Wazi Mkuu: Kwamba watz ni watu waexcuse

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,722
515
I am sorry to say this...Kwa kweli ndani ya moyo naamini kuwa the last time we hand as serious premier ilikuwa ni Hayati Sokoine..

Hivi Pinda kama waziri mkuu wa nchi anawezaje ku-sanction kauli kwamba watanzania hawapati fursa za ajira kwa sababu ya kuwa na excuses. After all kila nchi ina social cultural yake.

Hivi WM anapaswa kusimamia policy na sheria za nchi au feelinga za wawekezaji? SHAME
 
Watanzania wanatoa excuse.....mara mtoto anaharisha.....nimefiwa n.k.......dah
 
Niliamini huyu jamaaa anaweza kuja kuwa moja ya viongozi mashuhuri kumbe bogas kabisa
 
Watanzania wanatoa excuse.....mara mtoto anaharisha.....nimefiwa n.k.......dah
Preta kimsingi nakubali kuna swala la excuses. Issue hapa ni kwamba tuna policies zinazopashwa kulinda na kutengeneza ajira kwa watz kwa kada fulani.Kauli ya kiongozi wa juu inaua nguvu ya watu wa idara za chini ku-enforce sheria husika. Ni kwamba PM anazifanya hizo polisi kuwa irrelevant.
 
I am sorry to say this...Kwa kweli ndani ya moyo naamini kuwa the last time we hand as serious premier ilikuwa ni Hayati Sokoine..

Hivi Pinda kama waziri mkuu wa nchi anawezaje ku-sanction kauli kwamba watanzania hawapati fursa za ajira kwa sababu ya kuwa na excuses. After all kila nchi ina social cultural yake.

Hivi WM anapaswa kusimamia policy na sheria za nchi au feelinga za wawekezaji? SHAME

Hii habari ya watanzania kuwa na excuse nyingi ni slogan maarufu sana kwa wawekezaji ili wajipatie nafasi ya kuajiri watu kutoka nchini mwao.

Na katika hili wakenya na wahindi wanaongoza kwa kuitumia hii slogan ili kuwanyima ajira wazawa na kuwaleta nchini watu kutoka nchini mwao.

Bahati mbaya sana viongozi wetu wengine kwa kujua kabisa na wengine kwa kutokujua wamekuwa wakiingizwa mkenge na hawa wanaojiita wawekezaji kwamba watanzania wana excuse nyingi ilihali sio kweli kabisa.

Mimi huwa najiuliza, hivi mtanzania akiajiriwa kwenye sekta binafsi ndipo anakuwa na excuse lakini akiajiriwa shirika la umma ama serikalini excuse zinakwisha?? manake ilitakiwa viongozi wetu hawa waanzie maofisini kwanza kuangalia uhalisia wa hizi allegations za hawa wawekezaji uchwara.

Kuna rafiki yangu mmoja anafanya kazi na mhindi mmoja aliyeajiriwa kama expert lakini akienda likizo hali inakuwa mbaya sana ofisini hata likizo hawezi kuifurahia muda wote "expert" anampandia hewani kupata ushauri na bahati mbaya sana kutokana na hali hiyo huyo mhindi ambaye ni expert na ndiye bosi wake hawezi kumruhusu kwenda likizo zaidi ya wiki mbili!!

ukweli ni kwamba watanzania tunachapa kazi, tatizo viongozi wetu ndio wanatuangusha.
 
Watanzania wanatoa excuse.....mara mtoto anaharisha.....nimefiwa n.k.......dah

wao watoto wao wakiharisha wanakimbizwa aga khan ama tmj na hospitali nyingine nyingi nzuri za kiwango cha juu tena kwa kutumia gharama za kampuni wakati wazawa wakiuguliwa ni juu yao, katika hali kama hiyo lazima watakuwa na mtazamo huo.

Labda nikusaidie kitu kimoja kwamba, hawa wageni wakiajiriwa wanapatiwa matibabu hospitali za kueleweka wao na wenzi wao na watoto wao, tena ikionekana tu hapati nafuu haraka mara moja kapandishwa ndege kakimbizwa nairobi, bondeni ama ulaya, sas jiulize hawa wamatumbi wakiugua ama kuuguliwa wanatibiwa wapi?? kuna mfanya kazi mwenzetu alitakiwa kwenda india kutibiwa lakini mwajiri a.k.a mwekezaji hakutoa chochote ilibidi wafanyakazi na ndugu zake tuchangishane ili kupata fedha za kumpeleka india lakini alipopona akarudi kuchapa kazi kwa mwekezaji!!
 
Watanzania wanatoa excuse.....mara mtoto anaharisha.....nimefiwa n.k.......dah

Preta, hivi Watanzania hao wakilipwa vizuri kama watu wa nje unadhani excuses zitakuwepo? Kwa mtazamo wangu wafanyakazi wengi wako demolorised ndo maana hawafanyi kazi seriously.

Mfano wa karibu kabisa chukulia mfano Ufanisi wa Kazi ulivyo ofisi ya PM ni tofauti kabisa na ufanisi wa mwalimu anayefundisha shule ya Sekondari Ulyampiti. Ufanisi wa mfanyakazi wa ikulu hauwezi kuwa sawa na tabibu wa zahanati ya mpitimbi. Ofisi hizo kubwa zina mishahara mizuri na marupurupu kibao mfanyakazi gani wa ofisi hizo atatoa excuse.

Tuwe realistic angalau for once
 
Hii hotuba ya mkuu niliisikia alhamis kwenye maswali ya papo kwa hapo kwa WM bungeni......nilichoka sana....sasa kama uongozi wa juu kiasi hiki ndio unatamka maneno kama haya......Watanzania tumlilie nani?.....
 
Mwita nimekupata...kwa kweli Pinda na wanzake waufahamishe umma wa Tanzania kwanini serikalini hawaajiri watu toka nje wasio na excuse ili tupate umeme wa uhakika?

Hawahitaji kuajiri watu toka nje, wafanyakazi are well taken care of by the governement,

Serikalini kuna bajeti ya chai ya mabilioni, wakiishiwa wanaenda shimiwi kufukuza kuku, kucheza karata na kuvutana kamba, ikifika pasaka ofisi za bara na visiwani zinatembeleana kimichezo, mwezi wa sita mko mnazi mmoja maonyesho ya utumishi wa uma (2 weeks), sabasaba maonyesho another two weeks nanenane maonyesho another two weeks utatoa excuse ya nini, labda uwe mwehu!!!!!
 
Hawahitaji kuajiri watu toka nje, wafanyakazi are well taken care of by the governement,Serikalini kuna bajeti ya chai ya mabilioni, wakiishiwa wanaenda shimiwi kufukuza kuku, kucheza karata na kuvutana kamba, ikifika pasaka ofisi za bara na visiwani zinatembeleana kimichezo, mwezi wa sita mko mnazi mmoja maonyesho ya utumishi wa uma (2 weeks), sabasaba maonyesho another two weeks nanenane maonyesho another two weeks utatoa excuse ya nini, labda uwe mwehu!!!!!
You are right! Na zote hizo ni posho.
 
Hii hotuba ya mkuu niliisikia alhamis kwenye maswali ya papo kwa hapo kwa WM bungeni......nilichoka sana....sasa kama uongozi wa juu kiasi hiki ndio unatamka maneno kama haya......Watanzania tumlilie nani?.....

Nami nilisikia, nilishituka sana.

Kama hiyo ni statement ya serikali , kwa mantiki hiyo waziri anayetoa work permit anaweza kuchukulia hiyo kama sababu ya kukubali work permits zote za wageni.

Nangojea na kuomba siku moja Cameroon aseme waingereza ni walevi ndio maana kazi tunawapa wapakistan na wahindi.
 
Hata kama amechoka kiasi gani kuwaongoza waingereza hawezi kuthubutu kuzungumza utumbo kama huo.
 
Hii hotuba ya mkuu niliisikia alhamis kwenye maswali ya papo kwa hapo kwa WM bungeni......nilichoka sana....sasa kama uongozi wa juu kiasi hiki ndio unatamka maneno kama haya......Watanzania tumlilie nani?.....

Wala hatuhitaji kumlilia mtu yeyote, utaambiwa umekalia kulia lia tu badala ya kuchapa kazi!
 
Preta, hivi Watanzania hao wakilipwa vizuri kama watu wa nje unadhani excuses zitakuwepo? Kwa mtazamo wangu wafanyakazi wengi wako demolorised ndo maana hawafanyi kazi seriously.

Mfano wa karibu kabisa chukulia mfano Ufanisi wa Kazi ulivyo ofisi ya PM ni tofauti kabisa na ufanisi wa mwalimu anayefundisha shule ya Sekondari Ulyampiti. Ufanisi wa mfanyakazi wa ikulu hauwezi kuwa sawa na tabibu wa zahanati ya mpitimbi. Ofisi hizo kubwa zina mishahara mizuri na marupurupu kibao mfanyakazi gani wa ofisi hizo atatoa excuse.

Tuwe realistic angalau for once

Na ndio maana unaona seriklali imeamua kuondoa kodi kwenye posho wanazopata watumishi wa ummaas if wao tu ndo watanzania, wengine walioko sekta binafsi huenda ni wahamiaji haramu!!

Waziri anaamua kuuza sura kwenye runinga kwa kutangaza nyongeza ya mishahara ya sekta binafsi halafu anawapelekea barua waajiri/wawekezaji wa sekta binafsi kwamba msiongeze mishahara, enfdeleeni kulipa kidogo hivyo hivyo, unategemea mtoto asiharishe hapo kila siku!!??
 
I am sorry to say this...Kwa kweli ndani ya moyo naamini kuwa the last time we hand as serious premier ilikuwa ni Hayati Sokoine..

Hivi Pinda kama waziri mkuu wa nchi anawezaje ku-sanction kauli kwamba watanzania hawapati fursa za ajira kwa sababu ya kuwa na excuses. After all kila nchi ina social cultural yake.

Hivi WM anapaswa kusimamia policy na sheria za nchi au feelinga za wawekezaji? SHAME

Kwa upande wangu Kauri ya Mkuu yule ni moja ya kauri ambazo viongozi wetu wanazisikiliza toka kwa Wawekezaji [INVESTOR] na wao kuzipigilia msumali kuwa ni sahihi pasipo kuangalia UTANZANIA na MAZINGIRA YETU.Wanashabikia matakwa ya WAWEKEZAJI NA VIBARAKA WAO WA SIKU HIZI MAJIRANI WENYE KUJUA KWA UFASAHA LUGHA YA KIUWEKEZAJI.

Ndio maana WATANZANIA AWATAKI EAST AFRICA COMMUNITY,kwa kuwa wanajua watageuka MANAMBA ndani ya TAIFA LAO na viongozi wao ambao wanaafikiana na maneno yao.Watanzania wanautamaduni wao,sio kweli hawachapi kazi,watanzania uwa WANAHESHIMU MTU,AWAMNYENYEKEI MTU.

Ukiingia kwenye OFISI hizi nyingi za wawekezaji, watanzania ndio wafanyakazi wengi wa makampuni hayo [Nenda Migodini] utaona.Ninachokijua mimi binafsi kwa upande wangu OFISI nyingi za wawekazaji wale wanaoletwa kuja kuongoza ofisi za wawekezaji hawa na miradi ama shughuri zao wanakuwa hawana uwezo wa kuziendesha hivyo utumia BULLY STYLE MANAGEMENT kuwaendesha Watanzania KIUTAWALA.

Kwa kujua Serikali inawabeba na watanzania si watu wa kulalamika kwa kukabiliana uso kwa uso na hawa maafisa kwa kuzingatia mapungufu yao kwenye lugha ya kiingeleza.Kwa maana ya kujibizana kama ambavyo wangejibizana kwa lugha ya Kiswahili,uishi kunung'unika kwa kuwa hawana wa kuwatetea.Na kwa kuwa Mwalimu aliwajenga kuheshimu UTU basi wanabaki kwenye fukuto.,hivyo wakija mabwana wakubwa kama hawa ndio kabisa wanapigilia MSUAMALI WA MWISHO.

Mtanzania hana mtetezi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom