Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
... WaTanzania sote TUMESHAAMUA kwamba mambo yote ni kwa CHADEMA, je ni nani tena wa kutuzuia?????????????
Wazee maarufu ndani ya Chama cha Mapinduzi, Dr Hassy Kitine,Mzee Ibrahim Kaduma na Mzee Joseph Butiku wametoa ya mwaka walipokuwa wakihojiwa katika luninga Channel 10, jumamosi.
Habari hii imejirudia katika gazeti la Mwananchi leo(Machi ,26, 2012) ikisema:
"Na Elias Msuya,
Makada watatu wakongwe wa Chama cha Mapinduzi( CCM), Ibrahim Kaduma,Dk Hassy Kitine na Joseph Butiku wameibuka na kukutabiria anguko chama hicho tawala kwa kile walichosema, kwenda kinyume na misingi ya kuasisiwa kwake.
Kauili za makada hao maarufu, zinakuja kipindi ambacho upepo wa kisiasa umekuwa ukivuma vibaya ndani ya chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika, kutokana na vita ya makundi kati ya watuhumiwa wa ufisadi na wale wanaojipambanua kwamba ni wazalendo na wapinga."
Maoni Yangu:
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu!