Waziri aomba uume wa Mwalimu usifanye kazi

Taabu siku hizi watoto wetu wanafunzi nao wanapenda sana ng'ono! wasipofanya na waalimu hufanya wao kwa wao. Utakuta about 40% za hizi mimba wanafunzi wamepeana wenyewe kwa wenyewe!

Elimu pia ya hatari ya ng'ono kwa hawa watoto ni muhimu!
 
Kule Kilosa mwaka juzi mwalimu mmoja wa kike alipewa mimba na mwanafunzi wake wa darasa la sita. Hata wazazi walilalamika, lakini mwalimu alidai anampenda mwanafunzi huyo. Sikupata nafasi ya kufuatilia kesi ile hadi mwisho. Hivi huyu mheshimiwa waziri angepewa pia taarifa za mwalimu huyo wa kike angemwombea dua la vipi?
 
Kauli za mawaziri wetu wakati mwingine unajiuliza hivi...hawa ni viongozi kweli? Na hili wanafunzi wote wanatakiwa walisikie. Na ikiwa hili ni pendekezo la waziri ni sawa na kusema ili wanafunzi waepeshwe na upewaji wa mimba na walimu basi walimu wasi....(nashindwa kuyarudia matamshi ya waziri). Namna katoa ufumbuzi kama vile yupo na shoga zake anakazia mchapo! Waziri huyo!
 
Ile semina elekezi naona haikufanya kazi.........tatizo ni kuweka vihiyo kwenye nafasi muhimu katika uendeshaji wa nchi. Hivi unatagemea mtu kama huyu akipanda na kuwa waziri...atazungumza nini ndani ya baraza la mawaziri? si atabaki kunywa maji tu na kupiga makofi..!


Kwani mkuu waliokuwa kwenye uwaziri mpk sasa si ndio hao ambao wameipelekea nchi hasara kubwa pamoja na ujuzi wao na elimu yao kubwa waliyonayo.
 
Mwalimu kama kioo cha jamii na hata wazazi wote wanaokula uroda na wanafunzi wanatakiwa wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu za utumishi wa umma,na pia sheria za nchi. Mwalimu anatakiwa kumlea mwanafunzi, kiakili kimwili na kiroho. Kiakili anatakiwa amfundishe kukuza uwezo wake wa kufikiri wa namna ya kupambanua mambo mbalimbali katika maisha yake ya kila siku. Kimwili anatakiwa ajue usafi wa mwili wake, mabadiliko yanatokea katika mwili naaweze kuupa mazoezi mwili wake ili kuuweka katika afya nzuri. kiroho, mwanafunzi antakiwa afundishwe maadili yaliyomema na kuweza kutamua uwepo wa Mungu.

Hata kwa aoni yangu Mh. Naibu waziri ametoa laana kwa jazba mno, kwani kwa kufanya anaweza kutoa hat laana ya kuua mtu. Kwa sababu anaposema kuwa aombewe dua hata uume wake usimame milele si bsara sana kufanya hivyo kwa kiongozi anayesimamia taasissi kubwa namna hiyo katika nchi. Kauli hii haina tofauti na ile kauli iliyomliza Mh.Pinda Bungeni ya kusema wanoua alubino wauawe;

Kifupi viongozi wetu wawe makini katika kutoa kauli zao wanapokuwa katika majukwaa, watambue kuna sheria kanuni na taratibu katika nchi ambazo ndizo zinztoa mwongozo wa kushughulikia kila jambo lisilo zuri kwa nchi.
 
Sumbawanga

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza amewataka wananchi wa kijiji cha Muze wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kumuombea dua mbaya aliyekuwa mwalimu wa shule ya sekondari Mazoka aliyempa mimba mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo.

" Na hili la huyu bazazi, aliyemkatisha masomo mwanafunzi ni lazima tumuombee dua ili asisimame daima,uume wake uache kufanya kazi" alisema.

Hivi huyu mama ana dini kweli? Haya mambo ya KUOMBEANA mbona yamekaa kama kimilamila zaidi? Au kuna dini zina tabia ya kuombea LAANA impate mtu fulani? Kanisani utotoni tuliimba "Mungu Ni pendo, apenda watu..." Sasa hii laana Mungu ataitoa wapi? Huyu mama anaweza kuwa Mkatoliki fulani hivi.

Kwa nini huyo binti AKATIZE masomo? Si wamwache akazae na akizaa tu amwache mtoto kwa babu zake na yeye arudi shuleni. Walau atakuwa mfamo hai kwa wenzake kuwa "Utamu wa pilipili ni muwacho wake", neno ambalo ni sahihi ya member mmoja wa JF.
 
Back
Top Bottom