Wazee wa bagamoyo wafunguka!!!!!. -->-->--> chadema v

Mlalila

Member
Nov 19, 2011
35
17
Wakati WATANZANIA wanazidi kufunguka na kujitafakari, sasa wazee wa Bagamoyo wameona nuru ya CHADEMA na kuikaribia huku kukiwa na kundi kubwa la vijana hasa madriver boda boda ambao sasa wanasema mikwanja ya CCM tunalamba!!!!!!!, Kura mtosoooo wa kufa mtu!!!!!!!!.

Mkutano wa CHADEMA ambao ulifanikiwa kwa 100% ktk kukusanya wakaz wa bagamoyo bila kujal umri wao wala kazi zao hapo juzi. Katka mtuktano huo, watu walifunga barabara na mitaa ya Magomen sokon kiasi cha kutopitika kabisa utadhani ni siku ya gulio pale top top B/moyo. KWa kweli ulikuwa ni mkutano wa kihistoria kwa CHADEMA pale B/moyo. Wakati wa michango ya kumchangia mgombea Bwana SETEBE TIMIZA SETEBE, mtoto mmoja bila kulemba alichangia CHUNGWA ambalo badae liliuzwa kwa Tsh. 5,000/=.

Mara tu baada ya mkutano wananchi walitembea umbali wa kilometer 5 wakielekea maeneo ya eagle ambakon mzee mmoja mwenye kuona dira ya Tanzania ya Watanzania, bila kukosea alitundika bendera ya CHADEMA na ile ya magamba kuishusha. Kwa kweli kwa mkutano wa juzi, wakaz wa bagamoyo wamefunguka hasa kuunganisha mkutano na matembezi yaliyofuata ambavyo vyote kwa pamoja vilifanya vimekuwa mwiba mchungu.Big up CHADEMA!!!!!!!!!!!, Big up SETEBE!!! .Mwsho, Naomba msaada kuupload photo hapa JF, ujionee mwenyewe!!!!!.

Kwa sasa, spidi ya CCM kujimaliza imeshika kasi mpaka Bagamoyo. CCM kwishney!!!!!!!!!!!!!!.
 
Ni taarifa nzuri sana. Angalieni wasianze kuleta mikuki kudhuri wanachama wapya wa CDM. Maana CCM wako tayari kuua ilimradi warudishe mwanachama mmoja!!!!!!!!!

People's Power
 
Watanzania wanataka mabadiliko bila kujali kama mabadiliko hayo yatakuwa na faida kwao, wanacho taka ni mabadiliko tu, sasa CCM wanakuja na mbinu za kizamani za kupambana na makamanda wa CDM wanazani itasaidia, CCM wanatakiwa wapambane na wanachi na C CHADEMA,
 
Jipeni moyo nyinyi wafa maji, CCM haijawai kutetereka wala haija tetereka na haita tetereka. Tunaendelea na mambo ya kimaendeleo kwa waTanzania, siyo kupiga kelele kwenye mitaa ya watu, Tunamajukum mengi sana na hata nyinyi mnaojiita CHADEMA mnatutegemea kwenye huduma za jamii, ngoja tuhakikishe ustawi wa jamii kwanza.

Ushauri wabure,
mngeanza kuangalia majimbo yenu hali iliyopo kwa sasa na wapiga kura wenu wanavyojutia kujaribu kuchagua upinzani. Siyo kila kukicha mnazunguka kwenye maeneo ya watu wengine, majimboni kwenu hamna jipya hata kidogo.
 
Hapo ni Korogwe

Hii ndo offisi ya mwalimu
 
Hivi ili ujue ccm imefariki dunia unataka uone viwanda havitengenezi nguo za njano na kijani?
 
Nina mukar wa kuona hizo picha.
Kama unatumia PC njia fupi ni kui hold hiyo picha na kui drop kwenye text box (just like moving icon on your desktop)
 
Chasha

Usiwe mvivu kufikilia wewe,

Hivi huoni huo mjengo hapo nyuma unavyopanda kwa kaSi kubwa sana.
 
Last edited by a moderator:
Hivi ili ujue ccm imefariki dunia unataka uone viwanda havitengenezi nguo za njano na kijani?

CHADEMA. . . . !

kwani mkuu upo nchi gani?

juzi juzi tu CDM mmeangukia pua kule Mwanza au taarifa haijakufikia.
 
nadhani sasa imebaki tanga tu .............
Mara kwa mara mji huu umekuwa ukisahaulika na kila mara Chadema wakipanga kutua Tanga kwa ajili ya M4C inashindikana kutokana na kutokea vikwazo mbalimbali ikiwemo Helkopta kupata hitilafu mara wapangapo safari ya kwenda huko, mwishowe wanaghairi na kwenda miji mingine.

Huu mji unahitaji operesheni maalumu ambayo inatakiwa ichukuwe hata mwezi mzima kuwaelimisha wananchi wa hapo Tanga, kwani ccm imewaloga kwa muda mrefu na wamefungwa kabisa akili zao hawajui chama chochote zaidi ya ccm. Majimarefu ameizindika mipaka yote ya mji wa tanga kuhakikisha M4C haitui Tanga ila round hii hirizi zote alizozifukia ardhini zitatoka zenyewe, na upako utashuka Tanga hatimaye wanachi wa mji huo wapate mabadiliko ya kweli ikiwemo ukombozi wa kifikra.
 
Karibu kwetu chadema,Karibuni Bagamoyo,
Pekeee ni chetu chama, kututuliza mioyo,
Kwa wababa na wamama, vilema na vibogoyo,
CCM ipate zama, dua yetu ndiyo hiyo.

Karibuni magomeni, wananchi tuwashike,
Awape nguvu manani, Chalinze yote mteke,
Mkoa wote wa pwani, Ngome kuu ijengeke,
Kuwa chama upinzani, CCM kigeuke.

Hiyo kwetu ni hedaya, CCM kuanguka,
Hatofurahi Jakaya, kuona tunafunguka,
Lakini jueni haya, tumechoka kupigika,
Pasina hofu na haya, Njooni tutawashika.

Karibu kamanda Mbowe, Karibu na wewe Sugu,
Mkaribie Mbwewe, Chole na Misugusugu,
CCM muing'owe, Mng'oe na zake mbegu,
Waingiwe na kiwewe, waanzilishi vurugu.

CDM Daima.
 
Mara kwa mara mji huu umekuwa ukisahaulika na kila mara Chadema wakipanga kutua Tanga kwa ajili ya M4Cinashindikana kutokana na kutokea vikwazo mbalimbali ikiwemo Helkopta kupata hitilafu mara wapangapo safari ya kwenda huko, mwishowe wanaghairi na kwenda miji mingine.

Huu mji unahitaji operesheni maalumu ambayo inatakiwa ichukuwe hata mwezi mzima kuwaelimisha wananchi wa hapo Tanga, kwani ccm imewaloga kwa muda mrefu na wamefungwa kabisa akili zao hawajui chama chochote zaidi ya ccm. Majimarefu ameizindika mipaka yote ya mji wa tanga kuhakikisha M4C haitui Tanga ila round hii hirizi zote alizozifukia ardhini zitatoka zenyewe, na upako utashuka Tanga hatimaye wanachi wa mji huo wapate mabadiliko ya kweli ikiwemo ukombozi wa kifikra.

umenena vema mkuu maana naona yule profu kawashika pabaya sana tanga hawafurukuti ila naamini kiama chake kisiasa karibia kinafika maana hakuna ukombozi mkubwa zaidi ya ukombozi wa kifikra.......
 
Karibu kwetu chadema,Karibuni Bagamoyo,
Pekeee ni chetu chama, kututuliza mioyo,
Kwa wababa na wamama, vilema na vibogoyo,
CCM ipate zama, dua yetu ndiyo hiyo.

Karibuni magomeni, wananchi tuwashike,
Awape nguvu manani, Chalinze yote mteke,
Mkoa wote wa pwani, Ngome kuu ijengeke,
Kuwa chama upinzani, CCM kigeuke.

Hiyo kwetu ni hedaya, CCM kuanguka,
Hatofurahi Jakaya, kuona tunafunguka,
Lakini jueni haya, tumechoka kupigika,
Pasina hofu na haya, Njooni tutawashika.

Karibu kamanda Mbowe, Karibu na wewe Sugu,
Mkaribie Mbwewe, Chole na Misugusugu,
CCM muing'owe, Mng'oe na zake mbegu,
Waingiwe na kiwewe, waanzilishi vurugu.

CDM Daima.

Wewe ni mkali Mkuu!
 
Hongera Timiza Setebe.Pambana sana 2015 ugombee Ubunge wa Jimbo hilo!kila heri.
 
Back
Top Bottom