Wazanzibari wataka ajira kwa Watanganyika huko Visiwani ikomeshwe; wagonga mwamba!

Mimi hata wakanipa kazi huko siendi, Wala it doesn't matter at all, hawa Jamaa hata Ukioa watafanya fitna! Huu muungano sasa jamani hebu na uishe, kwani kuna Faida gani, kila mzanzibari kiongozi, na Kama wange kuwa waungwana hata Hilo baraza wange save hela, maana wana wabunge, they could have done the same!


RIP muungano
 
Jambo la msingi kwa watanganyika ni kutambua wazanzibari hawatupendi,lolote lililopo sasa ni kulazimishwa na uwoga,mahusiano mazuri kati ya pande hizi mbili ni mzuri tu kwenye makaratasi kama sheria na makubaliano mbalimbali,lakini rohoni nsä wazanzibari wengi kumejaa chuki dhidi ya watanganyika.

Nampenda Jussa kwa kutokuwa mnafiki na kuthubutu kuonyesha chuki yake binafsi na wale anaowawakilisha,kuwa watanganyika hatuwataki na hatuwapendi. Kwa kuwa mkweli hongera Jussa kwani unatupatia watanganyika angalizo mapema. Jussa alisema sababu mojawapo ya CUF kushindwa uchaguzi mdogo jimbo la Uzini ni kuwa na watu wa bara na wakristo wengi. Leo kama mwakilishi anawasilisha hoja ya kuwatenga wa bara katika ajira katika sekta ya utalii.

Tusihoji ni wazanzibari wangapi tunafanya kazi bara katika sekta ya utalii na sekta nyinginezo,tujiweke tayari tumekataliwa na hili liko rohoni mwao na limejaa akilini mwao. Eritrea na Ethiopia zilikuwa nchi moja,Sudani na Sudani kusini zilikuwa pia nchi moja,kutokana na utofauti mkubwa wa maslahi walitengana,ili kila upande ulinde maslahi ya wananchi wake. Sioni tabu yoyote tukijitenga nao,na sioni sababu ya kuwangangania kama hawatuhitaji na wanaliweka wazi!

It is an alarm, lets respond accordingly and we have no reason to hastate to depart,break-up the acceptable union. Tanganyika will expand its export and foreign income by doing it. Every one of know how ships dock in Unguja and Pemba with life necessities originating from mainland,all food stuff they are depending for life,is we who provide. Don't mention the electricity supply,all that count in exports!

Lets go back to the drawing table and re-draft the matter. In the forth coming Tanzania constitution review,lets make no mistakes!
 
mimi sioni kosa kama zanzibar wanataka kuwatafutia vijana wao ajira wakati tunajua kuna watu wengi sana kutoka kenya, msumbiji na nchi nyenginezo majirani wanaandikwa kazi mahotelini. First priority, iwe vijana wa zanzibar. Ukiwa zanzibar, utashangaa kuna wafanya kazi za hoteli kutoka south america , kutoka italy wakati vijana wetu wapo na hawana kibarua. Tatizo la ajira lipo na viongozi wetu wamo katika kutafuta ufumbuzi.
 
KUSHINDA KWA KURA MOJA NI DALILI KUWA TUSHATENGANA. Ni vizuri muungano TUUVUNJE, ni mbaya sana kuungana na mtu anayekulalamikia kila kukicha kwamba wewe ndiyo sababu ya matatizo yake.
 
mimi sioni kosa kama zanzibar wanataka kuwatafutia vijana wao ajira wakati tunajua kuna watu wengi sana kutoka kenya, msumbiji na nchi nyenginezo majirani wanaandikwa kazi mahotelini. First priority, iwe vijana wa zanzibar. Ukiwa zanzibar, utashangaa kuna wafanya kazi za hoteli kutoka south america , kutoka italy wakati vijana wetu wapo na hawana kibarua. Tatizo la ajira lipo na viongozi wetu wamo katika kutafuta ufumbuzi.
Mkuu, hapa wanaolalamikiwa siyo wafanyakazi toka Kenya, Msumbiji nk, bali ni wafanyakazi wanaotoka Tanganyika. Hata kura iliyopigwa ilikuwa na kuruhusu au kutoruhusu ajira za wabara katika sekta ya utalii.
 
Hivi huyo Jusa huwa anakuja kufanya nini bara?Akija kwanini huwa wanamwacha?daamn!

Mtu kama huyu si wa kuchekewa hata siku moja, unless tuwe tunataa kuuvunja muungano, kuendeleza siasa hatari kama hizi ambazo zinaweza kupelekea vurugu za kidini na mauwaji, na huku kumwachia mtu huyu aendelee kufanya haya ni sawa na kujimwagia wese na kujipiga kibiriti!
 
7th April 2012

Ladhu%2810%29.jpg

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismael Jussa Ladhu (CUF)

Wajumbe Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), jana wamelazimika kupiga kura ya kuamua watu wa Tanzania Bara waendelee kuajiriwa katika sekta ya utalii Zanzibar au wapigwe marufuku ili kuongeza ajira kwa Wazanzibari.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismael Jussa Ladhu (CUF), kuzuia kifungu cha kuweka utaratibu wa ajira katika sekta ya utalii wakati Baraza lilipokaa kama kamati kupitisha vifungu vya muswada wa kurekebisha Sheria ya Utalii namba 6 ya mwaka 2009.

Jussa alisema kwamba kifungu cha 23 (3) cha sheria kinachosema ajira katika sekta ya utalii lazima awe Mtanzania neno Mtanzania lifutwe na kuweka lazima awe Mzanzibari kwa malengo ya kulinda na kuongeza ajira kwa Wazanzibari.

Kifungu kinasema "mtu yeyote anayefanya biashara ya utalii aliyeajiri mtu ambaye sio Mtanzania kutoa huduma, lazima apate ruhusa ya maandishi kutoka kwa waziri baada ya kumthibitishia Waziri kuwa hakuna mtu wa ndani wa kujaza nafasi hiyo." Umesema muswada huo.

Jussa alisema kwamba sheria hiyo kuruhusu watu kutoka Tanzania bara kunufaika na ajira bila ya kuwepo udhibiti kunachagia sekta hiyo kunufaisha wageni wakati wazanzibari wengi hawana kazi Zanzibar. Alisema kwa kuwa Zanzibar ni nchi ndogo lazima iwe na utaratibu wa kulinda ajira kwa maslahi ya wananchi wake.

Hata hivyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Abdillah Jihad Hassan, alisema kwamba haiwezekani Watanzania bara kuzuiwa kunufaika na ajira Zanzibar kwa vile kitendo hicho kitakuwa kinakwenda kinyume na sheria za kazi za kimataifa.

Alisema kwamba Tanzania na Zanzibar zimeridhia mkataba wa sheria za kazi za kimataifa na haiwezekani kutunga sheria zinazokwenda kinyume na sheria hiyo hasa kwa kuzingatia Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Jihadi alisema kwamba iwapo serikali itakaribisha wazo hilo sheria hiyo italeta mgongano mkubwa katika utekelezaji wake na kutaka watanzania bara waendelee kunufaika na ajira kupitia sekta ya utalii Zanzibar.

Msimamo wa Jihadi uliungwa mkono na Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar, Abubakari Khamis Bakari, ambaye alisema kufanya hivyo kutaibua mgogoro wa kuwepo sheria mbili zinazogongana katika utekelezaji wake.

Hata hivyo, alisema kwamba jambo la msingi ni kuwepo na kanuni ambazo zitasaidia mzanzibari kupewa kipaumbele katika utaratibu wa ajira kupitia sekta ya utalii Tanzania Zanzibar.

Kutokana na Jussa na wajumbe wengine wa CCM kuendelea kutetea Wabara kufutwa katika ajira Zanzibar, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, alisimama na kusema kwamba haiwezekani kuweka sheria ya kuwanyima ajira Watanzania bara wakati kuna Wazanzibari pia wananufaika na soko la ajira la Tanzania bara.

Alisema kwamba kufanya hivyo kuna weza kuibua matatizo makubwa katika sura ya muungano iwapo serikali ya muungano itaaamua kudhibiti Wazanzibari kuajiriwa katika soko la ajira la Tanzania bara.

Othman alisema kwamba wakati huu Tanzania inaelekea katika soko la pamoja la Jumiya ya Afrika Mashariki sio muafaka kuwa na sheria inayoweka mipaka ya ajira katika eneo moja la muungano wa Tanzania.

Kutokana na mvutano huo Mwenyekiti wa Baraza, Mgeni Hassan Juma, aliamua wajumbe kupiga kura wanaotaka Watanzania bara waendelee kunufaika na ajira Zanzibar na wale wanaopinga wabara kuajiriwa Zanzibar kwa kupiga kura ya Ndiyo na Hapana.

Hata hivyo, matokeo ya kwanza mshindi alikosekana baada ya matokeo kufungana kwa kura 20 dhidi ya 20 na kulazimika kura hiyo kurudiwa kwa mara ya pili na serikali kuibuka mshindi katika kura hiyo.

Kabla ya kura hiyo kurudiwa wajumbe saba waliongezeka na kufanya idadi ya wajumbe 47 lakini baada ya kupiga kura wanaotaka wabara waendelee kunufaika na ajira waliibuka washindi wakiongozwa na Baraza la Mawaziri Zanzibar.

CHANZO: NIPASHE

Kwa kweli tunapoelekwa siko kabisa, Hili suala la ubaguzi linalofanywa na wanzanzibari limezidi kushamiri sasa, tunalipatiaje ufumbuzi?

 
huyu ismMail jussa ni mbaguzi sana....hizo ajira chache za mahoteli zinamtoa roho.....hataki waajiriwe wabara ila wakenya hamna neno....
sasa waanze wao sisi yunamaliZa
 
Inasikitisha kuona mtu aliyemwakilishi wa Baraza la Wawakilishi akiwabagua wenzake huku akiamini bado kuna muungano.Ni dalili mbaya ya mtafaruku katika muungano
 
Kuna kosa moja la kiufundi linafanywa na wazanzibari wehu aina ya Jussa ambao kadiri siku zinavyosogea wehu wa aina hiyo kwa zanzibar wanaongezeka.
Wazanzibar wanatakiwa kuwapinga watanganyika kwa hoja zingine thabit zisizo na uhusiano na udini.
Kuupinga ukristo zama hizi ni kupoteza muda na kujihangaisha tu.
Ukristo ndio unaoendesha ulimwengu.
Wakristo ndio wanaoitawala dunia. Mfumo huo haupo Tanzania tu. Waislam mkubali mlichelewa kujipanga na sasa ni wakati wenu wa kujipanga upya bila ya kuwa na chuki. Vinginevyo tegemeeni vikwazo katika kila plan mtakayoipanga. Pole sana Jussa ukristo umeinfluence mapendekezo ya ubaguzi wako uwekwe kapuni
 
Na watanganyika tukilinda ajira zetu kwa wazawa tu wa Tanganyika, hawa wazanzibar waliojazana kwenye ajira huku Tanganyika watakwenda wapi? Au labda mnadumisha falsafa ya "Chako chetu, Changu changu"? Fikirieni kwa makini kabla ya kuwa na hayo mawazo mabaya yanayoweza kuwaathiri wazanzibar wengi kuliko hata watanganyika.


Asante....Umenena hasa...
 
mimi sioni kosa kama zanzibar wanataka kuwatafutia vijana wao ajira wakati tunajua kuna watu wengi sana kutoka kenya, msumbiji na nchi nyenginezo majirani wanaandikwa kazi mahotelini. First priority, iwe vijana wa zanzibar. Ukiwa zanzibar, utashangaa kuna wafanya kazi za hoteli kutoka south america , kutoka italy wakati vijana wetu wapo na hawana kibarua. Tatizo la ajira lipo na viongozi wetu wamo katika kutafuta ufumbuzi.
utamuajiri vipi mzanzibari kwenye hoteli ya kitalii wakati hata kizungu chake cha kuombea maji ya kunywa ni mgogoro tu...changamoto waliyonayo itakayowafanya vijana wengi waingie kwenye ajira wanaijua lakini kwa sababu ya chuki zao ndiyo wanataka kuwabania wabara...!
 
Tatizo wa Tanganyika tuna wema wa mshumaa,huu muungano hautusaidii kitu zaidi ya kutunyonya, kwa nini chao kiwe chao halafu cha kwetu kiwe chao?
This is foolishness mwageni hiyo robo tumwage hii kilo,tuone nani ataumia.
 
right friend,but once yu decide to fjght with your enemies yu should make sure yu won't show them your weapons,lijussa shown to us his axe this meaning he is ready to fight but we mailanders always we hide our differences we always stand up & singing Ta'nza'nia nakupenda. Do yu know why we singing like this b'coz father of nation j.k.nyerere&karume mixed the soil of both sides to show that we have the same race,culture&historical background,lijussa refers 1964 united republic laws(Tanzania).Mungu ibariki Tan'zan'ia ,Mungu ibariki Africa
 
mimi sioni kosa kama zanzibar wanataka kuwatafutia vijana wao ajira wakati tunajua kuna watu wengi sana kutoka kenya, msumbiji na nchi nyenginezo majirani wanaandikwa kazi mahotelini. First priority, iwe vijana wa zanzibar. Ukiwa zanzibar, utashangaa kuna wafanya kazi za hoteli kutoka south america , kutoka italy wakati vijana wetu wapo na hawana kibarua. Tatizo la ajira lipo na viongozi wetu wamo katika kutafuta ufumbuzi.
Mkuu, naomba urejee post hii.

Tatizo la ajira lipo kila pahali ulimwenguni kwa sasa. lakini kumbuka kuwa huu ni ulimwengu wa ushaindani. Nchi yoyote inaweza kufanya hilo la kuajiri wananchi wake kwanza katika sekta ya umma, lakini katika sekta binafsi ni kama msituni - mwenye nguvu ndiye anayeishi. Ni kweli kuwa ZNZ wapo waajiriwa kutoka Kenya, Msumbiji, Afrika ya Kusini na kwengineko, lakini hawakuajiriwa kwa sababu wametoka huko, bali kwa sababu ya elimu yao.

Watanzania (hasa Wazanzibari kwa hili), tuache kulalamika. tusome,tujitayarishe ili tumudu ushindani. Tuache kulalamika tu Watanzania Bara eeeh, Wakenya eeeh, Wazungu eeeh...Watu wanasoma na kusonga mbele wakati sisi tunakamata ngao ya uzalendo, tunasubiri mjomba, vijana wetu wanachakachua hata mitihani.
 
Back
Top Bottom