Waziri atajwa kupewa kontena la baiskeli kabla ya uchaguzi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Waziri atajwa kupewa kontena la baiskeli kabla ya uchaguzi
Send to a friend
Tuesday, 05 July 2011 20:17
0digg

maige%20ezekielwaziri.jpg
Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige

Ramadhan Semtawa, Dar
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, ametajwa kupewa kontena la baiskeli za walemavu kupeleka jimboni miezi minane kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana.Akizungumzia utekelezaji dhana ya utawala bora wakati akichangia bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa Ofisi ya Rais (Utumishi, Utawala bora, Uratibu na Uhusiano wa Jamii) bungeni jana, Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habib Mnyaa, alisema kontena hilo alipewa Febuari 2, mwaka jana.

Kwa mujibu wa Mnyaa, kontena hilo ambalo lilitolewa na Asasi isiyo ya kiserikali ya Unit Diversity Foundation (UDF), inaacha maswali mengi katika dhana nzima ya usimamizi na utekelezaji wa misingi ya utawala bora.

Mnyaa alifafanua kwamba, asasi hiyo yenye makao yake makuu Dar es Salaam imekuwa ikitoa misaada ya baiskeli kwa walemavu na kuongeza kuwa, ni asasi isiyofanya biashara, hivyo kuhoji waziri kupewa kontena zima.

Waziri Maige alipopigiwa simu jana ili kupata ufafanuzi wa kitakwimu kujua idadi ya walemavu waliopo jimboni kwake kulinganisha na idadi ya baiskeli kwenye kontena hilo, simu yake ya kiganjani iliita bila majibu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi (SMS), hakujibu.
Lakini, Mnyaa katika kuweka bayana hilo, alisema hata aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mufundi, mkoani Iringa, hadi Februari mwaka jana naye alipewa kontena kama hilo.

Mbunge huyo alienda mbali kuwa, baadhi ya mawaziri wamekuwa wakitumia ushawishi wao kuomba misaada katika asasi mbalimbali kwa nadharia ya, "Nipe ni kupe."
"Sisi wabunge wa kawaida tukienda kuomba misaada katika mashirika au kampuni mbalimbali hatupewi mikubwa, lakini mawaziri wanakwenda kwa nyadhifa zao na kupewa misaada mikubwa, hii inaondoa dhana nzima ya utawala bora,” alisisitiza.

Hata hivyo, alitetea asasi hiyo akisema inafanya kazi nzuri kusaidia walemavu na kwamba, hivi sasa inakabiliwa na ukosefu wa Sh58.5 milioni kwa ajili ya kutoa makontena mawili ya baiskeli bandarini.

Mnyaa alifafanua kwamba, asasi hiyo ambayo watendaji wake wamepiga kambi Dodoma imeonyesha nia ya kusaidia baiskeli tatu kwa kila mbunge kwa Sh50,000 baada ya kufanikiwa kuondoa kontena hilo.



 
[h=4]Comments [/h]


0 #6 kidongo 2011-07-06 17:33 Tatizo ndugu yangu ni utaratibu na muda uliotumika kutoa msaada. Yaani asasi impe kontena mbunge waziri mtarajiwa halafu wakati wa kampeni!? hapa lazima mtoaji anategemea malipo fulani. Pia anaua dhana nzima ya uchaguzi huru!. Bado tutasikia n waliopewa maboksi ya kondomu kupeleka majimboni! Yetu macho na masikio!
Quote









+1 #5 Mtanzania 2011-07-06 12:43 Tunaomba waandishi mfanye utafiti japo kidogo kukamilisha habari mnazoandika. Waziri kupewa kontena la baiskeri za walevu na kuwapelekea wananchi wake siyo tatizo kwa upande wangu. Muhimu mngetueleza kama kulikuwa na "nipe nikupe" aliyoisema mh. Mbunge. Huyu waziri anahusika na usimamizi wa maliasili zetu sasa mngetueleza kuwa hao waliompatia baiskeli wanafanya biashara zinazonufaika na ukaribu wao na waziri hapo lingekuwa tatizo. Mkiwajua na kutueleza UDF ni akina nani basi jamii ya watanzania itapima madhara ya hilo kontena la baiskeri. Pokeeni misaada pelekeni kwa wananchi huku mkitekeleza majukumu kwa misingi na maadili ya kazi. Ufisadi iwe mwiko. Tanzania itasonga mbele.
Quote









+3 #4 Beano 2011-07-06 12:17 Misamaha ya kodi kwenye madini inawezekana lkn msamaha wa kodi kwa kontena la baiskeli za walemavu haupo?

Lkn na hii asasi ina haja gani ya kugawa hizo baiskeli kupitia kwa wabunge ilhali ikijua kwamba hiyo ni sawa na kuvaa sura ya kisiasa. Huu si utaratibu sahihi wa kuwafikia wananchi kwani watabeba sura ya kwamba mbunge wao ndio mwezeshaji wa msaada huo.
Quote









+2 #3 Anko Sam 2011-07-06 11:51 Ukifuatilia kwa ndani si ajabu ukakuta ni asasi ya kigogo serikalini! Asasi hizi zinatumiwa na mafisadi kufanya ufisadi kwa kivuli cha kutoa misaada!
Quote









+1 #2 Innocent 2011-07-06 07:48 Quote:
Do kaz kweli kweli !!! mambo ya wakubwa ni mengi na ya aibu sijui kesho nini tena tutaambiwa manake kila siku ina kashfa yake​

Kashfa zitaendelea hadi siku ya mwishooo... walishazoea kufanya ma dudu..
Quote









+2 #1 Mchangiaji 2011-07-06 05:16 Do kaz kweli kweli !!! mambo ya wakubwa ni mengi na ya aibu sijui kesho nini tena tutaambiwa manake kila siku ina kashfa yake.
Quote







Refresh comments list

[h=4]Add comment[/h] Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!
 
asipojibu hizi tuhuma ndani ya siku tatu basi ijulikane kuwa amekiri dhambi hizi dhidi yetu..................................hatutahitaji ushahidi mwingine tena..........
 
huyu waziri siyo kabisa ana ujanja ujanja sana siata kwenye kamati ya zito kabwe alimkuta na makosa mengi sana yakuliinguzia taifa hasara baada ya kutumia wazifa wake kupunguza kodi uko tanapa
 
Ngoja kwanza, Hivi baiskeli za walemavu nazo zinalipiwa KODI? Tafadhali mwenye jibu anijuze.
 
Back
Top Bottom