Waziri akishaisoma hotuba bungeni, bunge haliwezi kubadilisha kitu-Spika makinda

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,193
1,434
kwenye taarifa ya habari ya saa 2 jana usiku, Spika (bi Kiroboto) wa bunge la JMT clearly alisikika akisema kwamba once waziri (mathalani) wa fedha akiisoma hotuba yake ya bajeti ambayo imeshapitishwa na vikao vya chini basi wabunge kwenye bunge hawawezi kubadilisha kitu. kama huyu ndio refarii na kamisaa wa mechi ana-declare kwamba mechi anayoichezesha tayari ina matokeo fixed yaliyopatikana kwenye pre-match meeting, je anafaa kwa faida ya taifa hili? kama hii ndio mind-set yake kwamba bunge letu ni rubber-stamp, je anatufaa?
 
Hahahahahaha et bi kiroboto. Mkuu hapo umenisababishia maumivu ya mbavu. By the way huyo bi kiroboto kapewa nafas pale mjengon ili alinde chama so usishangae anavyobehave..
 
Huyu mama alishawahi kupewa ushauri wa bure na former Spika Msekwa kwamba
ni vizuri spika akawa na taaluma ya sheria yeye akasema sio lazima. Hivyo anaanza
sasa kuwatisha wabunge hata kabla bajeti haijasomwa. Hivi huwa hasomi hansard za bunge.

Nakumbuka mwaka jana wakati wa bajeti la bunge serikali ilifuta misamaha yote
ya kodi kwa taasisi za kidini. Lakini baada ya viongozi wa dini kupiga kelele (hasa wakiristo)
ilibidi serikali isalimu amri na kurudisha misamaha ya kodi ya taasisi za kidini.
Waziri wa fedha ilibidi aifumue bajeti yake na kure-budget upya, kuziba pengo
la misahama ya kodi.

Sasa kama hili liliwezekana anasemaje kwamba bugdet ikishasomwa na waziri
haiwezi kuabadilisha?. Anne makinda ni kihiyo mwingine na tunda la mafisadi no
wonder sasa hivi amefunga barabara ya wananchi wa Kijitonyama na Sinza!
 
Bi kiroboto wewe, hivi unazitaka roho zetu wa Tanzania. Tumetuma wawakilishi wetu badala yake mmewageuza ma rubber stamp wa kupitisha ma deal yenu. Kuna siku patachimba hapa, halafu tutawafukua kwenye mahandaki kama Gbagbo au Saddam. Ninyi tuchezeeni tu mkidhani mna guarantee ya kuitawala hii nchi. Jiulize mapinduzi yalianzaje kwa nchi zingine, yanakuja na hapa kwetu, tena hayapo mbali
 
Kwa maana hiyo kwa nini kuwepo na vikao vya bunge? Bunge linafanya kazi kwa maelekezo ya serikali? na nini maana ya separation of powers?

Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba wakubwa wamedhamiria kufanya maamuzi kuwa maoni yote juu anything yatolewe wakati wa kamati za bunge. Kwa maana hiyo akishasoma mwenyekiti wa kamati ya bunge basi hakuna mtu anaruhusiwa kusema kitu tofauti especially kama ulikuwa ni mjumbe kwenye hiyo kamati. Lakini kama tujuavyo wenyeviti wengi wanatoka ccm na kazi yao kubwa wanapopewa miswaada na taarifa nyingine za serikali huwa wanaishia kuangilia comma na full-stop!
Chadema mjiandae maana kuna mkakati mkubwa sana wa kuzuia hoja zenu ili serikali isiumbuliwe kama Lissu alivyowaumbua Mwanasheria mkuu na Celina Kombani.

Mwanzoni huyu mama alifanya kila awezalo kuwafungisha ndoa ya lazima chadema na cuf etc. Nadhani huu ulikuwa ni mkakati maalum wa kuzima moto wa chadema. Sasa wamesikia mawaziri vivuli wakitoa videkezo vya nini watasimamia kwenye bunge la bajeti huyu mama anatangaza kuwa akishaongea waziri basi.
 
Mimi siumizwi na kauli yake, mhanga mkubwa wa hilo ni ccm yenyewe kwakuwa wananchi wa sasa wanaufahamu wa hali ya juu tofauti na miaka ya nyuma. Ukweli hawa jamaa hawafanyi utafiti wa nini kinachowakera wananchi mpaka wanazomewa na kukataliwa ila kwa kifupi ni mambo kama hayo.

Bibi Kiroboto unaharakisha mageuzi kwa kauli yako hiyo, napenda kukumbusha tu fanya kweli, zuia hoja za nguvu, fukuza wapambanaji bungeni nk kwa kufanya hivyo kazi inazidi kuwa rahisi.
 
Tehe tehe tehe eti bi kiroboto ahahaaaahaaa lakini kama wanafanana vile!!!!???
 
Bibi Kiroboto = Dr. A Makinda?

09_10_csyf2q.jpg
Anne-Makinda.jpg
 
Back
Top Bottom