MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Na Ramadhan Mbwaduke
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya, amesema Bungeni kuwa, hakustushwa na bomu la tuhuma za ufisadi katika mradi wa maji mkoani Shinyanga lililolipuliwa na Dk.Wilbroad Slaa, kutokana na ukweli kwamba anamfahamu mbunge huyo hizo ndiyo zake na kila wanapomuona na kabrasha, wanajua amebeba taarifa nyeti.
Profesa Mwandosya alisema hayo jana jioni wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2009/2010.
Pamoja na ufafanuzi wa hoja za wabunge wengine kadhaa, pia alikuwa na kazi ya ziada ya kujibu kombora la tuhuma za ufisadi lililolipuliwa na Mbunge huyo wa Karatu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Prof. Mwandosya alisema licha ya ukweli kuwa Wizara imebaini taratibu hazikufuatwa katika kumsimamisha Mkurugenzi wa Fedha wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Shinyanga, (SHUWASA), Bw. Charles Mwibula, ambaye Slaa alisema amesimamishwa kinyume cha utaratibu kwa sababu tu alikataa kushiriki 'dili' hilo, lakini kamwe wao hawakushtushwa na hoja zilizoibuliwa na Dk. Slaa kwa vile wanamjua kuwa kila anapokuwa na kabrasha, huwa ndani yake amebeba siri za Serikali.
"Kama Slaa atakuwa na nyaraka zaidi ya hizi anazosema, nitafurahi akinionyesha... kwa sababu lengo letu ni moja ambalo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji," akasema Prof. Mwandosya.
Kuhusiana na kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa Fedha, Prof. Mwandosya akasema: "Tunakiri kuwa taratibu hazikufuatwa... tumeelekeza aitwe tena, taratibu zifuatwe," akasema.
Sakata lenyewe lililoibuliwa na Dk. Slaa jana wakati akichangia bajeti ya Wizara hiyo, ni juu ya tuhuma za ufisadi, ambapo anadai zilitokana na kukiukwa kwa sheria za manunuzi ya umma katika mradi wa Maji Shinyanga uliotajwa kuwa na thamani ya Shilingi Bilioni 2.1.
Alidai kuwa vigogo katika Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Shinyanga (SHUWASA) ndio waliokiuka sheria kuhusiana na mradi huo wa usambazaji maji na kusababaisha Mkurugenzi wa Fedha wa SHUWASA, Charles Mwibula, asimamishwe kazi na wakubwa wake hao baada ya kukataa kushiriki mradi huo.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, SHUWASA waliomba Sh. bilioni 2.1 kinyume cha utaratibu, ambapo licha ya kasoro kadhaa zilizopo, bado kuna maofisa wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji walipeleka Sh. Milioni 700.
Akadai kuwa jambo hilo linaonyesha wazi kuwa maofisa wengine wizarani wanashirikiana na wale wa SHUWASA kufanyia ufisadi fedha za mradi huo.
Alidai kuwa kinacholalamikiwa hapo ni kuwa taratibu za tenda zilikiukwa na kiwango cha fedha kilikiukwa kwani kilipaswa kupata kibali kutoka kwenye bodi ambayo kwa bahati mbaya, haikuhusishwa na pia kuna nyaraka za kugushi zilitumika.Hata hivyo, katika ufafanuzi wake kuhusiana na sakata hilo, Profesa Mwandosya alisema kwa mujibu wa taarifa alizo nazo, hakuna ubaya wowote uliofanyika kuhusiana na mchakato wa mradi huo.Katika hatua nyingine, Prof. Mwandosya alieleza kuwa awali, makampuni mawili yalipewa tenda ya kusambaza maji, moja ikiwa kwa wateja wa Kahama na kampuni nyingine kwa wateja wa Shinyanga.Hata hivyo, Profesa Mwandosya akasema kuwa kampuni iliyopewa tenda ya Shinyanga ilionekana kushindwa kazi, kwani hadi kufikia Februari mwaka huu, ilikuwa imeweza kuunganishia maji wateja 200 pekee na kuibua shaka ya wazi kuwa hawataweza kufikia lengo la kuwasambazia maji wateja 5,000 kufikia mwezi Machi mwaka huu.
Source: ALASIRI