Wazazi wa kambo

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
13,544
21,004
Hivi kwa nini mengi ya manyanyaso ya wazazi wa kambo kwa watoto yanafanywa sana na wanawake (mama wa kambo) na si wanaume (baba wa kambo)?
 
Hivi kwa nini mengi ya manyanyaso ya wazazi wa kambo kwa watoto yanafanywa sana na wanawake (mama wa kambo) na si wanaume (baba wa kambo)?

Nani hukaa na watoto zaidi - baba au mama? Nani huhudumia watoto zaidi siku hadi siku?
Manyanyaso ni relative.
 
Usikimbie swali mama wanawake wengi wanaroho mbaya
Ndugu
Siyo swali la wanawake au wanaume na roho mbaya.Ni ukweli tu wa maisha. Unaweza kuwa na roho mbaya sana lakini usijulikane kwa vile hukutani na watu kivile.
na unaweza kuna na roho nzuri sana lakini ukaonekana uko mkataili kwa vile unataka standards fulani ( I am in this category by the way) mwisho wa siku utashukuriwa mno maana utaleta ubora kwa mtu na maisha yake.
 
Usikimbie swali mama wanawake wengi wanaroho mbaya

Si kweli kwamba wanawake wana roho mbaya, mazingira ya kulea hao watoto yanawza kuwafanya waonekane wana roho mbaya.
Mama hukaa na mtoto muda mwingi na ndie anajua shida za kukaa na mtoto huyo baba wala anaweza asijue huyo mtoto anapata wapi chakula, nguo na mahitaji yake muhimu. na mara nyingi mtoto akishajua huyo si mamake huanza kiburi na mama inabidi awe mkali ili kuweza kukababiliana na kiburi cha mtoto na hpo ataonekana anamnyanyasa mtoto.
 
Kuongezea kwenye "roho ya ukatili":

Wanawake wengi ndiyo hufanya "mapinduzi" na hivyo watoto anaowakuta humchukia hata kabla hajawa "mama wa kambo"!
 
nina rafiki yangu, msomi na digrii juu... jamaa mkatili sana kwa mademu... kurusha mvua ya matusi/makofi kwa mwanamke ni kama kuwasha taa ya umeme... baadae wababe wenzake tulimvyombana atuambie sababu ya tabia hiyo... alikiri kuwa alilelewa na mama wa kambo na alimnyanyasa sana.. hivyo hataki tena kuhisi anadharauliwa na mwanamke yeyote!!!:confused2:
 
Hivi kwa nini mengi ya manyanyaso ya wazazi wa kambo kwa watoto yanafanywa sana na wanawake (mama wa kambo) na si wanaume (baba wa kambo)?

Kwa kifupi ni kuwa mwanamke ana uhakika wa watoto ambao ni wa kwake na wasio wa kwake. Kwa mwanaume hata wale anaodhani kuwa wa kwake( hata wale waliozaliwa katika ndoa yake)inawezekana kuwa siyo wa kwake. Labda ndio maana wanaume hawahangaiki kubagua kwani hakuna maana yoyote.
 
it sound
 
Hivi kwa nini mengi ya manyanyaso ya wazazi wa kambo kwa watoto yanafanywa sana na wanawake (mama wa kambo) na si wanaume (baba wa kambo)?
ila watoto waliolelewa na mama wa kambo katili, wakiwa watu wazima halafu wawe na akili iliyotulia, huwa wanakuwa watu wazuri sana coz wanajua shida ni nini, ukatili sijui ni maumbile? nafikiri ni kitu ambayo mtu hawezi kupretend lazima atajisahau tu!! (me hate mama wa kambo katili) ila kuna wengine wako poa kweli kweli yaani roho muzuri mpaka basi. Big Up Mothers:preggers:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom