Waziri amtetea mkurugenzi kukataa kumkirimu Dk Shein

Andindile

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
304
16
SAKATA la Halmashauri ya Karatu, kugomea kulipia malazi ya Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein na ujumbe wake limechukuwa sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani kuunga mkono uamuzi wa halmashauri ni sahihi.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Kombani alisema halmashauri za wilaya haziwajibiki kuchangia ziara za mawaziri, rais au makamu wake, wanapotembelea katika maeneo yao.

Kombani alibainisha kuwa kama ingekuwa utaratibu huo upo, halmashauri nyingi zingefilisika hasa ambazo mawaziri wanatoka, kwa sababu wana utaratibu maalumu wa kutembelea zaidi ya mara tano kwenye maeneo yao, kwa mwaka.


"Kwa mfano kwa mwaka mimi hufanya ziara mara sita katika wilaya yangu ya Ulanga (Morogoro). Tukisema wanigharamie basi ingefilisika pamoja na halmashauri nyingine ambazo zina mawaziri," alisema Kombani ambaye ni Mbunge wa Ulanga Mashariki.

Akielezea kuhusu taratibu za matumizi ya fedha kwenye halmashauri, alisema kwa kawaida matumizi yote hupitishwa kwenye vikao vya madiwani.

Alibainisha kuwa gharama za msafara wa rais, makamu wa rais na mawaziri hugharamiwa na serikali kuu, kulingana na taratibu zilizowekwa.

"Ndiyo maana rais anapokuwa kwenye ziara huenda na vyakula vyake," alisema Kombani lakini akafahamisha kuwa halmashauri zinaweza kutenga fungu kwa ajili ya kuuandalia ugeni kwenye maeneo yao chakula cha jioni.

Iwapo halmashauri itaamua kufanya hivyo, alisema kuwa ni lazima fungu hilo liwe limepitishwa na halmashauri kupitia vikao vyake halali na si mkurugenzi na watendaji wake.

Alipoulizwa juu ya adhabu ya kiongozi wa halmashauri atakayetoa fedha pasipokufuata taratibu; alisema kila halmashauri ina taratibu zake za kuwajadili viongozi au maofisa waliokiuka taratibu na kuwachukulia hatua.

Suala la Halmashauri ya Karatu, kugomea kulipia malazi ya Makamu wa Rais pamoja na ujumbe wake liliripotiwa na gazeti la Mwananchi Jumatano iliyopita likionyesha kuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Mathew Sedoyeka alimjia juu na kumtaka aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Majid Myao, aandike barua ya kujieleza kwanini alikataa kutoa fedha za kulipia ziara ya makamu wa rais wilayani humo.

Sedoyeka hakufurahishwa na kitendo cha halmashauri hiyo kugoma kulipa kiasi cha Sh2 milioni ambazo ni malipo ya kulala siku moja pamoja na chakula kwa ujumbe huo wa makamu wa rais, katika hoteli ya Bougain Villea ya mjini Karatu.

Kwenye barua ya kujieleza iliyoandikwa Machi 3, 2009 yenye kumbukumbu namba kdc/ded/cv.3/1/121, Myao amejitetea kuwa uamuzi wa kutolipiwa ziara hiyo, umetokana na kamati ya fedha ya madiwani kukataa kuidhinisha fedha hizo.

Alisema kutokana na kutoidhinishwa malipo hayo, aliona angekiuka Sheria namba tisa ya mwaka 1982 ambayo inahusu masuala ya matumizi ya fedha za halmashauri na maamuzi ya kamati ya fedha.

“Kama mimi ningetoa malipo hayo ni wazi ningekiuka sheria za serikali za mitaa hasa ikizingatiwa madiwani katika kikao chao halali ndio waligomea,” alieleza Myao.

Akizungumzia sakata hilo, Mbunge wa Jimbo la Karatu, Dk Willibrod Slaa alisema alichofanya ofisa huyo wa serikali ilikuwa halali kwa sababu walikuwa hawana bajeti ya malipo hayo.
Dk Slaa alitoa wito kwa serikali kutomuadhibu mtendaji yoyote wa halmashauri hiyo kutokana na uamuzi uliochukuliwa, ambao ulizingatia maadili ya kazi na utekelezaji wa utawala bora.

Source: Mwananchi ::4/18/2009

Karatu wamewasha moto wengine wafuate.
 
Wameanza kuzisoma alama za nyakati sasa. I hope kutakuwa na halmashauri nyingi nchini zitakazokataa kubebeshwa gharama za 'milo na malazi ya wakubwa' zisizowahusu.
 
Selina Komba sijakufuatilia sana na sijui track record yako sana lakini unatia moyo sana.

Kwamba kuna waziri anayeweza kuja kutoa ufafanuzi wa hakika tu kuhusu mambo yanavyoendeshwa ni kiti kizuri sana, hasa ukizingatia ulimwengu huu wa "no comment"

Swali linakuja, kama Ofisi ya Makamu wa Rais ilishagharamia, hizi hela za Halmashauri zilikuwa zinaenda wapi?

Kama ofisi ya makamu wa rais haikugharamia na hela za halmashauri zinatakiwa kugharamia, hela zilizotengwa na ofisi ya Makamu wa rais zinakwenda wapi?

Hapa kunanuka ufisadi!
 
Selina Komba sijakufuatilia sana na sijui track record yako sana lakini unatia moyo sana.

Kwamba kuna waziri anayeweza kuja kutoa ufafanuzi wa hakika tu kuhusu mambo yanavyoendeshwa ni kiti kizuri sana, hasa ukizingatia ulimwengu huu wa "no comment"

Swali linakuja, kama Ofisi ya Makamu wa Rais ilishagharamia, hizi hela za Halmashauri zilikuwa zinaenda wapi?

Kama ofisi ya makamu wa rais haikugharamia na hela za halmashauri zinatakiwa kugharamia, hela zilizotengwa na ofisi ya Makamu wa rais zinakwenda wapi?

Hapa kunanuka ufisadi!

Mkuu sidhani kama Kombani katoa ufafanuzi kwa sababu ana uchungu na pesa za walala hoi huko kwenye halmashauri. Ngoma imekuwa nzito ikabidi ajinasue tu kwa kutoa hizo porojo. Labda angesama kuwa hilo suala halipo na kama kuna mtendaji yeyote wa halmashauri nchini amewahi kufanya hivyo achukuliwe hatua mara moja. Hapo ningemwona kama yuko kazini. Haya mambo yanafanyika sana na hasa hasa zile halmashauri zilizo chini ya CCM. Hii kazi nzuri ya Karatu imefanywa na CHADEMA na huyo waziri inabidi ajikoshe tu. Vinginevyo yeye bado ni msanii kama wasanii wenzake wa serikali ya awamu hii na hawezi kuwa na jipya.
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni, Waziri Kombani kalonga jambo la maana. Ni kupitia kauli hii, ndio inazifungua macho zile halmashauri nyingine zote kuwa kumbe pesa yao ni takrima kwa wengine.
 
Utaratibu wa matumizi ya fedha za Halmashauri za miji unajulikana na upo wazi kama alivyoelezea Waziri Selina, Aidha kuwepo na matumizi kinyume na taratibu mara nyingi kunasababishwa na Madiwani wenyewe.

Kuna baadhi ya Madiwani ambao ugeuza Ofisi za Halmashauri zao, kuwa kama ofisi zao na kuweza ukijikuta ukidhania ni watendaji wa Halmashauri. Tabia hii uwafanya wawe wanatoa maelekezo kwa watendaji kinyume na utaratibu, kwa kuwapa ahadi ya kuwatetea siku kamati husika ikikutana.

Wenyeviti wa kamati mara nyingi wamekuwa na tabia hii, na iwapo Madiwani wa kamati sio wakakamavu, basi huwaburuza vizuri pamoja na watendaji wake kwa manufaa yake binafsi ama ya chama chake.
 
Back
Top Bottom