Wazawa wakaribishwa kuwekeza sekta ya gesi

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa JUSTIN NTALIKWA ametembelea mradi wa gesi wa SONGOSONGO wilayani KILWA, mkoa wa LINDI
image.php


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa JUSTIN NTALIKWA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa JUSTIN NTALIKWA ametembelea mradi wa gesi wa SONGOSONGO wilayani KILWA, mkoa wa LINDI na kusema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza uzalishaji wa gesi hapa nchini na kupunguza matumizi ya nishati nyingine kwa zaidi ya asilimia tisini.

Profesa NTALIKWA ametembelea eneo ambalo kisima cha kuzalishia gesi kijulikanacho kama SS12 kinachimbwa na kampuni ya PAN AFRICANISM na kuridhishwa na utendaji kazi unaoendelea.

Kuhusu wazawa wenye uwezo kuwekeza katika sekta ya gesi Profesa NTALIKWA amesema milango ipo wazi na kuwataka kujitokeza kwaajili ya kufanya uwekezaji huo.

Katika hatua nyingine serikali imetakiwa kusomesha na kutoa motisha kwa wazawa hususani katika fani za petroli na gesi.

Mradi wa gesi asilia ya SONGOSONGO uligundulika rasmi mwaka 1974 na kuanza kutumika rasmi kibiashara mwaka 2004 ambapo mpaka sasa visima SABA vinazalisha gesi yenye futi za ujazo wa 155 na kukamilika kwa mradi wa kisima cha SS 12 kutafanya gesi inayozalishwa kufikia futi za ujazo 200.



Chanzo: Wazawa wakaribishwa kuwekeza sekta ya gesi - TBC.go.tz

02 Februari 2016
 
Back
Top Bottom