitu hadharani kuhusu Richmond na Dowans akirudi salama!
 
Kodi zetu hizi watatibiana wao tuuuuuuuu jamani jamani tutaonana wabayaa kila mtu india mie naenda hosptali za kulipia mitaani nyie endeleeni tu

Hivi kwanza hospt zetu za Rufaa haziwezi kutibu magonjwa yao au ndio kutuashiria jinsi huduma za hospt zetu zimeoza?
 
wakuu huyu jamaa chemi haumwi, nasikia katumwa na kile kikundi cha mauwaji cha ccm kwenda kuwamaliza mwakyembe na Prof mwandosya. angalizo kwa mwaky na mwandosa huyu jamaa asifike hospital mlizolazwa atawamaliza wala asiwakaribie hata kidogo anasumu kali sana ya kuwamaliza.

Wewe Kama sio mchawi basi ...umetoka familia ya kichawi...sorry to say that.....

.....katika mawaziri waadilifu ,chami ni mmoja wao...hapendi Makuu,...haabudu fedha wala utajiri...ni waziri kijana ..below 40...Ambaye anaweza kuwa hazina ...tumuombee apone...

Napata mashaka...idadi ya mawairi wa Jk Wenye matatizo ya kiafya kuelekea 2015 inazidi kuongezeka....sijui ni balaa gani hili......
 
nadhani kuna viongozi chini ya 5 wamelazwa huku India nzima. Kuna watanzania wengi sana wamelazwa huku wafanyakazi wa taasisi mbalimbali, wengine kutoka mikoani na raia wa kawaida ndio wanapata matibabu India. Mzee alikuja baada ya ushauri wa madaktari Muhimbili, ambao tunawashukuru sana kwa ushauri huo.
 
Basi tufungue Serikali Ya Jamuhuri Ya Wadanganyika Tawi La India
 
Kwa nini wao wanakimbilia nje wakiumwa? Hii ina maana madaktari wa hapa Tanzania hawana uwezo.
 
Hapa kuna ka mchezo kanachezwa tuwe makini. Tukumbuke kwenye bajeti ya kila wizara kuna kifungu cha matumizi mengineyo matibabu ya waziri na naibu waziri yakiweno. Matibabu ya nje ya nchi ulaji kwa waziri ni mkubwa pia. Mwisho wa cku hela iliyotengwa inaonekana imetumika sawasawa otherwise inabidi irudishwe hazina. Tuamke toka usingizini.
 
jamani kuweni kuweni na HURUMA hata kidogo basi ikibidi. sote sisi ni wagonjwa!

kama viongozi wameamua kuwa wanyama na mimi sasa nitakuwa zaidi yao.myaone haya ndiyo majitu kupe wanadhani india ndiko kuna uhai labda mh ajui maana ya medical check up anadhan ni ugonjwa ambao tiba yake ipo india
 
] Mi wasi wasi wangu kuhusu wagonjwa walioko huko muda mrefu, inabidi wakae mkao wa kujilinda zaidi maana huwezi kujua hawa wagonjwa wapya ni kweli wagonjwa au wanaenda kwa kazi maalumu.[/COLOR]

Nchi inahitaji mabadiliko ya lazima hakuna options!! we need the changes, na wazungu walishaona kipindi hiki ndo watuvune haswa mpaka tutoboke mifuko. Utasikia serikali imekopa, mara dharura, mara kampuni la kimarekani mara NGOs hadi machozi ya damu yatutoke.

Hapo kwenye red, mmhhhhhh, makubwa!!!!! Yetu macho na masikio na matokeo ya hizo special assignment zinazofikirika. Inanikumbusha motto ya cinema za James Bond 007 za enzi zile 'Licenced to Kill'
 
nadhani kuna viongozi chini ya 5 wamelazwa huku India nzima. Kuna watanzania wengi sana wamelazwa huku wafanyakazi wa taasisi mbalimbali, wengine kutoka mikoani na raia wa kawaida ndio wanapata matibabu India. Mzee alikuja baada ya ushauri wa madaktari Muhimbili, ambao tunawashukuru sana kwa ushauri huo.

Tupo nanyi kwenye sala......kuanzia mzee Mwandosya ,mwakyembe, na sasa chami......tunamuomba Mungu awajalie warudishe....wote magonjwa Yao yanaendana endana....

Pia tuiombee serekali yetu ya mh KIkwete .....ili naye apate kusamehewa.....makosa hasa yaliyotokana na pilika na siasa chafu za mwaka 2005....na kuendelea....ili balaa zisiwapate wasiohusika.....au dhambi zisizae dhambi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom