Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
Naomba kichwa cha habari kisomeke; Wazazi msiwaambukize watoto wenu chuki dhidi ya wazazi wenzenu
Wapo watu waliozaa, na kwa sababu moja au nyingine hawaishi pamoja. Wapo baadhi ya watu (hasa wamama) ambao kwa sababu fulani wamekorofishana na wazazi wenzao au wamekimbiwa au kutelekezwa na wazazi wenzao. Naomba ninene nao...
Acheni tabia ya kuwapandikiza chuki watoto hawa dhidi wa ya wazazi wasioishi nao
Acheni kuwakataza watoto hawa kuwajua au kuwaona wazazi wao wasioshi nao
Ugomvi wako na baba mtoto au mama mtoto wako uishie kati yenu, usiuambukize kwa mtoto
Wakati mnafikiria kuwa mnawakomoa au kuwaadhibu hao wenzenu, jueni kuwa mnapandikiza ugonjwa mbaya sana wa kisaikolojia, ambao baadae utakuja kumdhuru mtoto mwenyewe, watu wengine (akiwepo mwenzi wake wa ndoa) au hata wewe mwenyewe
asanteni