Wazee wauawa kwa kushindwa kumfufua mtu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
WAZEE wawili wa Kijiji cha Mpenje katika Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, wameuawa baada ya kushindwa kumfufua mwanakijiji mwenzao wanayedaiwa kumuua kwa kumloga.

Baada ya kuuawa kinyama kwa kukatwa mapanga, miili ya wazee hao Gasper Mwanisenga (70) na Noel Sangu (70), ililazwa juu ya kaburi la marehemu anayedaiwa kurogwa.

Mauaji hayo yalitokea Aprili 30,mwaka huu mchana wakati wakazi wa kijiji hicho walipokusanyika kwenye msiba wa mwanakijiji mwenzao ambaye jina lake halijapatikana, lakini inadaiwa alikufa ghafla baada ya kurogwa na kuzikwa kijijini humo.

Habari kutoka kijijini humo zinadai kuwa waombolezaji hao walikodisha wauaji watano baada ya kuthibitishiwa na mganga mmoja aliyewapigia ramli, kuwa wazee hao wawili Mwanisenga na nduguye Sangu ndio waliomroga.

Inadaiwa kuwa baada ya maziko ya anayedaiwa kurogwa, wauaji hao watano walifika msibani na kuwakuta waombolezaji wakila chakula, wakawaita Mwanisenga na Sangu na kuwataka wabebe sahani zao za chakula wawafuate.

Wazee hao na wauaji hao inadaiwa walikwenda katika kaburi na marehemu anayedaiwa kurogwa na walipofika, wauaji hao wakaanza kuwaamuru Mwanisenga na Sangu wamfufue marehemu lakini wazee hao wakajibu hawana uwezo wala karama ya kumfufua mfu.

Baada ya kutoa majibu hayo, inadaiwa wazee hao waliamriwa kula chakula walichokuwa nacho kama ishara ya kumaliza kuomboleza msiba wao wenyewe, huku wakicharazwa viboko.

Mmoja wa viongozi wa kijiji hicho aliwaeleza waandishi wa habari kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini kuwa wakati wauaji walipokuwa wakitenda uovu huo, kule msibani kulipitishwa bakuli la kuchangisha fedha za kuwalipa wauaji hao.

“Miili ya marehemu hao ilichomwa moto na watu wasiofahamika siku iliyofuata,” alisema kiongozi huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage amekiri kutokea kwa mauaji hayo na kuongeza kuwa chanzo chake ni imani za kishirikina na hakuna aliyekamatwa hadi sasa kwa kuhusishwa na mauaji hayo.
 
R.I.P. all of the the three guys. Natambua elimu duni ndo chanzo cha yote, siwalaumu sana.
 
This is happening in the 21st Century?? Mkoani kwa Waziri Mkuu wa Tanzania?? Kamanda wa Polisi anasema hakuna aliyekamatwa hadi sasa kutokana na mauaji hayo?? Mganga aliyepiga ramli na kuwataja marehemu kuwa ndio waliomuua marehehemu wa kwanza? Kama muandishi aliipata stori hii Mkuu wa Polisi na Jeshi lake ameshindwaje kuipata na kuifanyia kazi?????
 
Sijui tanzania tunaelekea wapi! hivi kweli?hapa jeshi la police tunaomba mkomeshe mchezo huu,uwezo huo najua mnao
 
R.I.P. all of the the three guys. Natambua elimu duni ndo chanzo cha yote, siwalaumu sana.
Unadhani ni elimu duni tu ndugu yangu? Mbona mpaka maprofessor wanapanga line kwa babu wa Loliondo amabye hata composition ya dawa yake haijui lakini watu kibao wamejaa kwake wakiamini kwenye ndoto ya ambayo hawawezi kuithibitisha kama kweli alioteshwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom