Wazee wakitukana, vijana wajifunze nini?

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
Heshima zenu wakuu nyote!

Kwa muda uliopita takribani wiki moja na nusu kuna matukano yaliyotolewa na mzee kwenda kwa wazeee ambayo yameacha mwangwi hadi wiki hii ya sasa katika akili za wanajamii ya kitanzania.

Ndiyo, ni matusi ya Mzee Yusufu Makamba, kwenda kwa wazee wakina Matheo Qares, Nkhangaa, Butiku, Warioba, Dk. Salimu na wengineo ambao kama watanzania waliokula chumvi nyingi walikizungumza kile wanachokiona kilichopo sasa ambacho kinaamua hali yetu ya badaye. kama wazee wakatoa maoni yao na kwenda mbele ni kifanyike ili tanzania tuwe hatima njema.

Matusi ya mzee Makamba ni yale ya kuwaita wazee wenzake WEHU. Kwa lugha nyingine ni kuwafananisha na wendawazimu,vichaa watu wenye kuweweseka...ni matusi aliyoyatoa hadharani, na akataka yaandikwe na kusomwa hadharani[maana ndiyo makusudi ya kuwaita waandishi wa habari].

Katika jamii niliyokulia, nilikuwa sijapata kusikia Mzee (mwenye akili timamu) akimtukana Mzee mwenzake hadharani namna hii. Kwani hata kama mzee huyo ni mwongo, hawatamwambia mwongo bali watamwambia si mkweli.Tafsida ikitumika kupunguza makali ya neno husika. Ndiyo maana hata sophia Simba alivyomwaibisha mzee Malecele,chigwiyemisi hakutukana bali alitaka jamii ijiridhishe juu ya utimamu wa akili ya Sophia Simba kwa kushauri akapimwe Mirembe kabla ya kuondoka Dodoma.

Kutokana na tabia hii ya kutukana, na si kutukana tu bali ni kutukana hadharani, vijana watanzania wanaoandaliwa na wazee wa kitanzania wajufunze nini?

Ukitaka kupuuza swali hili, hebu kumbuka kauli za Tambwe Hiza dhidi ya hao wazee, Mwenyekiti wa UVCCM Moro dhidi ya Masishanga and the like.
 
Back
Top Bottom