Wazee wamlaani Kikwete, Vikongwe watoa machozi; Wasema wamamua kufa! Serikali ya JK imewadhulumu

CCM walipeni hawa wazee hela zao hamuoni aibu nyie?lakini kumbukeni kwamba IN ONE NIGHT there is a BRIGHT DAY,mtaumbuka kwa mabaya mnayotufanyia,endeleeni kula na kunywa mtakavyo wakati wengine hawana uhakika hata wa kula mlo mmoja.
 
Hii hela lazima ilipwe!kama vipi wazee waandamane bila kukoma kuishinikiza serikali ya uingereza ilipe haki zao.
 
denoo49 itabidi utupe reference

2be honestly, ckufanikiwa kufanya recording, lakini kama "itv" watakua waungwana, wanaweza kutoa support kwa kuonesha japo marudio ya kipande cha habari ya mh.membe cku anaongelea kuhusu kesi ya pesa iliyozidi kwenye manunuzi ya rada
 
sasa hawa wazee ifike wakati Tuwasaidie kudai chao kwa nguvu ya Umma mana yake hii minyang'au Magamba bila ku4cwa haiwezi kuwalipa.
 
Kusema ukweli inabidi tuwaandike kwa mwezi mzima mpaka taarifa zifike vijijini kwa wazeee wote.
 
Jamani hameni sasa hivi muangalie thread hii ya Regia mtema jukwaa la siasa inasema hivi

Breaking News: Hali ni mbaya Tarime Polisi Watembeza Mabomu Usiku huu-Kina Lissu Wakamatwa
 
nchi yetu haina mwelekeo tena wazee nao tunawadharau na kuwaonea? wakati nchi za watu wazee wanaheshimika sana wanajengewa had i nyuma, wewe nenda ussr, europe asia na usa wazee wote wanaheshimika , sisi tunashindwa ku import hii kitu?
 
Wakifa ha wazee atapata laana
Karne hii bado unaamini superstitions za "laana"?

Thumbs up serikali kwa kutoingilia mahakama japokuwa unpopular judgment kama hii lazima itawa cast in bad light katika li nchi ambalo 95% ya watu hawajawahi kusikia dhana za "separation of powers" wala "utawala wa sheria."
 
Hao wazee wamezidi na wenyewe, CCM imewatenda sasa maana wao wanapenda sana kung'ang'ana nayo, waje Chadema tuendeleze mapambano!
 
I saw this coming ... mwaka jana wakati tukielekea kwenye uchaguzi kesi hii ilipigwa dana dana kwa kuwa serikali ilikuwa inajua madhara ya hukumu yake ingekuwaje kwa chama tawala. Wazee walipozwa na Jaji Ramadhani kwamba ameita jalada la kesi hiyo ili alipitie na kwamba haki yao wangepewa.

Wazee kwa imani yao wakajua kwamba mambo yatakuwa poa na Idara ya Mahakama ilijitahidi sana kutoa ufafanuzi wa dana dana za hii kesi, nikajua hapo siasa imeishaingia tayari. Wazee walikuwa wanawekwa sawa ili wasije wakahamishia hasira zao kwenye sanduku la kura. Hukumu ya kesi hii ilikuwa tayari tangu mwaka jana, tatizo ni kwamba Idara ya Mahakama siku hizi imeingizwa kwenye politics na matokeo yake hata baadhi ya hukumu zake zinakaa kisiasa siasa tu kwa kuzichelewesha au kukwepa kuzitoa kwa wakati unaotakiwa.

Mjengwa juzi kasema kwamba akina mama watu wazima wameanza kuonekana kwenye mikutano ya CHADEMA na hiyo ni dalili mbaya kwa CCM maana hiyo ndio ilikuwa ngome ya CCM. Haya yanayotokea sasa ni mtaji kwa CHADEMA, ipo siku hao wazee watapiga kura ya hasira na wala si mbali sana.

Mikutano ya kampeni ya CHADEMA mwaka jana ilikuwa na akina mama wachache na wazee wachache na ndio maana watu walikuwa wanasema wahudhuriaji wa mikutano ya kampeni za CHADEMA ni vijana ambao ni rahisi kurubuniwa na kubadilisha mawazo, sasa kuna dalili zote za ngome ya CCM kuanza kuingiliwa [wazee na akina mama], hapo tayari wameishapoteza idadi kubwa ya wapiga kura.

Kijana Nape ninamuonea huruma, maana akifunika kwenye hili, then linaibuka jingine. Chuki ya wananchi dhidi ya CCM inazidi kuongezeka na kuwagusa hata wale ambao hatukutegemea kwamba wangeguswa na ufedhuli wa serikali iliyo madarakani. Kitu chochote kibaya kinachofanywa na serikali, as long as serikali iliyo madarakani ni ya CCM, basi wananchi wanazidi kuichukia CCM na kuiweka mahali pagumu.

Kwenye CC na NEC iliyopita, walisema ufisadi ndo umewapa wakati mgumu sana, lakini sasa sio ufisadi tu, bali hata haya madudu ya mauaji na hukumu za kukandamiza haki za watu moja kwa moja. Unaweza kumchezea mtu asiye na njaa, lakini mtu aliye na njaa huwa hachezewi maana hasira yake ni mbaya sana. Wazee walikuwa wanajua watapata haki zao na hivyo kupunguza ukali wa maisha, lakini sasa maisha ndo yatazidi kuwa magumu, ninatamani 2015 ingekuwa mwakani.
 
Mkuu umesema kweli hii hali si shwari hata kidogo. Kule Tarime wameua, wazee wamewadhulumu, walimu walitukanwa, kila mahali CCm inachemsha sijui mwisho wake nini. Yaani imefikia watu wakiona rangi ya kijani mwana ccm anaongea kwenye runinga wanabadili channel hawataki kuona wala kusikia. Hii inamaanisha nini? Ngoja tuone
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom