Wazee wa CCM wa Kawe wanataka 2015 nikamng'oe Mdee ila mi ni CHDEMA

Jipange vizuri kwani 2010 hata fedha za madawa ya kulevya ya chama cha magamba hazikufua dafu; Mdee anakubalika Kawe tafuta jimbo lingine!!
 
kuna baadhi ya viongozi wa cdm wanatembelea marekani zaidi kuliko wanavyotembelea majimbo yao:thinking:
 
Ben,
Huyu mzee Slaa akiomba tena kugombea urais 2015 mtampa nafasi?

Labda tujadili tafsiri ya uzee...pengine nikijibu swali hili kama unavyotamani ninaweza kuishia kupotosha watu.Nalinda hadhi ya hoja,JF na members wake!
 
Nenda kwani katiba inaruhusu, ballot box ndo itakayoamua, kwani Mdee kasems yeye atapita bila kupingwa? Hivi kila mtu wazee wazee ndo nani hao?
 
napenda sana kushindanishwa, na ni muumin wa siasa shindanishi


Huo uumini wako wa siasa shindanishi unakuambia ukashindane pahala palipokamilika? sio panapolegalega ili upaletee ubora zaidi? na ni kwanini usifanye hivyo kwa utashi wako binafsi mpaka ubuustiwe na wazee hao? anyway we jiandae 2015 sio mbali kihivyo kwenye ushindani kuna kushindwa na kushinda ulifahamu hilo mapema tuu.
 
yaani wewe ni mwanachama CDM,wewe binafsi unamkubali Mdee?Kama jibu ni hapana,wazee wa CCM walioona wewe unaweza kuwa Mbunge uliwapa nini hapo Kawe?Mbona kuna kijana aligombea kupitia CCM hapo Kawe wazee hao hao wa CCM wakamwambia angewafaa isipokuwa mkono mtupu haulambwi?Ndoto nyingine ni za hatari sana!Kama jibu ni kuwa unamkubali,nisamehe nikihisi bado wewe ni mtoto ambaye hujafikia umri wa kufanya uamuzi wowote kisheria,kwamba uko na miaka chini ya 18,tukusubirie ukomae ndipo utie timu Jf
 
CDM 4 LIFE.jpg
i like this kind of creativity . M4c .
 
Uongozi ndani ya CDM sio swala kung'oana, soma dira ya Uchaguzi CDM 2015

CHADEMA watoa dira ya Uchaguzi Mkuu 2015
Katika jitihada za kujiandaa na uchaguzi mkuu wa 2015 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka wanachama wake wenye nia ya kugombea ubunge na udiwani kuwasilisha barua za maombi, picha, vyeti, wasifu na jimbo wanalotaka kugombea kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu, tayari kwa maandalizi.Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema jana na kuwaagiza wanafunzi ambao ni wanachama wa Chadema wanaohitimu mwaka huu katika vyuo vikuu vya Mkoa wa Dodoma kufanya hivyo mara moja.

Akihutubia katika mahafali ya kuwaaga wanachama hao wanaosoma vyuo vikuu vya Dodoma, St. John’s na Chuo cha Biashara (CBE), Mbowe, alisema kila anayetaka kugombea awasilishe maombi na kwamba mwaka 2015 wagombea watakuwa wengi kwa kila jimbo ili kuleta ushindani.Alisema taarifa za wagombea hao zitafanywa kuwa siri na watakaojitokeza kugombea 2015 watapata mafunzo maalumu ya uongozi, kampeni na pia watapewa ajenda za kuzungumzia majukwaani wakati wa kampeni.
 
Huu siyo wakati wa mwanacdm kufikilia kumung'oa mwanacdm mwenzake hasa kwa mtu kama mdee ambae ni jembe na mwenye hoja kama zimepimwa na rula.bali ni wakati wamwanacdm kujipanga kuwang'oa ccm.ungekuwa unakwenda kumng'oa shibuda ambae ni gugu katikati ya ngano natumaini ungepata kura zote za ndio kwa wanacdm.
 
Back
Top Bottom