Wazanzibari Wenyewe Mnajirudisha Nyuma: DR. Salim

Mkandara said:
Matatizo ya ndani tu yanawashinda kuyaweka wazi na kuwalaumu vviongozi wahusika badala yake wanatumia UNAFIKI kutafuta mchawi toka bara na sii visiwani.

Mkandara,

..hicho ulichokiandika hapo juu ndicho kilichopaswa kuwa maudhui makuu ya hotuba ya Salim Salim. siyo kuanza kudai Wazanzibari waungane kudai haki zao kwetu, wakati wao ndiyo wanaofaidika zaidi na huu Muungano.
 
Mkandara,

..hicho ulichokiandika hapo juu ndicho kilichopaswa kuwa maudhui makuu ya hotuba ya Salim Salim. siyo kuanza kudai Wazanzibari waungane kudai haki zao kwetu, wakati wao ndiyo wanaofaidika zaidi na huu Muungano.
Mkuu ndio maana nikasema inabidi kwanza umwelewe Salim alikuwa akizungumza kitu gani..
Hakusema Wazanzibar waungane kwa mtazamo wako isipokuwa waungane wenyewe kuondoa tofauti zao kama vile yeye yuko CCM na Seif S. Hamad yuko CUF wanaweza kukaa wakazungumza vizuri na kuelewana, inabidi Wazanzibar wote wafuate mfano huo..
Hivyo, anachokipendekeza ni Muungano wao kuwa ni muhimu zaidi ya matatizo yaliyopo ktk muungano wa kitaifa, kwani bila wao kuungana wakakubaliana ktk masala ya msingi kuwalisha matakwa ya Wazanzibar ktk muungano mzima inakuwa vigumu kufikia muafaka...Sioni mapengufu ktk hoja hiyo..
 
si wamesema wanamafuta na hawataki ku share na bara

kinachotakiwa ni serikali moja
unguja mkoa na pemba mkoa
total population ya zanzibar ni sawa na mkoa wa kinondoni
lakini znz kuna raisi, mawaziri na viongozi kibao halafu kazi hamna...

lakini kama muungano huu wa znz wana rais halafu bara hawana haufai, wala serikali tatu no....
wakati umefika wa serikali moja au basi lakini haya mambo ya znz kila siku kusema sisi ndio tunawanyima maendeleo haiwezekani......

embu fikiria mwanza ni kubwa kuliko znz, ina watu wengi mara mbili ya znz, uchumi wake ni mkubwa kuliko znz lakini znz kuna wabung 50 na mwanza 13
halafu bado wanaonewa na bado kuna baraza la wawakilishi...


Matatizo ya muungano yataanza kutatuka siku ndugu zetu wa Danganyika watapoacha huu umbumbumbu wao katika muungano, wengi wao wameanza kuijua Zanzibar baada ya kufa Nyerere halafu leo wanajifanya kila kitu wanakijua wao kuhusu Zanzibar, wao ndio wataalamu wa kila tatizo la Zanzibar. Kumbukeni kuwa Zanzibar ilikuwa ni nchi kamili isiyokuwa na tofauti na nchi nyengine yoyote kabla ya huu muungano, na huu muungano ni baina ya Zanzibar na Tanganyika na sio Zanzibar na Mwanza hivyo hii hoja ya kuifananisha Zanzibar na Mwanza haina mbawa.

Kuhusu rais wa Tanganyika na serikali ya Tanganyika kamuulizeni Nyerere na wenzake kwanini hawakutaka iwe hivyo?, hakuna Mzanzibari hata mmoja aliyesema na anaesema hataki kuona serikali ya Tanganyika hivyo musiwatupie Wazanzibari hili, wachawi wa hili munao wenyewe.
Vile vile uamuzi wa viongozi wangapi wawepo Zanzibar ni wa Wazanzibari wenyewe kama ambavyo Tanganyika (population 40 million) ilipoamua kuwa na mikoa 25!!! na wakuu wa mikoa namba hiyo hiyo ambapo nchi kama Marekani ina watu zaidi ya millioni 300 na ina majimbo hamsini na kitu tu au hata Canada ina watu kama TZ lakini pamoja na utajiri wao wote wana majimbo 13 tu (ukihesabu territories zao pia), haya ni mambo ya ndani ya kiutawala yasiwatie watu joto, uendeshawaji wa ka nchi kao ka Zanzibar ni wao wenyewe sasa tatizo lipo wapi?.

Muungano ni makubaliano baina ya nchi mbili, sasa kama wewe ungelikuwa umeungana na mwenzako (mfano kwa biashara) na ukaona mwenzako anaenda kinyume na makubaliano yenu (hata kama sio kweli kuwa mwenzio anakuendea kinyume) ungelifanya nini? ungelikaa kimya tu ukamwacha afanye anavyotaka?, Wazanzibari na Watanzania kwa jumla wana kila haki ya kudai haki ya muungano ili kujua nini kimekubaliwa na ili tukianza kuuchambua muungano tujue tunaongea nini, hivi sasa watu wanajisemea tu kutokana na wanavyojua au walivyoambiwa wao, wakati umefika tuweke mambo wazi halafu kama tunaamua kuwa na serikali kipande, moja, mbili au hata tatu basi itakuwa angalau tunajua tunafanya nini na kwa makubaliano gani sio haya ya sasa - kizungumkuti kitupu.
 
Nkazahau,
Mkuu maelezo yako murwa kabisa isipokuwa tu nawe unapindisha sana kuingia ktk Muungano wakati wenye matatizo ni sisi.
Nikisoma malalamiko yako yote hayaelezi kile unachokitaka wala mapungufu ktk Muungano. Nchi ikiwa na serikali moja, mbili au tatu haiwezi kuleta matatizo ikiwa sisi wenyewe tumejipanga vizuri na kuna makubaliano ya kimsingi..

Kila nchi zilizoungana zina Uhuru wa majimbo yake na ilikuwa hiyari kwa nchi hizo kujiunga wala haikutokea kuwa kila raia wa nchi alikubaliana na muungano huo..Na zaidi ya hapo kila muungano wa nchi mbili au zaidi hauna sheria za kiutawala sawa sawa..
Mimi nakubali kabisa kwamba Zanzibar ni nchi ambayo ina rais wake..Bara inatakiwa kuheshimu hilo kwa sababu ni ktk makubaliano yetu tumekuwa na marais wawili..ndio mfumo tulikubali kuungana ktk kuendesha serikali zetu mbili.

Inasikitrisha tu pale Waziri mkuu anapoweka madai kwamba Zanzibar sio nchi wakati akijua fika kwamba hakuna nchi yoyote inayoweza kutambulika kama nchi ikiwa haina Mtawala iwe rais, waziri mkuu au Sultan..Zanzibar inaye rais wake hivyo ni nchi kamili iliyoungana na Bara kujenga Taifa la Watanzania..
lakini pamoja na yote haya ni pale mnaposhindwa kukaa pamoja nyie wenyewe mkakubaliana kuwakilisha hoja zenu kama Wazanzibar..Utaona kwamba Baraza la Mapinduzi haliwezi kabisa kukubaliana na CUF ama wawakilishi wengine nje ya utawala wa ASP.

Kwa hiyo kimsingi tatizo la Muungano linaanza na ASP ambako Salim hayupo na ndio maana akasema - Wazanzibari Wenyewe Mnajirudisha Nyuma:
Haya ni maneno mazito sana ambayo inatakiwa myafanyie kazi.. ondoeni kwanza tofauti zenu kisha mnaweza kusimama kama kitu kimoja sii habari za Iraq ambako Sunni na Shia (wakijiita Waislaam) wanapigana wenyewe kwa wenyewe huku wakimlaumu Marekani kuingia Iraq..Bila maelewano ya ndani ni vigumu sana kwa mtu kama mimi kuamini kwamba Marekani akiondoka Iraq kesho kutakuwa na usalama.. watauana kama mbwa mfano mzuri tunauona Somalia..
 
Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuwa United States of Tanzania, hivyo hatuhitaji Rais 2. Rais ni 1 tuu kama USA.
 
Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuwa United States of Tanzania, hivyo hatuhitaji Rais 2. Rais ni 1 tuu kama USA.

Na hapo Tanganyika na Zanzibar zilipoungana zilikubaliana kutakuwa na serikali ngapi? na marais wangapi?, ninavyoelewa mimi ni kuwa Zanzibar ilikubaliana kuwa na serikali yake na rais wake na kujiamulia mambo yake wenyewe ukiyatoa mambo yaliyoingizwa kwenye muungano na wala haikutaka serikali ya Tanganyika ivunjwe na kamwe haikutaka serikali moja - haya ndio makubaliano ninayoyaelewa mimi sasa pengine kuna makubaliano mengine ambayo wananchi hatuyaelewi na hapa hili suala la mkataba wa muungano linakuja tena - wakuu hebu uwekeni wazi huu mkataba kwani kuna tatizo gani wandugu?, muungano ni wa watanzania wote sio wa viongozi wa juu wa CCM tu, kila raia wa nchi hii ana haki ya kujionea mwenyewe nini kilikubaliwa na kutiwa saini kwa niaba yake, ikiwa tunaiona katiba ya nchi kwa nini hatuonyeshwi mkataba wa muungano?, kuna usiri gani ndani ya huu mkataba?, au kweli haupo?.

USA walikubaliana kuwa na rais mmoja na sisi tulikubaliana tuwe na marais wawili sasa tatizo lipo wapi?. Mara ya mwisho nilipoangalia nchi yetu ilikuwa ikiitwa United Republic of Tanzania na sio United States of Tanzania - jee na jina nalo limeishabadilishwa bila hata ya kuambiwa wananchi? :)
 
Masatu,

..Wazanzibari wanadai wananyimwa haki lakini hawaishi kungangania huku Tanganyika.

..kama kweli Tanganyika na wa-Tanganyika wangekuwa wabaya kiasi hicho, na wanawanyima haki basi, wangeisha ondoka kurudi kwao.

..tena wanadai "Wazanzibari tuungane kudai haki zetu" sasa nini kinakufanya wewe uamini kwamba wao na sisi tu wamoja?

..unadai tuweke UTAIFA mbele, sasa of all the ppl Salim Salim kwenda kutoa kauli ile "Wazanzibari tuungane kudai haki zetu" hivi unaona ameweka utaifa mbele? au tunaotakiwa kuweka utaifa mbele na wa-Tanganyika tu?

..binafsi sioni ambacho Mtanganyika anaweza kukipata huko Zanzibar ambacho hawezi kukipata hapa Tanganyika. Mtanganyika hana maslahi yoyote yale na muungano huu.

..ni kweli kwamba wakubwa wa Ulaya wanasisitiza sana masuala ya muungano. lakini tukumbuke kwamba wana sababu zao.

..kabla ya Watanganyika kurukia tu mawazo ya wakubwa, tunapaswa kuchunguza faida wanazozipata wakubwa hao kwa kuungana.

..WATANGANYIKA TUNAPATA FAIDA GANI KWA KUUNGANA NA NCHI YENYE WATU WACHACHE, ENEO DOGO, NA RASILIMALI KIDUCHU, KAMA ZANZIBAR?

Jasusi,

..watu kama Masatu huwa nawapa "thank you" hata wakinitukana!!

..and I never reply in kind kwa matusi yao.


Jokakuu,

Ni kweli wazanzibar wanadai wananyimwa haki na bado wamo kwenye muungano hata hivyo na sisi wabara pia tunadai kunyimwa haki lakini pia tumo kwenye muungano! jaribu kuwa open minded sio mbali hapo kuliona hilo.

Hilo la kudai kuungana kudai haki yao Mkandara kalielezea vizuri sana. Inavyoelekea hujamulewa Dr Salim kuungana hapa ni kwa kuondoa tofauti zao za U CUF na U CCM ili wawe na kauli moja na hili wala sio jipya wa Scotish kila siku wanalalamikia muungano wao na England mpka wengine kufikia kutaka kuuvunja.

Hakuna ubaya kwa wazanzibar kujizungumzia kama wazanzibar hata wewe hapo unazungumza kama m-bara na kulinda maslahi ya u-bara na ndio maana unakuja na hoja legevu eti hakuna tunachonufaika kwa kuungana na Zanzibar nchi ndogo na yenye rasilimali kiduchu, halafu mkiambiwa mnatoa hoja za kijinga mnakuwa mbongo.

Hakuna mahala ulipotukanwa acha kulia lia if anything nimekusaidia kukupa mwangaza kutoka kwenye giza totoro!
 
Nkazahau,
Mkuu maelezo yako murwa kabisa isipokuwa tu nawe unapindisha sana kuingia ktk Muungano wakati wenye matatizo ni sisi.
Nikisoma malalamiko yako yote hayaelezi kile unachokitaka wala mapungufu ktk Muungano. Nchi ikiwa na serikali moja, mbili au tatu haiwezi kuleta matatizo ikiwa sisi wenyewe tumejipanga vizuri na kuna makubaliano ya kimsingi..


Mkuu mimi ni "back bencher" kwenye mijadala ya JF na napenda kupata maoni ya wenzangu na nini wanakifikiria kwenye masuala mbali mbali yanayotukabili. Sasa wakati mwengine nashindwa kujizuia kujibu hoja zisizo na macho ndio maana sio rahisi kuona nini ninakitaka kwani huwa najibu hoja tu na kujaribu kutikisha fikra za wenzangu ili tupate kuelewa haya mambo kwa kina.

Kuhusu ninachokitaka mimi kwa sasa ni serikali tatu au mbili, hizi mbili moja ya Tanganyika na nyengine ya Zanzibar halafu tunaangalia maarifa ya kwenda kwenye East African Union :), maana hapa East Africa sisi ndio wenye uzoefu wa muungano na tutasaidia sana katika kuimarisha muungano wa EAU. Na kama tumenufaika na muungano wetu basi inabidi tuwagawie ndugu zetu (wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi) hii neema tusiwe wachoyo.

Matatizo ya mgawanyiko wa wazanzibari ni ya kihistoria na sio rahisi kwa kiongozi mmoja au wawili kusimama jukwaani kulikemea hili halafu tukategema "miracle", kunatakikana mikakati mizuri na kila upande unaohusika au kila raia aelewe athari ya haya yanayoendelea sasa na kuwa tayari kuweka pembeni tofauti zetu, ni hapo tu ndipo tutakapokuwa na umoja wa kweli, matokeo ya hivi karibuni ni mwanzo mzuri lakini "we have a long way to go".

Kuhusu mapungufu ya muungano nadhani kama unafuatilia threads za JF basi ni mengi tu na ndio maana mimi kama raia naona kabla ya kuwa na informed opinion nilikuwa na hamu kubwa ya kuyajua makubaliano na hasa kuiona hii hati ya makubaliano, nishachoka kuwasikiliza baba, babu wajomba na shangazi etc wakifanya opinions zao kuwa ni facts.
 
kwa kweli salim amezungumza wazi na ujumbe umefika sasa kilichobaki wahusika kuufahamu huo ujumbe na kuamua kuufanyia kazi au kuuacha

matatizo kwenye muungano yapo, na kiudhati wazanzibar walio wengi wanapenda muungano uendelee ila wanachotaka ni kuona zile kasoro zilizokuwepo zitatuliwe.

hili ni la muda mrefu na limeainishwa vizuri kwa nyakati tofauti na wasomi na watu tofauti

tokea tume ya nyalali, jaji kisanga na wengine

matatzio ya kina jumbe, seif sharif, salmin amour na wengineo hadi juzi kuhusu mafuta na zanzibar nchi au si nchi

ila kinachoonekana kuwa wazanzibar wao kama wao hawajajipanga kueleza ajenda zao na kuziwakilisha kwenye muungano vizuri

utaona sio ccm wala cuf waliosimama kwa umoja kuaddress matatizo yao

juzi juzi mawaziri wa smz walikuwa wakipingana na waziri wa muungano ambae ni mzanzibari mohammed seif khatib

muungano ni wetu na ss tunayo nafasi yuko makamo wa rais waziri wa muungano na waziri kiongozi ambao ni wajumbe wa kamati inayojadili na kutafuta suluhisho la kero za muungano, sasa hawa wote ni wazanzibar isipokuwa pinda kwa nn wasiwe na sauti moja ya kumwambia pinda kuwa njia nzuri ni hii moja mbili tatu hakafu tuangalie nn kitafuatia.

kilichopo kila mtu hutaka aonekane peke yake ni shujaa huu ni upuuzi na kesho wakiondoka hapo watueleze tulivyoonewa

umoja kwetu ni jambo pekee litalosaidia kuleta muungano ulio bora na baada ya hapo tushirikiane na ndugu zetu wa tanganyika kuleta mapinduzi ya kiuchumi ktk taifa letu la tanzania


nnaaamini maendeleo yaje kwanza kuwepo na haki na kuaminiana naamini pia tukiweka sawa mambo ya muungano na kutumia akili na busara zetu kwenye uchumi tutasonga mbele.

siasa ziwekwe pembeni na tuangalie mambo muhimu ya taifa letu
 
Ukweli utabakia pale pale kuwa Hawa ndugu zetu wengi wao hawajaenda shule ya ki magharibi.

Uwezo wa kutoka nje ya box inakuwa ndogo.

Hilo ndo tatizo. Mimi huwa nawafananisha na wa Pelestina!

Ngoja nikimbie kabla ya mawe kurushwa humu!
 
Nasitiza tena Dr Salim Ahmed Salim,leave us alone,we do not need you any more!leo hii ndiyo anaisema chuki Waznz baina yao?alikuwa wapi miaka yote ambapo yeye akiwa waziri mkuu na baadae waziri wa ulinzi akiwa mjumbe mwenye nguvu sana ndani ya NEC ya CCM aliyehudhuria vikao na wenzake kuwetenga baadhi ya waznz ndani ya serikali ya Nyerere na mzee Mwinyi!
Alifanya nini alipokuwa na vyeo vya ndani na vya kimataifa kuwawezesha waznz wenzake wasizidi kujitemga na kutengwa?leo hii kawekwa kando na siasa za kiimla za tz ndiyo anayaona haya?
Amuulize mzee Machano,Mbwelezeni,Duni,Maalim na wenzake ambao wamerudishwa nyuma sana na serikali kuu ikiwemo kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.kwa ufupi hata yeye Salim alishiriki kuweka tabaka la utengano kati ya waznz wenyewe!
Why sasa anaanza kuzisema kuhusu kutengena kwa waznz akiwa nje ya dimba,na alipokuwa ndani ya duara kama tu wenzake na yeye alishiriki kuwatenga waznz hasa wenye muonekano tofauti na yeye kimawazo!
Dr salim hukuwepo kwenye vikao vya CCM vilivyofanyika Karimjee hadi usiku wa manane na kuwavua madaraka akina Maalim kwa kisingizio cha "kuchafuka hali ya siasa znz?",Je sio hapo ambapo hasa wanzn walianza kujitenga kutokana na ukanda kwa kiwango cha kutisha?ulifanya nini?Mauaji ya wanachama wa CUF mwaka 2001 ulichukua hatua gani kuyasemea?Pumzika tu salama Dr wetu Salim Ahmed Salim
 
Ukweli utabakia pale pale kuwa Hawa ndugu zetu wengi wao hawajaenda shule ya ki magharibi.

Uwezo wa kutoka nje ya box inakuwa ndogo.

Hilo ndo tatizo. Mimi huwa nawafananisha na wa Pelestina!

Ngoja nikimbie kabla ya mawe kurushwa humu!

Mkuu,

Pitia tena archives zako. Zanzibar imekuwa ni chimbuko wa wasomi mahiri na literacy level ya zanzibar ni kubwa kuliko bara.

Mtu kama unamkanyaga akisema unanikanyaga toa mguu wako imekuwa ndio uwezo mdogo wa kutoka nje ya box?

Matatizo ya wapalestina sio "elimu ya magharibi" wala uwezo mdogo wa kufikiri nje ya box. Hilo ni somo zito for your pea brain to grab!
 
Nasitiza tena Dr Salim Ahmed Salim,leave us alone,we do not need you any more!leo hii ndiyo anaisema chuki Waznz baina yao?alikuwa wapi miaka yote ambapo yeye akiwa waziri mkuu na baadae waziri wa ulinzi akiwa mjumbe mwenye nguvu sana ndani ya NEC ya CCM aliyehudhuria vikao na wenzake kuwetenga baadhi ya waznz ndani ya serikali ya Nyerere na mzee Mwinyi!
Alifanya nini alipokuwa na vyeo vya ndani na vya kimataifa kuwawezesha waznz wenzake wasizidi kujitemga na kutengwa?leo hii kawekwa kando na siasa za kiimla za tz ndiyo anayaona haya?
Amuulize mzee Machano,Mbwelezeni,Duni,Maalim na wenzake ambao wamerudishwa nyuma sana na serikali kuu ikiwemo kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.kwa ufupi hata yeye Salim alishiriki kuweka tabaka la utengano kati ya waznz wenyewe!
Why sasa anaanza kuzisema kuhusu kutengena kwa waznz akiwa nje ya dimba,na alipokuwa ndani ya duara kama tu wenzake na yeye alishiriki kuwatenga waznz hasa wenye muonekano tofauti na yeye kimawazo!
Dr salim hukuwepo kwenye vikao vya CCM vilivyofanyika Karimjee hadi usiku wa manane na kuwavua madaraka akina Maalim kwa kisingizio cha "kuchafuka hali ya siasa znz?",Je sio hapo ambapo hasa wanzn walianza kujitenga kutokana na ukanda kwa kiwango cha kutisha?ulifanya nini?Mauaji ya wanachama wa CUF mwaka 2001 ulichukua hatua gani kuyasemea?Pumzika tu salama Dr wetu Salim Ahmed Salim

Jizungu mzie wewe kama wewe haya mambo ya kuwasemea watu authority hiyo kakupa nani? Kama wewe humtaki wapo watakaokuwa wanamtaka nikiwemo mimi.
 
Masatu;

hao unaowasema weye hawapo Zanzibar au Pemba.

Ni sawa na kusema Tanzania tuna ma dakitari wengi halafu 60% yao wapo Botswana ...
 
Watz tuache kumpenda mtu kwa sababu tu aliwahi kuwa katibu mkuu AU au kwa s ababu tu aliwahi kuwa afisa wa ngazi za juu wa UN bali tumpime kwa kile alichokifanyia nchi yetu!Likely akiulizwa hapa sasa hivi ndugu Masatu ni sababu gani "cardinal"anaweza kutupa kuhusu mchango wa Dr salim na uimarishaji wa znz kuwa kitu kimoja kudai haki zao toka mwaka 1963 hadi leo?Huwa mimi binafsi sipati lolote la maana alilofanya!
Dr Salim anazungumzia leo kuhusu kushikamana kwa waznz kudai haki zao ili hali kwa zaidi ya miaka 40 alipokuwa na nafasi nono za kimataifa na za ndani hakufanya hivyo!leo hii ujasiri huo kautoa wapi?iweje asubiri hadi CCM imtenge ndiyo acharuke?
Nasisitiza tena,tulia kwako nyumbani,tz itakombolewa na wengine wewe umeshindwa kufanya lolote la maana na sana sana anaona tu aibu!
Mungu iweke roho yake peponi simba wa vita vya ukweli kuhusu kuwa kitu pamoja wanzn hayati Othaman Haroub na kamwe Dr salm huwezi kuwa "role model'wa wanzn wa kizazi kipya kuhusu kuondoa tofauti zao za kikanda,ulishindwa kufanya hivyo mwaka 1984 ulipokuwa PM au miaka ya ya 90 ulipokuwa General sec wa OAU utaweza leo?
 
Salimu anaonyesha ukomavu wake kisiasa na nafikiri angetufaa sana kama angepewa nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania, labda angeweza kukemea ufisadi kuliko serikali tuliyo nayo sasa ambayo inakumbatia sana ufisadi au niseme ni sehemu ya ufisadi. Ni kweli tatizo la Wazanzibar ni kuwa na umoja na kuwa na sauti moja lakini tatizo lao ni kwamba kila mtu anashika lake halafu at the end of the day wanalaumu wanaburuzwa na Tanganyika (sikukosea kutoandika Tanzania).

Tiba

Mkuu unatakiwa ukumbuke kuwa kuna wengi walipenda Salim ahcukue hatamu za Uongozi wa nchi, lakini kuna mtu mmoja aliandikja makala ya kumchafua sana kwa sababu hakuwa mtandao. Na Tanzania ya sasa uongozi hautokani na uwezo wa mtu, hilo labda ni la tatu au la nne, Kama wewe ni mtanzania halisi basi utakuwa unajua.
 
Back
Top Bottom