Wazanzibari Wenyewe Mnajirudisha Nyuma: DR. Salim

Masatu;

hao unaowasema weye hawapo Zanzibar au Pemba.

Ni sawa na kusema Tanzania tuna ma dakitari wengi halafu 60% yao wapo Botswana ...

Ur missing the point, mjadala hapa sio wazanzibari waliopo zanzibar tu bali wote kwa ujumla wao katika mada pana ya muungano.

Hata hivyo hao unawaona hawana elimu ya magharibu ndio wenye upeo mkubwa katika suala zima la elimu ya uraia na hilo linathitishwa na chaguzi zao zinakuwa na ushindani kuliko sisi wenye elimu ya magharib lakini kofia, kanga, Tshirt nk vimetosha kubadili mtu msimamo wake.
 
Sijamiss the point ila kwenye letu la bara UMEGONGA IKULU.
 
Ukweli utabakia pale pale kuwa Hawa ndugu zetu wengi wao hawajaenda shule ya ki magharibi.

Uwezo wa kutoka nje ya box inakuwa ndogo.

Hilo ndo tatizo. Mimi huwa nawafananisha na wa Pelestina!

Ngoja nikimbie kabla ya mawe kurushwa humu!
Mijitu iliyotoka huko utumwani ndo ilivyo, inapandikizwa visiwani kuharibu muruwa wa watu halafu wanajidai kutoa vijisababu vya kijinga jinga, wasomi kuweni nyie na elimu ya kijinga ya kimagharibi yaani Utamaduni kwao ni ushoga na umalaya, Siasa udikteta, Uchumi ni ubepari na ufisadi, bora ujinga wetu tunamjua Mungu kuliko werevu wenu wa kimgharibi mnamjuwa bilisi.
 
mijitu iliyotoka huko utumwani ndo ilivyo, inapandikizwa visiwani kuharibu muruwa wa watu halafu wanajidai kutoa vijisababu vya kijinga jinga, wasomi kuweni nyie na elimu ya kijinga ya kimagharibi yaani utamaduni kwao ni ushoga na umalaya, siasa udikteta, uchumi ni ubepari na ufisadi, bora ujinga wetu tunamjua mungu kuliko werevu wenu wa kimgharibi mnamjuwa bilisi.

lol.................lmao!!!!
 
Ukweli utabakia pale pale kuwa Hawa ndugu zetu wengi wao hawajaenda shule ya ki magharibi.

Uwezo wa kutoka nje ya box inakuwa ndogo.

Hilo ndo tatizo. Mimi huwa nawafananisha na wa Pelestina!

Ngoja nikimbie kabla ya mawe kurushwa humu!

Hivi ndugu elimu ni ya kimagharibi tu? elimu katika maisha inakuja kwa njia tofauti na shule ni mojawapo tu, kama wewe unaitumia hiyo elimu basi ungelifahamu hilo. Hivi una takwimu yoyote inayoweza kulinganisha per capita ya wasomi walioenda shule ya ki magharibi Tanzania Bara na Visiwani?, tuletee tuone - sio unaongea tu, hata literacy rate ya Tanzania bara haiifikii Zanzibar - unajua hayo au ushabiki na pride zisizo mbele wala nyuma?.
 
Watz tuache kumpenda mtu kwa sababu tu aliwahi kuwa katibu mkuu AU au kwa s ababu tu aliwahi kuwa afisa wa ngazi za juu wa UN bali tumpime kwa kile alichokifanyia nchi yetu!Likely akiulizwa hapa sasa hivi ndugu Masatu ni sababu gani "cardinal"anaweza kutupa kuhusu mchango wa Dr salim na uimarishaji wa znz kuwa kitu kimoja kudai haki zao toka mwaka 1963 hadi leo?Huwa mimi binafsi sipati lolote la maana alilofanya!
Dr Salim anazungumzia leo kuhusu kushikamana kwa waznz kudai haki zao ili hali kwa zaidi ya miaka 40 alipokuwa na nafasi nono za kimataifa na za ndani hakufanya hivyo!leo hii ujasiri huo kautoa wapi?iweje asubiri hadi CCM imtenge ndiyo acharuke?
Nasisitiza tena,tulia kwako nyumbani,tz itakombolewa na wengine wewe umeshindwa kufanya lolote la maana na sana sana anaona tu aibu!
Mungu iweke roho yake peponi simba wa vita vya ukweli kuhusu kuwa kitu pamoja wanzn hayati Othaman Haroub na kamwe Dr salm huwezi kuwa "role model'wa wanzn wa kizazi kipya kuhusu kuondoa tofauti zao za kikanda,ulishindwa kufanya hivyo mwaka 1984 ulipokuwa PM au miaka ya ya 90 ulipokuwa General sec wa OAU utaweza leo?

Don't kill the messenger. Naona unamchambua mjumbe badala ya ujumbe wake, Dr. Salim inawezekana kuwa hana credibility mbele ya wa Zanzibari lakini aliyosema ni ukweli mtupu sasa kuanza kumsakama yeye badala ya ujumbe wake ni makosa na ndio haya haya aliyoyazungumza yeye. Ukweli ni ukweli tu hata akiuzungumza nyani - tuache hizi siasa za kuwasakama watu badala ya kuzichambua fikra zao.
 
Kaeni saa mbaya huenda uchaguzi Mkuu ujao wa 2010 usifanyike Pemba ,nilipotembelea huko katika ziara yangu ya Mikoa mitatu ya Tanganyika na kule Zanzibar na Pemba ,wenyeji wa Pemba wanasema wako njiani kuitia Nchi yao Mikononi na wana tamaa kubwa sana.
Ila uhakika wa kweli sikuweza kuupata maana wanasema mambo yao yanatambaa kama mito ndani ya bahari .
 
kwa hiyo hayaonekani! Mkuu umeadimika kweli hapa jamvini!
 
kwa hiyo hayaonekani! Mkuu umeadimika kweli hapa jamvini!

Ni kweli hayaonekani ,wengi wametumia .."Huenda Pemba usifanyike Uchaguzi Mkuu " Ukiwauliza kwa nini wanasema ..yale madai yao kwa wanavyoyafanyia kazi yana sura nzuri. Na katika huo uzinduzi naona CCM - vigogo wa Zanzibar hawakuhudhuria ,pengine kwa vile Salim ni Mpemba na Seif ni mmoja katika walioshiriki katika kutunga kitabu nae pia ni Mpemba , halafu ukipima vipimo vya hali ya Pemba na wananchi wake katika serikali zote basi utaona wanazo sababu za kuyakoromea madai yao kwa kuwa vipimo hivyo vinaonyesha hawatendewi haki kama sehemu moja ya Tanzania au Zanzibar.
 
Watz tuache kumpenda mtu kwa sababu tu aliwahi kuwa katibu mkuu AU au kwa s ababu tu aliwahi kuwa afisa wa ngazi za juu wa UN bali tumpime kwa kile alichokifanyia nchi yetu!Likely akiulizwa hapa sasa hivi ndugu Masatu ni sababu gani "cardinal"anaweza kutupa kuhusu mchango wa Dr salim na uimarishaji wa znz kuwa kitu kimoja kudai haki zao toka mwaka 1963 hadi leo?Huwa mimi binafsi sipati lolote la maana alilofanya!
Dr Salim anazungumzia leo kuhusu kushikamana kwa waznz kudai haki zao ili hali kwa zaidi ya miaka 40 alipokuwa na nafasi nono za kimataifa na za ndani hakufanya hivyo!leo hii ujasiri huo kautoa wapi?iweje asubiri hadi CCM imtenge ndiyo acharuke?
Nasisitiza tena,tulia kwako nyumbani,tz itakombolewa na wengine wewe umeshindwa kufanya lolote la maana na sana sana anaona tu aibu!
Mungu iweke roho yake peponi simba wa vita vya ukweli kuhusu kuwa kitu pamoja wanzn hayati Othaman Haroub na kamwe Dr salm huwezi kuwa "role model'wa wanzn wa kizazi kipya kuhusu kuondoa tofauti zao za kikanda,ulishindwa kufanya hivyo mwaka 1984 ulipokuwa PM au miaka ya ya 90 ulipokuwa General sec wa OAU utaweza leo?

Mkuu,
Sema wewe hupati lolote alilofanya lakini sii wote kwa sababu huna kumbukumbu.na kibaya zaidi unataka kumhukumu mtu hoja zake ukiwa mtupu..
Ikiwa Zanzibar ilipigania Uhuru wake toka mwaka 1963 unajua Salim alikuwa wapi na akifanya nini!.. Unajua kwamba Salim ndiye alikuwa muasisi wa Zanzibar student Union na pia Secretary General wa chama cha waandishi Zanzibar wakati akiwa Chief editor..

Umezungumzia wakati akiwa na nafasi nono amewahi kufanya kipi! je, umesahau kwamba waakti wote akiwa PM, huyo Sharrif Hamad alikuwa Waziri kiongozi Zanzibar (1984 -1988). sijui huyu alileta mabadiliko gani kwani kazi unayodai haikuwa ya Salim peke yake.. Team kubwa ya Wazanzibar walishika madaraka ya juu kabisa ktk Uongozi wa serikali ya Jamhuri toka Makamu wa rais, PM, Waziri kiongozi huyo Seif Sharrif Hamad na kina Mwinyi akiwa Waziri wa mambo ya ndani.. Hawa walifanya nini?

Mkuu wakati Salim akiwa madarakani, ni wakati ambao Tanzania ilikuwa shwari kabisa hapakuwepo na migogoro kama ya leo hii pamoja na kwamba bara walitakiwa kubeba pass kuingia Visiwani.. hakuna aliyejali wala kufikiria utengano kwa vipimo kama mnavyotaka kutumia.Leo hii unaona CCM bara wameshika wizara zote kuendeleza libeneke la Ufisadi..I mean mkuu tazama wizara zetu leo hii wangapi wantoka Zanzibar na wameshika wizara gani?..

Mkuu ni lazima usome wakati na kuelewa kinatendeka kitu gani leo hii..Tanzania ya Nyerere pamoja na lawama zote zinazotolewa dhidi yake ilikuwa shwari kabisa kila upande uliridhika na mfumo wa uongozi..Ni pale tu tulipoanzisha vyama vingi ndipo tulipoharibu kila kitu, kwa sababu viongozi wengi wamejipanga kuchukua ruzuku na sii kutetea maslahi ya nchi.

Mtu kama Salim ni sumu ya mafisadi, hanunuliki na amechukiwa sana kila sehemu aloongoza kwa sababu hapendi mission town ktk ofisi zake. hapendi kuzembea na kupendelea ndugu ktk ajira...Hatoi wala hachukui rushwa kitu ambacho baada ya Azimio la Zanzibar kupitishwa alimwagwa.

Ni mtu ambaye kulingana na mazingira ya Kidanganyika naweza kusema ana roho mbaya! kwani sisi mtu anayejali sana maslahi ya Taifa ni mjinga, mchovu na atakufa maskini.He is the only person mimi ningempigia kura yangu bila hata kuuliza kama angepitia mwaka 2005 potelea mbali umri wake.
Hakika mtu yeyote anayetaka Wazanzibar waungane kwanza kuondoa tofauti zao ni mawazo makini sana kwa pande zote mbili... na siku Wazanzibar watakapo fanya hivyo, thubutu CCM kufanya tena walofanya Pemba mwaka 2000.. itakuwa kazi mpya..
 
Last edited:
Could be me.

Kama unashindwa hata kutumia jina lako unategemea kuna mbadala wowote unaoweza kuleta ukipewa urais. Moja ya utamaduni wa watawala tulio nao ni uoga wa kusimamia hoja za hadharani, sioni tofauti na wewe hapa...

Omarilyas
 
Kwanza nimesema "could be" which means maybe. Pili sijasema nataka huo uraisi. Kuwa na vigezo vya kitu fulani siyo kutaka kufanya hicho kitu. Niweke jina langu kwani naomba kura hapa JF? Kama nikija kugombea nitawapa jina langu.
 
Uweke jina lako kuonyesha kuwa unajiamini na unaweza kuwa mfano makini wa ulichoita NEW BREED na kuwa hao NEW BREED ni tofauti na hiyo OLD BREED tuliyonayo akiwemo Salim...

Na pia kama tutasubiri hao new breed kuanza kujitokeza hadharani pale tu watakapokuwa wakitaka kugombea basi ni wazi tutaendelea kuchagua viongozi waliojaa mapungufu na ambao hatuwajui vilivyo kiasi cha kuamini kuwakabidhi jukumu adhimu la kutuongoza...

Be the change u want to see....

omarilyas

Nishakuambia iwapo nitataka kugombea utajua jina langu. Nini tena wataka mkuu? Haya nikisema sasa hivi mimi Peter Luther utaridhika? Mkuu don't worry new breed wako wengi tu kama kweli you are interested kuwajua personally it doesn't take long to notice them. Kwani hauoni vijana wowote kwenye siasa mkuu? Au? When my time comes utanijua if I decide to. Hayo mengine it's a personal choice. Ila asante kwa ushauri.
 
Mkuu,
Sema wewe hupati lolote alilofanya lakini sii wote kwa sababu huna kumbukumbu.na kibaya zaidi unataka kumhukumu mtu hoja zake ukiwa mtupu..
Ikiwa Zanzibar ilipigania Uhuru wake toka mwaka 1963 unajua Salim alikuwa wapi na akifanya nini!.. Unajua kwamba Salim ndiye alikuwa muasisi wa Zanzibar student Union na pia Secretary General wa chama cha waandishi Zanzibar wakati akiwa Chief editor..

Umezungumzia wakati akiwa na nafasi nono amewahi kufanya kipi! je, umesahau kwamba waakti wote akiwa PM, huyo Sharrif Hamad alikuwa Waziri kiongozi Zanzibar (1984 -1988). sijui huyu alileta mabadiliko gani kwani kazi unayodai haikuwa ya Salim peke yake.. Team kubwa ya Wazanzibar walishika madaraka ya juu kabisa ktk Uongozi wa serikali ya Jamhuri toka Makamu wa rais, PM, Waziri kiongozi huyo Seif Sharrif Hamad na kina Mwinyi akiwa Waziri wa mambo ya ndani.. Hawa walifanya nini?

Mkuu wakati Salim akiwa madarakani, ni wakati ambao Tanzania ilikuwa shwari kabisa hapakuwepo na migogoro kama ya leo hii pamoja na kwamba bara walitakiwa kubeba pass kuingia Visiwani.. hakuna aliyejali wala kufikiria utengano kwa vipimo kama mnavyotaka kutumia.Leo hii unaona CCM bara wameshika wizara zote kuendeleza libeneke la Ufisadi..I mean mkuu tazama wizara zetu leo hii wangapi wantoka Zanzibar na wameshika wizara gani?..

Mkuu ni lazima usome wakati na kuelewa kinatendeka kitu gani leo hii..Tanzania ya Nyerere pamoja na lawama zote zinazotolewa dhidi yake ilikuwa shwari kabisa kila upande uliridhika na mfumo wa uongozi..Ni pale tu tulipoanzisha vyama vingi ndipo tulipoharibu kila kitu, kwa sababu viongozi wengi wamejipanga kuchukua ruzuku na sii kutetea maslahi ya nchi.

Mtu kama Salim ni sumu ya mafisadi, hanunuliki na amechukiwa sana kila sehemu aloongoza kwa sababu hapendi mission town ktk ofisi zake. hapendi kuzembea na kupendelea ndugu ktk ajira...Hatoi wala hachukui rushwa kitu ambacho baada ya Azimio la Zanzibar kupitishwa alimwagwa.

Ni mtu ambaye kulingana na mazingira ya Kidanganyika naweza kusema ana roho mbaya! kwani sisi mtu anayejali sana maslahi ya Taifa ni mjinga, mchovu na atakufa maskini.He is the only person mimi ningempigia kura yangu bila hata kuuliza kama angepitia mwaka 2005 potelea mbali umri wake.
Hakika mtu yeyote anayetaka Wazanzibar waungane kwanza kuondoa tofauti zao ni mawazo makini sana kwa pande zote mbili... na siku Wazanzibar watakapo fanya hivyo, thubutu CCM kufanya tena walofanya Pemba mwaka 2000.. itakuwa kazi mpya..

Mkandara

Napenda kuzungumzia mambo makubwa 3 kutokana na habari yako nzuri uliyoitoa hapo juu!na kikubwa zaidi ni mada yenyewe hasa kuhusu kuimarika kwa Muungano wa znz miongoni mwao!

Kwanza sio kweli kama ulivyosema hapo juu kuwa Dr Salim alipokuwa kwenye madaraka ZNZ haikujikita kwenye migogoro kama hii ya leo.Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa ZNZ ilijitumbukiza kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa tena wa chama kimoja kipindi ambacho Dr Salim alikuwepo madarakani kuzidi hata sasa ambapo ni mfumo wa vyama vingi!tuanze na vifo vya Mzee Khasim Hanga na Dr Othman nambaye hadi leo miili yao haijulikani ilipo na kifo cha Rais Karume pale Kisiwandui,Dr Salim alikuwepo madarakani na machafuko yake yalikuwa makubwa sana na dalili za kwanza kujitenga kwa wana znz kutokana na vifo hivyo.

Mambo makubwa zaidi 2 yaliyosabisha na kuwafanya wanzn watengane ni haya;
@Mapinduzi haramu ya kumtoa madarakani Rais wa 2 wa znz ambaye alichaguliwa kikatiba Mzee Jumbe mwaka 1984 kwa kila walichokiita akina Nyerere na wenzake"kuharibika kwa hali ya hewa znz".Mkandara kipindi hicho Dr Salim yupo tz na ana madaraka makubwa sana,Nyerere alitutangazia habari hii akiwa Dar na pembeni yake alikuwepo Dr Salim.

@Kufukuzwa kwa uanachama wan CCM 1988 wenye msimamo mkali hasa wenye asili ya Pemba kwa kile kilichojulikana kama"saficha CCM",kipindi hicho bado Dr Salim alikuwa na nguvu sana kwenye siasa za tz.

@Kubadilishwa katiba ya tz na kumfanya Rais wa znz awe kama mkuu wa mkoa kimuungano,kumbuka kuwa Rais na Makamu wake wakiwa nje ya tz PM anachukua madaraka,ili hali kachaguliwa na watu wa jimbo la Mpanda tu!jambo hili liliwagawa sana waznz hasa waliopo madarakani na wasio na kitu.Dr Salim hadi leo hajalikemea jambo hili linalowafanya waznz wapigane vijembe!

Serikali kuu ilizidisha utengano kwa wanzn ili hali waznz waliopo madarakani kama akina Mwinyi,Salim na wengineo wakiwa tu wametulia tuli.Tulishuhudia wana harakati waliojaribu kutetea U-znz wao bila kujali itikadi za kisiasa wakiishia kituo cha Polisi cha Madema na baadae gereza lenye balaa la Kiinua-Miguu!

Nahitimisha kuwa kutengana kwa wanzn sio suala la jana au leo,lina mizizi yake toka miaka mingi sana na hawa akina Dr Salim hawawezi kukwepa lawama hizi toka akiwa balozi wetu Misri,Waziri wa kigeni,Waziri wa Ulinzi,PM,nfasi kubwa kubwa za kimataifa na nyinginezo.Salim hakukemea wala kueleza hisia zake pale ambapo wanzn walipotengwa ndani ya katiba,pale mbapo kundi moja la wana znz lilipodhulumiwa haki zake wala pale ambapo kundi la mzee Jumbe lilipodhihakiwa adharani.

Ni nani waliopindisha uchaguzi wa CCM wa kumpata atakayerithi Urais wa ZNZ kutoka kwa mzee Mwinyi kati ya Abdul Wakil na Maalim Seif mwaka 84?Mzee Wakil alishinda kihalali?Wanzn si ndiyo walianza kujitenga hapo kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba hata machafuko ya mwaka 2000 yalikuwa ni hitimisho tu la kutengana kwa wanzn?
Baadhi ya wanzn wanaotoka upande mmoja wa nchi wanadhulumiwa haki zao waziwazi,wanafukuzwa kazi na kuvunjiwa makazi yao,na haya yanatendeka hawa akina Dr Salim wanayaona!Yaliyomkuta wakili Mbwelezeni,Yusufu Hariri aliyekuwa mwakilishi wa Konde, na watu wengine mashuhuri,kutengwa zaidi kwa Dr Ghalib hata aliposhinda kura za maoni mwaka 2000 kunafanya zaidi kuwa kitu kimoja kwa waznz kuwa kama wimbo tu!

Mkandara,msome vizuri mzee huyu na utakuja kukubaliana na mimi kuwa nae ni mmoja kati ya waliochangia kuwafanya waznz wajitenge!
 
all in all kila siku tukikaa na kuota jana hatutofika mahala.

yeyote yule awaye na kwa njia moja au nyengine ktk ushiriki wake juu ya hilo haliondoshi ukweli kuwa wazanzibari tunajirejesha nyuma wenyewe. kwanza tukubalini sote kuwa huko nyuma tulikosea tulisalitiana na kufanyiana mabaya au kutowajibika vyema katika nafasi tulizopewa.

tunasema ya leo sio ya jana au iliopita si ndwele tugange lijalo, wakati umefika kukaa chini kwa nia na dhamira moja ya kusafisha yaliopita na kujipanga kwa kuungana na kuangalia ni jinsi gani tutayasukuma mbele yale madai yetu kwa manufaa ya wazanzibari na watanzania kwa ujumla.

haya ya kun'gan'gania nani kafanya nn hayatusaidii na ndio maana akasema wazanzibari tunajirudisha nyuma wenyewe na yeye hapo kiungwana kakiri kuwa yumo na ndio maana hata hapo alikuwepo na seif sharif wa cuf na yeye wa ccm na akatamka watu waanze hapo
 
Back
Top Bottom