Wazanzibari wataka ajira kwa Watanganyika huko Visiwani ikomeshwe; wagonga mwamba!

mungu saidia huu muungano uvunjike
Nadhani kuna haja ya kuchukua kile chungu chenye udongo uliochanganywa na Nyerere na Karume siku ya muungano kirushwe katikati ya bahari kama ishara ya kuuvunja huo muungano ila kila nchi ijue lake.
 
Na watanganyika tukilinda ajira zetu kwa wazawa tu wa Tanganyika, hawa wazanzibar waliojazana kwenye ajira huku Tanganyika watakwenda wapi? Au labda mnadumisha falsafa ya "Chako chetu, Changu changu"? Fikirieni kwa makini kabla ya kuwa na hayo mawazo mabaya yanayoweza kuwaathiri wazanzibar wengi kuliko hata watanganyika.

ukumbuke kuwa Zanzibar ni nchi ndogo sana na hakuna ajira nyingi kama huku kwetu Tanganyika...kwa hiyo ni haki yao kulinda kazi zao kwa ajili ya vijana wao
 
Hivi huyu Jussa ziko timamu kweli? Hafikirii kuwa huku bara ndugu zake wazanzibari wamejaa tele na hawabaguliwi? Kama ni damu ya ubaguzi mwenzetu amejaaliwa (kama mtu aweza jaliwa kitu kibaya)!
 
ukumbuke kuwa Zanzibar ni nchi ndogo sana na hakuna ajira nyingi kama huku kwetu Tanganyika...kwa hiyo ni haki yao kulinda kazi zao kwa ajili ya vijana wao

Aliyekuambia Tanganyika kuna ajira nyingi nani? Wewe ni walewale tu wazanzibari mnataka kupewe kila kitu toka Tanganyika lakini mnataka kubana chochote kile toka Zanzibar mtanganyika asiguse!
 
Siku muungano unavunjwa nitafanya sherehe kubwa sana. Huu upumbavu wa kujibembeleza kwa wazanzibari unaletwa na CCM kwa kuwa imegundua huku bara haina chake. Watu wenyewe ni wavivu kutwa kucha wanashinda vibarazani halafu tunataka kuendelea kuwa nao katika muungano, na uwaziri wa bara tunawapa. Mimi mtu wa kijijini huo muungano wenyewe nausikia tu. We watu hata bia hawanywi unaungana nao kufanya nini?
 
We know Zanzibar is small island with small population too which could be accommodated in mainland without problem but what I see is some Zanzibaris want us to take harsh measures toward their unthinkable and discriminatory actions. So to solve let's decide in new constitution to declare Tanzania as one federal government state.
All these insinuations and provocative actions will end.
 
...Mchango wangu ni kuwa ZANZIBAR ni nchi yenye mamlaka kamili (rais,bunge(BW),mawaziri n.k), wana haki kulinda ajira kwa wazawa (Wazanzibar) tu.
Unaweza kujiita kuwa una mamlaka kamili, lakini wengine wasikutambue kama wewe una mamlaka kamili. Ukweli ni kwamba Zanzibar sio nchi ndio maana hata AU na UN hawaitambui kabisa, kama unabisha jiulize kwa nini Shein haudhurii vikao vya AU na UN. Waziri Mkuu wa NCHI alishasema kuwa Zanzibar si nchi, na Rais wa JMT akamoderate kuwa Zanzibar si nchi nje ya mipaka ya JMT, ni nchi tu ndani ya mipaka. Kwa hiyo mamlaka ya kuwa na rais, bunge na mawaziri yanaishia humu humu tu Tanzania, huko kwingine nobody knows the Isles zaidi ya kuwa eneo la kutalii
 
Nashindwa kumuuelewa Ladhu, anaonekana kuwa mwerevu sana na mzalendo, ila huenda akawa ni mnafiki mkubwa na aliyejaa chuki ndani yake. Leo hii mtataka watanganyika waondoke, kesho mtataka wapemba waondoke unguja. Kwa hali hii wanzazibar msipokuwa makini mtaparanganyika na mwishowe mtajikuta mmekuwa kama Somalia, ingawa hatuwaombei hayo. Pia jiulizeni ni wanzazibar wangapi wanaofanya kazi bara? Je, nao tuwatimue warudi kwao???
 
JUSA...Jina lenyewe ukiondoa herufi S unapata JUHA....Mnajadili JUHA wa nini, au hamfahamu maana ya juha? ngoja nifunue kamusi ya kiswahili.....

....JUHA...Mpungufu wa uwezo wa kufikiri na kuelewa mambo: mpumbavu, jura, mjinga, ****, *****, bozi gulagula.

sasa sijui mnajadili nini, mtu mwenyewe juha....shenzi zake...
 
wakuu mimi nataka nijue kinachowapa kiburi hawa wa zanzibar ni nini.?
 
Katika maajabu ya dunia natamani Jussa naye angewekwa kama kumbukumbu ya wazanzibar. Ni kijana mwenye maono na mitazamo mizuri kwa masilahi ya watu wa zanzibar, kinacho msumbua kijana mwenzetu ni element ya kibaguzi ambayo sitaki kuamini kuwa atakuwa ameiridhi toka kwa wazazi wake (rejea utumwa) Tunatambua uhuru wa kuongea na kuelezea hisia zake lakini kila anapotumia nafasi hiyo matokeo yake wote tunayaona.Yeye na wenzake wanaamini kuwa kwa ubaguzi wanaoufanya Zanzibar itakuwa kama Dubai (rejea mwandishi Ahmed Rajabu) Kila wanapokumbana na tatizo wanaamini kuwa Tanganyika ndiyo chanzo, naomba nimkumbushe tu kuwa wazee wetu ndo wanao utetea huu muungano lakini kwetu sisi vijana hatuna cha kupoteza zaidi ya kupunguza wabaguzi katika jamii yetu. Wazee wetu andikeni kumbukumbu za mahusiano ya jamii hizi ili wabaguzi kama Jussa wapate mahali pa kusoma na kuelewa maingiliano ya waswahili kwani yeye anapakukimbilia kwa wajomba zake. -AACHE UBAGUZI WAKIDINI NA MAENEO-
 
Kichwa cha habari kinavutia ila taaarifa haisomeki kutokana na lugha!
Nitachangia kutokana na kichwa cha habari tu!
Mchango wangu ni kuwa ZANZIBAR ni nchi yenye mamlaka kamili (rais,bunge(BW),mawaziri n.k), wana haki kulinda ajira kwa wazawa (Wazanzibar) tu.

hata JF tuwatoe. Kwa kweli dini ni bangi
 
It is our wishes that this kind of unitary government reaches its end. With these kind of (segregate) ideas from one part of the union our wishes are around the corner. We need Tanganyika
 
Motion to bar mainlanders jobs in Isles narrowly rejected

Members of the House of Representatives and the Isles government were at loggerheads on Thursday night when debating an amendment on the tourism Act which almost ended up in barring mainlanders from securing jobs in Zanzibar.


Source:
http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=40269
 
Mimi nachukia sana "matusi". Kwa nini watu tulimchukia Lusinde wakati sisi wenyewe tunakazana kufanana naye?

Mimi sitaki kuzungumzia kabisa Muungano wala Wazanzibar bali nataka kuzungumzia kwa nini wazanzibar wanatumiwa na wanasiasa uchwara kwa maslahi yao. Kwanza kutokana na udongo wa eneo la Zanzibar ni rahisi kufanya siasa za kuhamasishana kuchukia au kupenda kitu fulani. Sote tunakumbuka kwamba si wakati wa Mzee Karume,Mzee Mwinyi, Mzee Jumbe, Mzee Abdulwakil (R.I.P) ambako kulikuwa na huu ubaguzi uliokithiri namna hii.

Salimin Amour alipoingia madarakani Zanzibar na muda wake ulipokaribia kuisha. ndipo hizi habari za ubaguzi namna hii zilipoanza kusikika. Wakati huo ndipo shriki za "mafuta" ya Zanzibar kuweza kuigeuza kuwa Dubai ya Afrika Mashariki ilipoanza. Matatizo ya Zanzibar si Muungano wa Watanganyika bali ni wanasiasa wao wanaofikiri bila kuitaja Bara wao hawana hoja za kujihalalisha kwa wazanzibar wenzao.

Hili la Jusa linatokana na ukweli kuhusu Urais wa mwaka 2015 ambapo kutokana na hali halisi ilivyo atatoka Bara... Lakini si tu Rais ajaye atatoka Bara lakini pia atatoka chama kingine (kinaweza kuwa CHADEMA) mbali ya CCM au CUF. Na kwa kulijua hilo wao wameanza kujilinda kabla ya kutokea la kutokea.
 
Back
Top Bottom