Wazee na madiwani Kyela kuunda tume kumuona rais juu ya ugonjwa wa Mwakyembe

BAGENI

Member
Jan 22, 2012
25
2
Katika hali isiyo ya kawaida leo wananchi wa wilaya ya kyela wamekutana maeneo ya viwanja vya siasa kyela mjini kujadili hatma ya jimbo lao pamoja na afya ya mbunge wao Dr.H.Mwakyembe, ambaye afya yake bado si shwari.

Wananchi hao wamejadili kuwepo haja ya kufanya safari ya kwenda kumjulia hali mbunge wao.

Mkutano huu umekuja huku kukiwa na tetesi kwamba huenda kiongozi huyo akaruhusu wananchi kuchagua mtu mwingine wakuendesha shughuli za kisiasa jimboni hapa.
[FONT=Tahoma, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]
Na Israel Mwaisaka, Kyela FM Radio

BAADHI ya Wazee na madiwani katika halmashauri ya wilaya Kyela wameazimia kuunda tume itakayokwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete ili kutaka kujua tatizo la ugonjwa anaougua mbunge wa Kyela na naibu waziri wa ujenzi Dkt,Harrison Mwakyembe.

Azimio hilo limefikiwa jana kwa pamoja kufuatia mkutano wa hadhara uliokuwa umeitishwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kyela na diwani wa kata ya Kyela mjini Bw, Gabriel Kipija ambapo moja kati ya ajenda za mkutano huo ilikuwa ni kutaka kuishinikiza serikali kueleza uwazi wa ugonjwa unaomsumbua Dkt, Mwakyembe hasa baada ya kutokea kwa mkanganyiko kwa baadhi ya watendaji wa serikali juu ya ugonjwa wa Mwakyembe.

Akizungumza katika kikao hicho mzee Benson Mwaikeke alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona serikali inakuwa na taarifa zinazokinzana miongoni miongoni mwa watendaji wake wa serikali ambapo taarifa ya DCI Manumba iliyosema kuwa Dkt, Mwakyembe akulishwa sumu imekinzana na taarifa ya waziri wa mambo ya ndani Vuai Nahodha ikiwa ni pamoja na ile ya waziri wa afya Dkt, Mponda.

Alisema kuwa kitendo hicho cha Dkt, Mwakyembe kuugua na kwenda kutibiwa katika hospitali ya kimataifa ya Apollo kule India wao kama watu wa Kyela wameumia kiasi kikubwa sana hivyo wanaposikia taarifa zinazokinzana juu ya ugonjwa wa Mwakyembe kati ya viongozi hao wa serikali ni bora sasa wamuonae Mhe. Dkt, Jakaya Kikwete ili aweze kubeba dhamana ya kuwaambia wananchi juu ya kile kinachomsumbua Dkt, Mwakyembe.

Diwani wa kata ya Bujonde Bw,Lameck Mwambafula kwa upande wake alisema kuwa ipo haja sasa kwa Rais ya kuhakikisha anamfukuza kazi DCI Manumba kutokana na taarifa yake ambayo anadai kuupotosha umma na kutaka kuuficha ukweli uliopo katika suala zima la kinachomsumbua mbunge wao na kuwa kutokana na hilo DCI Manumba amekosa sifa ya kuwa mtumishi ndani ya jeshi hilo la Polisi nchini na ipo haja ya kumfukuza kazi.

Mwenyekiti wa chama Cha NCCR-Mageuzi wilayani Kyela Bw,Robinson Fongo alisema kuwa umefika wakati kwa jamii sasa kuhakikisha kuwa wanafanya maandamano ya amani yatakayoishinikiza serikali kuweza kutoa taarifa sahihi na kuachana na ubabaishaji uliopo kati ya watendaji wa serikali na kudai kuwa hilo peke yake inaonyesha ni jinsi gani viongozi wa nchi hii wasivyokuwa pamoja na kufanya kazi kama timu moja inayopelekea kila mmoja kuzungumza anavyotaka yeye.

Alisema kwa hari hiyo hawataweza kupata taarifa sahihi za kinachomsumbua Dkt,Mwakyembe kwa maana viongozi wote wa serikali kila mmoja anatamka atakavyo yeye na kuacha maadili ya yanayowaongoza kwenye utumishi wa umma na kuwa njia pekee ni maandamano tu na kuunda tume ya watu kwenda kumuona mhe,Rais na kmpelekea ujumbe huo wa watu wa Kyela.

Akiitimisha hoja hizo mwenyekiti huyo wa halmashauri Bw,Kipija alisema kuwa hoja hiyo wataifanyia kazi haraka na kuunda tume ambayo itawashirikisha watu mbalimbali wa wilaya Kyela bila ya kujali itikadi za kisiasa kwani lengo ni kutaka kuunda umoja utakaoweza kumfikishia taarifa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema kuwa licha ya hoja hiyo pia watazingatia ushauri uliotolewa na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bw,Fongo ya kutaka kuitishwa kwa maandamano ya amani ili kuunyesha umma wa Watanzania kuwa sasa wamechoshwa na ubabaishaji unaofanywa na nchi hii
[/FONT]
 
Mkutano huu umekuja huku kukiwa na tetesi kwamba huenda kiongozi huyo akaruhusu wananchi kuchagua mtu mwingine wakuendesha shughuli za kisiasa jimboni hapa.
Sheria za Nchi haziruhusu ...

Nani atasimamia huo uchaguzi? Je, pia atapewa majukumu ya kuwawakilisha wananchi mjengoni? If so, ina maana jimbo litakuwa na wabunge 2? Nini mipaka ya hizo shughuli za kisiasa?
 
yawezekana anataka ajiuzulu ubunge na uwaziri. CHADEMA MPOO?? jimbo lenu hilo wala hamna haja ya kufanya kampeni
 
hawezi kujiuzuru we.inzi atafia kwenye kidonda madaraka matamu.nani atamlipia gharama za matibabu chezea india wewe.
 
Mkutano huu umekuja huku kukiwa na tetesi kwamba huenda kiongozi huyo akaruhusu wananchi kuchagua mtu mwingine wakuendesha shughuli za kisiasa jimboni hapa.
Nilisoma na kuamini habari ila nilipofika kwenye bold, nikaona huu nimuendelezo uleule wa walewale wanaomtakia mabaya Dr Mwakyembe.
 
Na Israel Mwaisaka, Kyela FM Radio

BAADHI ya Wazee na madiwani katika halmashauri ya wilaya Kyela wameazimia kuunda tume itakayokwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete ili kutaka kujua tatizo la ugonjwa anaougua mbunge wa Kyela na naibu waziri wa ujenzi Dkt,Harrison Mwakyembe.

Azimio hilo limefikiwa jana kwa pamoja kufuatia mkutano wa hadhara uliokuwa umeitishwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kyela na diwani wa kata ya Kyela mjini Bw, Gabriel Kipija ambapo moja kati ya ajenda za mkutano huo ilikuwa ni kutaka kuishinikiza serikali kueleza uwazi wa ugonjwa unaomsumbua Dkt, Mwakyembe hasa baada ya kutokea kwa mkanganyiko kwa baadhi ya watendaji wa serikali juu ya ugonjwa wa Mwakyembe.

Akizungumza katika kikao hicho mzee Benson Mwaikeke alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona serikali inakuwa na taarifa zinazokinzana miongoni miongoni mwa watendaji wake wa serikali ambapo taarifa ya DCI Manumba iliyosema kuwa Dkt, Mwakyembe akulishwa sumu imekinzana na taarifa ya waziri wa mambo ya ndani Vuai Nahodha ikiwa ni pamoja na ile ya waziri wa afya Dkt, Mponda.

Alisema kuwa kitendo hicho cha Dkt, Mwakyembe kuugua na kwenda kutibiwa katika hospitali ya kimataifa ya Apollo kule India wao kama watu wa Kyela wameumia kiasi kikubwa sana hivyo wanaposikia taarifa zinazokinzana juu ya ugonjwa wa Mwakyembe kati ya viongozi hao wa serikali ni bora sasa wamuonae Mhe. Dkt, Jakaya Kikwete ili aweze kubeba dhamana ya kuwaambia wananchi juu ya kile kinachomsumbua Dkt, Mwakyembe.

Diwani wa kata ya Bujonde Bw,Lameck Mwambafula kwa upande wake alisema kuwa ipo haja sasa kwa Rais ya kuhakikisha anamfukuza kazi DCI Manumba kutokana na taarifa yake ambayo anadai kuupotosha umma na kutaka kuuficha ukweli uliopo katika suala zima la kinachomsumbua mbunge wao na kuwa kutokana na hilo DCI Manumba amekosa sifa ya kuwa mtumishi ndani ya jeshi hilo la Polisi nchini na ipo haja ya kumfukuza kazi.

Mwenyekiti wa chama Cha NCCR-Mageuzi wilayani Kyela Bw,Robinson Fongo alisema kuwa umefika wakati kwa jamii sasa kuhakikisha kuwa wanafanya maandamano ya amani yatakayoishinikiza serikali kuweza kutoa taarifa sahihi na kuachana na ubabaishaji uliopo kati ya watendaji wa serikali na kudai kuwa hilo peke yake inaonyesha ni jinsi gani viongozi wa nchi hii wasivyokuwa pamoja na kufanya kazi kama timu moja inayopelekea kila mmoja kuzungumza anavyotaka yeye.

Alisema kwa hari hiyo hawataweza kupata taarifa sahihi za kinachomsumbua Dkt,Mwakyembe kwa maana viongozi wote wa serikali kila mmoja anatamka atakavyo yeye na kuacha maadili ya yanayowaongoza kwenye utumishi wa umma na kuwa njia pekee ni maandamano tu na kuunda tume ya watu kwenda kumuona mhe,Rais na kmpelekea ujumbe huo wa watu wa Kyela.

Akiitimisha hoja hizo mwenyekiti huyo wa halmashauri Bw,Kipija alisema kuwa hoja hiyo wataifanyia kazi haraka na kuunda tume ambayo itawashirikisha watu mbalimbali wa wilaya Kyela bila ya kujali itikadi za kisiasa kwani lengo ni kutaka kuunda umoja utakaoweza kumfikishia taarifa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema kuwa licha ya hoja hiyo pia watazingatia ushauri uliotolewa na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bw,Fongo ya kutaka kuitishwa kwa maandamano ya amani ili kuunyesha umma wa Watanzania kuwa sasa wamechoshwa na ubabaishaji unaofanywa na nchi hii
 
Ilo la maandamano ya amani naona ni jema pia ila tatizo lipo kwa polisi wetu hawa sijui huwa kwao Amani means FUJO!
 
Mimi naona hawa wazee na Madiwani waKyela wamechelewa saaaana.
Kwani walikuwa wapi muda wote huu? Kwanini hawakuanza kuhoji tangu wakti ule Mbunge wao alipolalamika kuwa kuna kikundi cha watu kimetumwa kuja KUMWUA/KUMMALIZA yeye na baadhi ya Wabunge wanaopinga UFISADI nje na ndani ya CCM? Kwa hili hakika wamechelewa saana.
 
Ukombozi wa nchi u karibu sana, hakika waliobeza na kujiita mungu mtu wataaibika kwani Mungu ni mmoja tu!
 
Kuna mkuu mmoja hapa JF aliwai kuleta uzi mmoja makini sana kuwa "Hakuna haja ya kumuonea huruma Dr Mwakyembe,kwani anavuna alichopanda" kwa hiyo nyie watu wa Kyela tulieni...
 
Watu waliohudhuria huo mkutano hawakuzidi hata 50 japo ulitangazwa kwa muda mrefu.

Kweli kyela sasa siasa zimewachosha sana. Sio tena Kyela ile ya Mwakyembe kupata ajali 2009 ambapo watu walijazana makanisani kuomba apate nafuu. Kyela ya 2012 kila mtu anaangalia mambo yake na ugumu wa maisha.
 
Kuna mkuu mmoja hapa JF aliwai kuleta uzi mmoja makini sana kuwa "Hakuna haja ya kumuonea huruma Dr Mwakyembe,kwani anavuna alichopanda" kwa hiyo nyie watu wa Kyela tulieni...

Haya yangu macho na masikio.
 
badala waunde tume ijadili kwa nin kyela pamoja na kuzalisha mpunga mwingi bado maskini wanaenda kujadili mtu mmoja ambaye ujinga wake ndio umemponza
 
Mm naona haina haja ya Raisi kueleza kinachomsibu Dr Mwakyembe kinachotakiwa kufanyika hapa kwa huyu Dr Mwakyembe yeye mwenyewe awaambie watanzania kinachomsibu na tena itakuwa vizuri ikiwa ile ripoti ya Ugonjwa wake kutoka Hospitali Apollo nchini India akiiweka wazi kwa watanzania!
 
WAZEE wilayani Kyela wametoa tamko zito kuhusu utata uliojificha juu ya ugonjwa usiojulikana unaomtafuna, Mbunge wao, Dk. Harrison Mwakyembe, na kufikia hatua ya kutaka kwenda Ikulu kumwona Rais Jakaya Kikwete awaambie Watanzania endapo mtoto wao kapewa sumu au ni ugonjwa wa Mungu.Wazee hao walikwenda mbali zaidi kwamba wanakusudia kufanya maandamano ya amani ili kuishinikiza serikali iseme ukweli juu ya tatizo hilo kwa kuwa taarifa nyingi za mawaziri na viongozi wa polisi zinapingana.

Katika mkutano huo wa wazi, baadhi ya wazee walitoa kauli ya kutaka baadhi ya viongozi na mawaziri wawajibike kwa kutoa taarifa za uongo.Mzee, George Mwakabumbi alisema wamefika mahali pa kujilaumu kwa uamuzi wao wa kumshauri Dk. Mwakyembe agombee ubunge wa jimbo hilo kwa kuwa wakati wananchi wa Kyela wakiumia wengine wamegeuza sherehe. Mwakabumbi alisema kuwa umefika wakati wanaona bora mbunge huyo aachane na siasa na kwenda kufanya kazi zake alizozizoea.

“Sisi tumeumia sana kuhusu ugonjwa anaougua kijana wetu, tunashindwa kuelewa ukweli ni upi; ni serikali yenyewe ndiyo iliyompeleka nchini India inashindwaje kutueleza anachoumwa Dk. Mwakyembe? “Kila mtu anasema lake, waziri huyu anapingana na huyu, wanatupa picha gani, kuna siri gani? Sasa tunataka Rais Kikwete atuambie.”
Kikao hicho kilichoonekana kuwa na mchango mkubwa na kutafuta sababu za kina za kutaka kujua chanzo cha ugonjwa huo, baadhi ya wazee hao walikwenda mbali zaidi wakimtupia lawama, Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa ameshindwa kuonyesha ushirikiano wa kutosha pale aliposema kuwa mwenye mamlaka ya kusema ugonjwa huo ni Dk. Mwakyembe mwenyewe au daktari wake.

Mzee Benson Mwaikeke alisema kitendo cha mawaziri wa serikali inayosimamiwa na Rais Kikwete kila mmoja kutoa taarifa yake juu ya kile ambacho anakiamini kuwa ugonjwa huo sio wa kawaida, kinawaacha njia panda huku akidai kuwa chochote kitakachotokea wao ndiyo wa kulaumiwa.
Alisema kuwa haiwezekani kuwe na mgongano wa taarifa zinazohusu ugonjwa na mazingira ya mashaka yanayoonyesha kuwa vita vyao vya kisiasa ndani ya serikali na chama tawala imechangia kuficha siri ya ugonjwa huo na kumfanya mbunge wao aendelee kuumia.

“Haiwezekani, DCI Manumba anasema Mwakyembe hajalishwa sumu, Waziri wa Mambo ya Ndani anamkana DCI, Waziri wa Afya anasema hajui DCI alipotoa wapi taarifa hizo, Waziri Mkuu anasema siri ni ya mgonjwa, Waziri Sitta anasema kalishwa sumu, hivi kuna nidhamu gani ndani ya utawala wa serikali ya Kikwete? Sasa tunataka Rais Kikwete atuambie Mbunge wetu anasumbuliwa na nini,” alisema Mwaikeke.

Ipyana Mwakila aliwashauri wazee wenzake kwamba waunde kamati ya kwenda kumuona, Rais Kikwete Ikulu ili kuhoji kinachomsibu Dk. Mwakyembe.
“Hakuna njia nyingine inayoweza kuwaridhisha wakazi wa wilaya hiyo ili angalau waweze kupata ukweli wa mambo baada ya kubainika kuwa taarifa nyingi zinazotolewa na mawaziri hao hazina ukweli wa kutosha huku taarifa hizo zikiendelea kuwaumiza wananchi wa Kyela,” alisema. Aliwatupia lawama mawaziri hao, DCI Manumba kuwa anapaswa kujiuzulu kwa kutoa taarifa za uongo na zinazopingwa na Wizara ya Afya huku wakijua fika kuwa Wizara ya Afya ndiyo yenye jukumu la kusema ukweli juu ya ugonjwa wa Dk. Mwakyembe.

Wakati wazee hao wakitoa kauli hizo, baadhi ya vijana waliokuwa kwenye mkutano huo, walimjia juu Waziri Mkuu, Pinda, kwamba ana tatizo la kutokuwa mwepesi wa kutoa maamuzi ya msingi kwa nafasi yake aliyonayo kiasi cha kuwaacha wasaidizi wake wakisema wanachotaka bila kupima ukubwa wa tatizo hilo. “Mizengo Pinda amekwishashindwa kama kuna Waziri Mkuu mwenye kiwango cha chini katika kutoa maamuzi magumu tangu nchi hii ilipopata uhuru basi si mwingine ni Pinda, yeye mwenyewe anakuwa mtu wa kwanza kulalamikia kila kitu na kwa mambo mengi.

Timoth Kisungujila, hakimu mstaafu na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo alisema kuwa nidhamu imepotea serikalini na kwamba haiingii akilini katika nafasi za viongozi hao kila mtu anatoa taarifa za uongo kwani kutokuwa mkweli kazini ni kuvunja sheria. Mkutano huo wa wazi uliowashirikisha wazee maarufu na vijana pia ulitoa kwa ujumla tamko la wananchi wa Kyela la kuiomba serikali iwaeleze Watanzania, hususan wananchi wa jimbo hilo kutokana na mkanganyiko unaohusu ugonjwa wa Dk. Mwakyembe ambaye kwa sasa yuko nchini India akiendelea kutibiwa.

Nafuu hata ya Wazee hawa kidogo wana Upeo, wanajua nini wanachofanya,
Kuliko wale wachawi wa Kishihili ambao wao kutwa kuchwa kazi kukalia majungu tu.
 
Back
Top Bottom