Wazazi,ndugu hawamtaki,na yeye hataki kuelewa,ushauri wako unahitajika sana hapa!!

Utakua hujampenda.... Pamoja na kusema wanandugu ni mhimu kuwahusisha haya maswala, the way you have presented hapa ni kana kwamba wana absolute say ya Mwanamke wa kumuoa. Naamini kama Kweli unampenda kwa dhati, ni lazima zipo tabia ambazo zimekuvutia kwake... tabia ambazo ungeweza zisimamia kwa kuzitaja na kumtetea Mpenzi wako kwa ndugu zako... Kwanza nashangaa nyie ni kabila gani for haya mambo sasa hivi ya kabila sio shida saana kama dini.

AshaDii

umenena vema,
tatizo hapa ni kabila siyo mtu,yaani they are not ready to hear anything kiwe kizuri/kibaya........................
kabila linamhukumu ndugu yangu!!! pamoja saaaNA
 
Hivi huyo binti anaolewa na wazazi wako au na wewe??
Una maamuzi gani juu ya binti huyo wewe km mwanaume?
Mchunguze tabia yake, je anafaa kuwa mkeo au tabia yake imefanana na hao waliowahi olewa na nduguzo?
Ila ni kweli kabisa hujampenda huyo binti na ulikuwa unampotezea tu muda wake!!! :smash:
 
i missed u,u hali gani?
 
Katika mambo ya kuoa ni muhimu kutazama pia kabila, si unavamia tu.

Msisumbuke kunipiga swali hapo mana sita wajibu.

unajua siku hizi vijana tunajidanganya,ooh,tumesoma na tunayapeleka mambo kisasa. Huu ni ******! Kuna mambo ambayo yapo lakini exeptions zipo pia. Tuishi kwa kutegemea hizo rare exeptions? Sishabikii mambo ya ukabila,ila kuna makabila the way walivyo yanaifanya jamii nyingine iwaogope. Kama mtu umeona ndoa kumi za aina hii na inayodumu ni moja kwa nn na wewe ujiingize huko? Haya mambo ya kukutana vyuoni/njiani na kuanza kupanga kuoana ndo yanayopelekea ndoa nyingi siku hizi hazidumu. Ndoa ni mtihani unaoufanya mara moja tu,ukifeli maisha yako ya kimahusiano hayawezi kutengamaa tena. Wazazi wana nafasi yao lakini sio absolute. Nna ndugu zangu waliopuuza ushauri wa wazazi wameishia kuoa mke wa pili baada ya ndoa ya kwanza kuyumba. Tusilete mambo ya born after computer kwenye mambo ambayo ni ya kudumu. Hatuna ndoa za mkataba sisi!
 
Tatizo la watu wengi ni kuifanya ndoa kuwa bidhaa ya familia au jumuiya fulani.Ndoa ni mke na mume.Basi.

mbona mnapogombana mnaanza kuomba ushauri kwa ndugu, jamaa na marafiki? Kwa nini uwashirikishe kwamba unataka kuoa au kuolewa? Ingekuwa hivyo basi unamaliza mambo yako na unakuja naye na kuwaambia ndugu zako huyu ndo mke wangu nimeoana naye. Matatizo yakitokea mnayamaliza wenyewe huko huko. Kwenye hizi extended family zetu ni ngumu kuwa na maamuzi yako peke yako. Kuna ndugu zako ambao nao wanahitaji unafuu wa aina fulani wakiwa wamechoka wapate hata mtu wa kuwapeleka japo hospitali. Wakishakuwa na experience na kabila fulani ni ngumu kukubali mtoto wao uje kuwa wa aina hiyo. Inaumiza kuona tunajadili mambo ya ukabila lakini kwenye maisha ambayo ni kufa na kufaana inabidi yawe na umuhimu wake. Hii siyo ajira ambayo ukishindana na wafanyakazi wenzio unahama.
 
nina msimamo kuliko hata huyo mumeo/mpenzio sema mimi siendeshwi na hisia zaidi kuliko kutumia akili.......nampenda sana mpenzi wangu lakini wazazi wangu ni zaidi yake mara100,mapenzi ya kijinga jinga ya kujifanya unaendekeza moyo wakati ndoa ni step muhimu sana kwenye maisha,mimi sina nafasi hiyo.....hapa nyie nisaidieni tu jinsi ya kuachana nae kwa amani!!

Muoneshe huu uzi na usifute wala kuedit hata comment yako moja!!
 
We kwani kabila gani?Ebu usituzingue hapa, yani karne ya 21 mnaulizana na kubaguana kwa makabila? Mi najua/nahisi kabila lako ni lipi kwa vile nawajua maadui wa wachaga. Lakini mi naona nyie bado mnahitaji ukombozi wa kifikra, hasa hilo kabila lenu wa*******
 
mbona mnapogombana mnaanza kuomba ushauri kwa ndugu, jamaa na marafiki? Kwa nini uwashirikishe kwamba unataka kuoa au kuolewa? Ingekuwa hivyo basi unamaliza mambo yako na unakuja naye na kuwaambia ndugu zako huyu ndo mke wangu nimeoana naye. Matatizo yakitokea mnayamaliza wenyewe huko huko. Kwenye hizi extended family zetu ni ngumu kuwa na maamuzi yako peke yako. Kuna ndugu zako ambao nao wanahitaji unafuu wa aina fulani wakiwa wamechoka wapate hata mtu wa kuwapeleka japo hospitali. Wakishakuwa na experience na kabila fulani ni ngumu kukubali mtoto wao uje kuwa wa aina hiyo. Inaumiza kuona tunajadili mambo ya ukabila lakini kwenye maisha ambayo ni kufa na kufaana inabidi yawe na umuhimu wake. Hii siyo ajira ambayo ukishindana na wafanyakazi wenzio unahama.

Among watu walioongea vitu vya maaana na msingi ni pa1 na wewe mkuu
unajua hapa jamvini si kwamba watu hawafahamu reality ya hii ishu,wanafahamu sana sana ila tu,wanaamua kuleta ushabiki wa kipuuzi na kuendekeza mapenzi ya kizungu wakati sisi ni waafrika na tuna mila na desturi zetu tunazopaswa kuzifuata na kuheshimu,
hata ktk amri 10 za mungu,kuna amri inatutaka kuwaheshimu wazazi
 
nina msimamo kuliko hata huyo mumeo/mpenzio sema mimi siendeshwi na hisia zaidi kuliko kutumia akili.......nampenda sana mpenzi wangu lakini wazazi wangu ni zaidi yake mara100,mapenzi ya kijinga jinga ya kujifanya unaendekeza moyo wakati ndoa ni step muhimu sana kwenye maisha,mimi sina nafasi hiyo.....hapa nyie nisaidieni tu jinsi ya kuachana nae kwa amani!!

Badirika ujinga mzigo kwn wazaz wako, ndugu zako na marafik ndio wataishi nae huyo bint bado unanuka maziwa.
 
Among watu walioongea vitu vya maaana na msingi ni pa1 na wewe mkuu
unajua hapa jamvini si kwamba watu hawafahamu reality ya hii ishu,wanafahamu sana sana ila tu,wanaamua kuleta ushabiki wa kipuuzi na kuendekeza mapenzi ya kizungu wakati sisi ni waafrika na tuna mila na desturi zetu tunazopaswa kuzifuata na kuheshimu,
hata ktk amri 10 za mungu,kuna amri inatutaka kuwaheshimu wazazi
Kama wewe unayaona hayo ni ya maana sasa hapa JF AMELETA HIYO MADA YAKE ILI IWEJE?? watu wengine bana hovyo kweli!!
 
Mimi nahisi damu wa jamaa atakuwa mmachame manake wanawaogopa kama ukoma.Lakini ukiniambia mrombo au wengine atakuwa amenipa wasiwasi kidogo
 
its all about money
sio kwa wachaga tu ni kwa kila mtu siku hizi

hata hao ndugu zako wanajifanya wanakupenda saana na kukushauri
ni kwa sababu 'una kitu' otherwise

ungekuwa juu ya mawe na huyo mwanamke ndo mwenye michongo ya kutoka

wasingenyanyua midomo yao.........

ndugu zako nao wanajipanga kunufaika na wewe..

hawataki mwanamke atakaekuwa mkali kuwazuia......full stop.....

ungekuwa lofa wasingejishughulisha na wewe
 
Tuspende kuhukumu kijiji chote kwa kosa lililofanya na mmoja wa wanakijiji...
 
Wakati umefika ukoo wenu wote mtangaziane MAFURUKU kuoa au kuolewa na kabila fulani ili muache kuchezea wenzenu hisia zao halafu kuwaletea vijisababu vya kizamani, period. :smash:
 
sababu ni mchaga,kwa iyo wachaga ndio awatakiwi kuolewa?pelekeni ujinga wenu uko we na awo wanaokushauri ******

Mangi Meli hebu kishauri hiki "chasaka" manake hakitambui kinachoandika huku!.. Bora angetuambia sababu zenyewe ili tuweze kumshauri!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom