Tz-guy
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 436
- 88
Hili swali nimelijibu huko juu, Sykes ana umuhimu kwani Ndio muasisi wa TAA kabla Nyerere hajaanza kujihusisha na siasa, ni Muasisi wa TANU na ndiye aliyetia jina la TANU na ndiye alimpokea Nyerere akamuweka nyumbani kwake na mengine mengi sana, Mohamed Said kaandika historia yake. Ni furaha kubwa kuona kuwa Mohamed Said hakuleta "porojo" kama wengi humu JF waliokuwa wanataka ieleweke, mpaka Rais wa JMT kamtaja rasmi kwenye kilele cha sherehe ya miaka 50, tunafarikika kuona kuwa kazi ya Mohamed Said haikupotea bure.
Inaonekana huyu Sykes unamkubali zaidi kwasababu alimkaribisha Nyerere nyumbani kwake na pia alikuwa muasisi wa TANU (Japo ni hoja nzito pia). Kama kuna hoja nyingine naomba uniambie ili nijue ni uhodari gani zaidi aliouonesha katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika mpaka ukamfurahia zaidi ya hao wengine.