Waziri apanda kizimbani: ...Kisa cha SANGAM SECURITAS!

Mzee Mwanakijiji, heshima mbele. Mzee nimekukubali na umekubalika. Kalamu imeshikika, taaluma, kipaji na uwezo wa uandishi ndio mahali pake na mwanga wa kisheria pia umesimama!.
Jana nilimsikiliza huyu Mhe. akijifagilia pale Clouds,nikasema bado hajakutana na waulizaji maswali. Japo sijaweza kuacess padomatic yako (Nokia E 90 bure kabisa), nakiri wewe ni muulizaji maswali mahiri. Mtafute Masha umkamue tuupate ukweli.
Pia nakushauri, fanya mawasiliano na vituo vya Radio home ili zile live zako, ziwe live broadcsast home na wengi tufaidike.
TBC wako mbioni kuanzisha live interactive programs. Tayari wameanza na Dar- Dodoma wakati wa Bunge na Dar-Arusha wakati wa Sullivan. Baada ya kuilink mikoa yote, watalink na EAC na hatimaye Global na hapa ndipo tutaweza kuipata michango halisi ya wenzetu mlio nje katika ujenzi wa Taifa letu.
Asante Mzee Mwanakijiji.
 
Mzee Mwanakijiji heshima mbele mkuu. Ningewashauri vijana wanaosomea sheria katika vyuo vyetu na mawakili wajitahidi kufuatilia ubunifu wako ili waweze kujifunza jinsi ya kuuliza maswali mahakamani mpaka mtuhumiwa anajifunga kamba mwenyewe kama MADUSHA alias Masha anavyojitundika mwenyewe kwa kushindwa kujibu namna alivyowasilishiwa malalamiko na wakola wake wa Sangam!! Mkuu kwa mara nyingine tena hongera na endeleza ubunifu wako ili nasi tuambulie angalau kidogo humo humo.
 
ngosha,

nakupaga mapongezi marefu kama mabugando ya maminara mapacha ya daslam

NB: Muulize huyo waziri kuwa hivi yule kaka (sijui baba yeake mdogo) anayevuka kila siku kutoka Kamanga ferry kwenda Mza mjini na kushinda tu Mza Hotel kaacha utapeli wake? Au na waziri ndio kaanza kufuata nyayo?
 
Mwandishi kanjanja..


kuna sehemu umetaja jina la masha na juu umedanika jina lingine.Mkapa alishamaliza kusema zamani,kuna baadhi ya watu wana wivu wa kike,yaani mtu bila sababu tu anaazalkuandika habari ya kufikirika bila hata ya kuwa na soni
 
Mwandishi kanjanja..


kuna sehemu umetaja jina la masha na juu umedanika jina lingine.Mkapa alishamaliza kusema zamani,kuna baadhi ya watu wana wivu wa kike,yaani mtu bila sababu tu anaazalkuandika habari ya kufikirika bila hata ya kuwa na soni

Naomba kurudia tena,

Labda ni mtazamo na matatizo yangu binafsi, lakini wivu juu ya uwezo wa mtu kwa kitu ambacho si nje ya mwili, yaani anacho kichwani, mikononi, miguuni au sehemu yoyote katika mwili si kitu chema wala cha kufurahia. Maana hata ukifanya vipi huwezi hata kuongeza urefu wa hata nywele yako.

Lakini kwa upande wa pili, wivu juu ya vitu vipatikanavyo nje ya mwili yaani magari, website au mali kwa ujumla si mbaya sana maana ukiutumia vema unakuletea maendeleo.

Nisivuruge mada, natanguliza samahani, huu ni mtazamo tu!

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-dr-tarab-wafanyiwa-umafia-13.html#post370774
Pongezi Mwanakijiji
 
hii tuifanye screen play jamani ni bonge ya movie naona kama ile ya Few Good Men
 
Mwandishi kanjanja..


kuna sehemu umetaja jina la masha na juu umedanika jina lingine.Mkapa alishamaliza kusema zamani,kuna baadhi ya watu wana wivu wa kike,yaani mtu bila sababu tu anaazalkuandika habari ya kufikirika bila hata ya kuwa na soni


Gembe

Bila sababu?!, real?

Tatizo liko wapi? Kutaja jina au wivu?
Labda mie ninakusoma kinyumenyume! Vinginevyo wenzako tumefurahia na kujifunza kutokana na utunzi huu wa kufikirika. Kwamba inakuwa hivi wakati wa baridi na je wakati wa joto?

Big ups Mwanakijiji. Thanks.
 
Mwanakijiji kiboko....duuuu!! KWANINI HII kitu usiiweka kama kajitabu ili iwe kumbu kumbu hata kwa vizazi...Good work great thinking

Masa
 
Kweli sheria msumeno katika nyakati fulani fulani, Masha ni mwanasheria lakini mwanasheria mwenzie bongo kamchezesha kidedea katika dakika chache tu, akapanick na kujibu kwa hasira, hapo kimbembe anacho.
Hii inaonyesha, kuwa kuna 'KUNA NURU GIZANI'
 
Waziri Valentino Madusha alishtakiwa kwa kuingilia mchakato wa utoaji na upatikanaji wa tenda ya kuchapisha vitambulisho vya Raia. Katika kesi iliyovutia Taifa Waziri huyo alisimama kizimbani kuhojiwa na upande wa mashtaka kuelezea nafasi yake na hasa jinsi alivyoitetea kampuni ya SANGAM SECURITAS: Mahakamani ilikuwa hivi katika siku ya kwanza.

Waziri alikuwa amevaa suti kijivu yenye michirizi midogo sana ya rangi nyeusi, alivaa shati la rangi ya bluu nyepesi na kwenye shingo yake alitinga tai ya rangi nyekundu iliyowiva. Miwani yake yenye rangi ya redha ilimfanya aonekane kama profesa fulani wa vile vyuo vikuu vya watu weusi kule Marekani ambako alisoma. Mwendesha mashtaka alikuwa ni "mtu wa kawaida kawaida tu".

Swali- Mwendesha Mashtaka: Ni makampuni mangapi yaliyolalamika kwako kuhusu mchakato wa tenda hii ya vitambulisho?

Waziri Madusha (Jibu): Haikuwa kampuni moja bali tano.

Swali: Kwenye barua yako kwa Waziri Mkuu ulisema kampuni ngapi zimelalamika kwako?

Jibu: Sikumbuki mara moja nilisema ni ngapi hasa ila nilitolea mfano wa kampuni moja.

Swali: Ngoja nikusomee barua yako hiyo ukurasa wa nne, Naomba ipokolewe kama kizibiti namba moja. Unasema hivi "baada ya kupitia taarifa ya Kamati ya tathmini (evaluation committee) na hasa kutokana na malalamiko niliyoyapokea toka Kampuni ya SANGAM SECURITAS niliona ipo haja ya kupata ufafanuzi" na pia unarudia kwenye ukurasa huo huo na kusema kuwa "Katika kikao hicho niliwafahamisha kuwa nimepokea malalamiko kutoka kwa mojawapo ya waombaji". Je, msomaji wa barua hiyo aelewe ulikuwa umepokea malalamiko kutoka makampuni mangapi?

Jibu: Anaweza kuelewa vyovyote lakini haiondoi ukweli kuwa nilipokea malalamiko zaidi ya kampuni moja.

Swali:
Bw. Masha, wewe umesema kuwa umepokea malalamiko toka "kampuni ya" na pia umepokea malalamiko toka "mojawapo" ya waombaji, sasa mtu kwanini aelewe "vyovyote"? Ni lini neno "mojawapo" linamaa ya wingi?

Jibu:
Mimi msukuma kwetu mojawapo inaweza kumaanisha mambo mengi (ukumbi unaguna kwa kicheko).

Swali: Je umewahi kukutana na maafisa wa kampuni ya SANGAM SECURITAS wakati wowote wa mchakato huu?

Jibu: Una maana gani "kukutana"?

Swali: Kwamba umewahi kuwasiliana nao aidha ana kwa ana, kwa njia ya barua, simu, barua pepe au kwa namna yoyote kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja nao?

Jibu: Huku kukutana unakozungumzia una maana rasmi au siyo rasmi?

Swali: Haijalishi kama rasmi au siyo rasmi! Umewahi kukutana nao wakati wowote kampuni hii?

Jibu: Nilipokuwa Uswisi Mkurugenzi wa Kampuni hiyo alinialika kwa dakika chache kuangalia shughuli zao pale lakini sijui kama huko nikukutana!

Swali: Mhe. Jaji naomba mahakama irekodi kuwa mshtakiwa amekubali kukutana na maafisa wa SANGAM SECURITAS huko Hispania?

Jibu: Hapana Jaji, sijakubali! Mimi nimesema tu kuwa nilialikwa nichepukie pale mara moja wakati natoka Oman na sidhani kama ile unaweza kuiita kukutana.

Jaji: Wakili endelea na maswali, karani, hakikisha umerekodi kuwa Bw. Masha alikutana na watu wa SANGAM.

Swali:Umesema kwenye barua yako na umerudia mara kadhaa katika vyombo vya habari kuwa ulipokea malalamiko kutoka kampuni ya SANGAM SECURITAS na sasa umeongeza kuwa makampuni mengine pia yamelalamika kwako. Ni barua gani ulipokea kuhusu malalamiko hayo?

Jibu:
Sikusema nimepokea barua yoyote.

Swali: Sasa ulipokea malalamiko hayo kwa namna gani?

Jibu: SANGAM SECURITAS walilalamika kwangu, na mimi baada ya kuona kuwa malalamiko yao yana msingi niliwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara yangu kutaka ufafanuzi kama nilivyosema kwenye barua yangu.

Swali: Naomba nirudie tena, ulipokea malalamiko kwa njia au namna gani?

Jibu: Kwani malalamiko yanatolewa kwa namna gani?

Swali: Mhe. Jaji, naomba mshtakiwa yuko argumentative naomba umlazimishe ajibu swali.

Wakili wa Utetezi: Mhe. Jaji, tayari Mshtakiwa ametoa jibu lake kuwa amepokea malalamiko sasa Wakili anachotaka kujua sijui ni kitu gani naona anataka kuipotezea mahakama hii muda tu!

Jaji: Jongeeni hapa. (mawakili wanasogea kwenye meza ya Jaji, Mic zinazimwa na anawanong'oneza jambo huku kidole chake kikionekana kinainuliwa inuliwa juu kutilia mkazo)

Jaji: Bw. Madusha iambie mahakama hii ulipokea malalamiko ya makampuni hayo kwa njia gani, kumbuka uko chini ya kiapo.

Jibu:
Nilizungumza nao ana kwa ana.

Swali: Kwa hiyo katika wizara nzima ni wewe peke yako mwenye rekodi ya kukutana na wawakilishi wa makampuni hayo katika mazingira unayoyajua wewe ambayo unasema kuwa yalitosha kwa wewe kuandika barua?

Wakili wa Utetezi:
Objection your honor!

Swali: Withdrawn naomba nilipange upya swali langu. Bw. Madusha, umepokea malalamiko kutoka kwa kampuni moja au nne, katika mazingira ambayo siyo rasmi, kwanini watu wasiamini kuwa kulikuwa na kukiuka taratibu?

Jibu: Mimi nilifanya hayo yote kulinda maslahi ya Taifa na ni kutokana na mimi kuwasilisha malalamiko hayo mchakato ukaangaliwa upya na ndiyo maana mchakato ukaangaliwa upya, kwa hiyo mimi natakiwa kutazamwa kama shujaa na mtetezi siyo mhalifu kama unavyoashiria.

Swali: Hivyo katika kuonesha uzalendo wako uko tayari hata kuvunja sheria ili uonekane kuwa shujaa?

Wakili wa Utetezi: Objection your honor, Wakili anamhukumu mshtakiwa!

Jaji: Wakili angalia mwelekeo wa maswali yako.

Swali:Kwanini ulikubali kupokea malalamiko ya makampuni haya nje ya taratibu (informal) wakati wewe hauko kwenye mchakato wa Tenda na hakuna mahali popote ambapo ulimuita Katibu wako awe sehemu ya kusikiliza malalamiko hayo?

Jibu: (kimya)

Swali: Narudia tena, Kwanini ulikubali kupokea malalamiko ya makampuni haya nje ya taratibu (informal) wakati wewe hauko kwenye mchakato wa Tenda na hakuna mahali popote ambapo ulimuita Katibu wako awe sehemu ya kusikiliza malalamiko hayo?

Jibu: Kutokana na ushauri wa wakili wangu sitopenda kujibu swali hili nikikwepa kujichongea mwenyewe.

Swali: Kama wewe hauko katika mchakato kusimamia tenda au hata kukata rufaa, imekuwaje usikilize malalamiko ya makampuni manne badala ya kukataa kabisa kuyachukua malalamiko hayo na kuwaelekeza kwa Katibu wako Mkuu?

Jibu: Kutokana na ushauri wa wakili wangu sitopenda kujibu swali hili nikikwepa kujichongea mwenyewe.

Swali: Bw. Madusha unafikiri lolote ulilofanya kwenye hili linakaribiana na heshima ya uzalendo, utawala bora, na kuheshimu sheria?

Jibu: Mimi ni Mwanasheria, nimesoma na kukulia Marekani. Nimerudi nchini kuijenga nchi yangu. Katika kufanya hivyo nimeshiriki katika mambo mbalimbali, nimeanzisha kampuni na kutoa ajira kwa watanzania wengi, nimechaguliwa na watu wa Isamilo na kuwa Mbunge, Rais ameamini katika uwezo wangu na amenidhamini wadhifa huu wa Uwaziri.

Hivyo katika yote ambayo nimefanya hadi hivi sasa naona fahari kujiona mzalendo kitu ambacho wakosoaji wangu hawaamini. Watu wananionea wivu kwa sababu mimi ni kijana tena msomi, na wapo wanaoona natishisha maslahi yao. Kwa hiyo ndiyo mimi ni mzalendo wa kweli!

Swali: (wakili ameongeza sauti na anazungumza kwa haraka huku akimkazia macho Waziri Madusha) Kwa hiyo ni huo uzalendo ndiyo umekufanya uwe tayari hata kuvunja sheria kutetea kile unachoamini ni maslahi ya nchi hata kuingilia mchakato wa tenda za wizara?

Jibu: Mimi ni mzalendo (huku naye anaongeza sauti na uso wake uko serious na anagonga kingo ya kizimba kwa jazba). Yote niliyoyafanya hadi sasa ni kwa ajili ya nchi yangu!

Swali: Hivyo kwa ajili ya nchi yako uko tayari kuvunja sheria Mhe. Madusha? Jibu swali!

Jibu: Ndiyo!!! Niko tayari kufanya lolote kama maslahi ya nchi yangu yanatishiwa, niko tayari kukutana na mtu yeyote mahali popote na wakati wowote, niko tayari hata kuvunja sheria ya tenda na manunuzi ya serikali kama nikiona sheria hiyo ni kikwazo kwangu! Ndiyo.. now you have it!

Wakili: Sina maswali ya ziada Mhe. Jaji!

Waziri Madusha anatoka kizimbani huku akitengeneza tai, na akiiweka sawa miwani yake ya jua. Kipara chake ambacho kinaonekana kinang'ara kama kimetiwa samri kiliakisi taa za ukumbi huo. Anajipangusa mdomo huku baadhi ya watu wakinong'ona. Wanasubiri kesi hiyo itapoendelea tena kesho!!

Disclaimer:
Kisa hiki ni cha kutunga, mfanano wowote wa majina ya watu, mahali, na matukio halisi ni mambo ya kinasibu na matokeo ya ubunifu wa mtunzi.

...a few good men!

standing ovation
 
Back
Top Bottom