Wazanzibari wanasubiri kwa hamu siku ya kuvunjika kwa Muungano

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Written by Nassor20
21/05/2011



Musiikatae Tanganyika yenu kwa kuitamani Zanzibar yetu,

Muungano maana yake ni makubaliano, kama ni wa nchi 2 maana ni makubaliano ya nchi hizo yanayotokana na ridhaa za watu wa pande mbili hizo husika kukubaliana? lakini huu Muungano wa Zanzibar na Tanganyika wenye kujita Watanzania hauna mvuto tena kwa upande mmoja wa Watu wa Zanzibar.

Jee nisababu gani zilizofanya upande mmoja wa Muungano watu wake washikilie Muungano uwepo na uenziwe na upande mwengine wa Zanzibar useme unataka ufe leo kesho?

Hakuna asio juwa kuwa Muungano huu una sababu kaza wa kaza kuwa haufai tena kuwepo kutokana na kupoteza uhalali wa makubaliano mama ya Muungano upande mmoja kuyakanyaga kanyaga na kutokuyaheshimu na kujipashika usuper power zidi ya upande mwengine.

Hivi sasa Upande wa Tanganyika ijitayo Tanzania imejifanya ni mtawala zidi ya upande mmoja wa Muungano ambayo ni Zanzibar kwa kisingizio cha kuwa na watu kidogo na ardhi ndoko na kutumia ilani za chama tawala na viongozi zaifu wasio jali uzalendo wa nchi yao na watu wao kuwatumilia kutokana na kuwahadaa kwa vyeo na kuwarubuni kimawazo na kipesa ili wawazibiti wazanzibar walio wengi.

Cha kusikiticha kikubwa ni kuona kuwa Mzanzibar 1 tu anaweza kulinakamiza taifa la watu wa Zanzibar kutokana na cheo chake tu chakunyakuwa kinyemela, iko mifano mingi ya wanafiki wanayo iuza Zanzibar na watu wake kutokana na njaa zao za kimaicha ama kupewa vijizweo Tanganyika au jijipendekeza waweze kuweko ktk madaraka wasio weza kuwatendea haki Wazanzibar.

Kumbuka Samia,Nahodha na kikubwa zaidi ni Spika wa Baraza la Uwakilishi Pandu Ameri Kificho hivi karibuni alivyo turubuni Wzanzibar kwa kuifanya Zanzibar kutiwa katika Group la mkoa.

Mfano hai kuwa wako Wzanzibar huangalia sana maicha yao kuliko uzalendo wa nchi, mfano ni Mh Jussa alipopeleka mswada wa sheria kuhusu kundwa tume yake Zanzibar yakukushanya maoni ili Zanzibar isingizwe ktk mkoa kama vile Dodoma na Dar-es-laam,.

Kilichotokea ni Spika wa Zanzibar Pandu Ameri Kificho kuupinga binafsi mswada yeye mwenyewe na hakuupeleka hata kwenye Baraza la Uwakilishi ili wajumbe wakaujadili na kupigia kura, yeye Kificho peke yake aliweza kutumia ubavu wake mwenyewe kutupilia mbali , tusema mawazo ya mtu moja Kificho nibora kuliko wawakilishi wengi?.

Huu ni unafiki ambao wazanzibar wanafiki tunawalea wenyewe na kuwaenzi wakati ktk mapambano ya ukombozo watu hawa hukumu yao ni kuwatenga au kifo.

Hivi sasa ukweli nikuwa Zanzibar haiwezi kupiga hatua yoyote ya maendeleo au kiuchumi kama hatujauvunja Muungano huu ambao ni fake na una choyo ndani yake.

Wenzetu wa Tanganyika wanajuwa fika kuwa kutokana na watu wake kidogo Zanzibar na fursa nyingi za kupiga hautu za maendeleo Zanzibar kumeingia uchoyo wa kuibinya kila nyanja za maendeleo na kutumia Wzanzibar wenyewe kuwa ndio waibane Zanzibar kwa kuwa chukuwa Tanganyika na kuwapa vijivyo na waliopo Zanzibar kuwazibiti kwa Sera na ilani za chama kuwa ndio mfumo wa maisha yao.

Bila ya kuvunja Muungano maendeleo nakupiga hatua za kiuchumi wzanzibar tusahau, hivi sasa kuna kila mikakati yakuimaliza Zanzibar kwa kuwazibiti Wzanzibar waloko ndani na walokuweko nje wakose haki zao.

Wtanganyika lao mmoja nikuiona Zanzibar na Wzanzibar hawafurukuti ktk ukoloni wa Muungano wa Tanganyika ijitayo Tanzania, kama kweli Wtanganyika hawana choyo basi Zanzibar ingekuwa kama Muungano wa Dubai ktk EMIRAT.

Dubai ni kijinchi kidogo na ardhi yake ni ndogo na watu wake ni kidogo,lakini kutokana na kuwa hawana uchumi mkubwa hususani mafuta, waliamua nchi za kiarabu kuifanya Dubai iwe Bandari huru (Free-port) na kuisaidia ili ipige hatua za kimaendeleo na kiuchumi.

Lakini sisi Wenzetu wa Tanganyika walivyo wachoyo hutuhukumu kila siku kutokana na udogo wa nchi yetu na watu wake na kufika hadi kutuzarau na kutubinya kiuchumi ili Wazanzibar Wzidi kumalizika kimaicha na wapate kuhama ili wao mipango yao ya kuitawala iwe.

Nyanja zote za uchumi wa Zanzibar zina-cantroliwa na Viongozi wa Tanganyika kiuchumi na kimaendeleo, kumbuka kuwa hata michahara ya wafanyakazi Zanzibar nimidogo ukilinganicha na Tanganyika, hali yakuwa makato ya TRA ni sawa sawa, hii niku-tu foolish Wzanzibar tuhame tuhamie Tanganyika kufuatia kipato kikubwa na wao ili waweze kuhamia Zanzibar na kulipwa michahara mikubwa kwa jina la Muungano.

Kama ni mshahara wa Muungano kutoka Bara jee Muungano Zanzibar haupo? au ndio kununuliwa tuze nchi yetu kwa Wabara, mimi nahisi hii ni choyo cha Tanganyika kuimeza Zanzibar kiimla, ilikuwa Kwa vile Zanzibar ni ndogo na watu wake nikidogo kuliko hata mkoa mmoja wa Tanganyika ? ilikuwa washukuwe mfano kama Dubai michahara iwe mikubwa au tulingane kwa michahara kwa vile Tanzania ni mmoja kama wenyewe wanavyo sema.

Lakini wenzetu wanafanya kila mbinu na kila hila ili waizibiti Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo kukuwa, hivi sasa ukipanda boat utaona watu wanao miminika Zanzibar kutoka Tanganyika hawana idadi na hii ni mipango kabambe ya Kanisa na Serekali kuwamimina na uhubiri wa kanisa ni kuwasaedia miradi midogo midogo ili wabakie wasirudi bara kwa lengo la kuongeza wingi watu wenye asili ya Tanganyika na chakuticha wengi wao ni watu wenye mazhebi ya ukristo.

Hii ni ajenda kabambe na Wzanzibar tukisema tuna subiri viongozi wetu watutatulie janga hili au atokee mtu mfazili atusaidie basi tumesherewa, nilazima sisi wenyewe wananchi tutatuwe matatizo yetu kwa kushirikiana na njia pekee na silaha yetu ambayo wenzetu hawaipendi ni Uzanzibar kwanza na hiyi tumeweza kwa kurusdisha amani na udugu wetu Wzanzibar ambao uligawika kwa misingi ya kupandikizwa chuki,uhasama na utengano kwa faida ya kugaiwa ili mafisadi na wasio itakia mema Zanzibar na Wazanzibar yao yawaendee.

Wazanzibar waloko nje ya Zanzibar kuna ajenda ya kulengwa kwa kupoteza haki zao za Uzanzibar.

Hivi sasa kuna hatari ya wale Wzanzibar waloko nje ya Zanzibar na walikwicha kubadilicha uraia wao kwa njia moja au nyingine lengo la Wtanganyika ni kuwageuza Wapalestina waloko nje kukosa haki zao ktk ardhi ya Palestina,huu ni mfumo tayari wamechafundiswa Tanganyika na Mayarudi kuwapunguza Wazanzibar na kuwaingiza Watanganyika Zanzibar.

Kutokana na kuparatikia madaraka viongozi wetu wa smz hudowa vitambulicho vya ukazi na uzanzibar kwa wasio Wzanzibar ili wapate kuendelea na madaraka? lakini jee wenzetu wa Tanganyika lengo na agenda ni lipi? nikuhakikicha kuwa kutokana na population ya Zanzibar million 1.2 itafunikwa na Wtanganyika million 44 kipindi kifupi tu kwa vile milango yote iko wazi ya kuingia Zanzibar na viongozi wa smz pado sio wazalendo wako na dogo za macho kuwa Tanzania ni mmoja na mtu yoyote anaweza kuishi sehemu nyingine ya upande wa Tanzania.

Tujifunze kutoka Kwa Maboorige na Ausralia Wazungu kutoka Uengereza kuivamia Australia nchi ya Maboo? hii leo Maboregen wanaonekana ni watu wa misituni tu na ngoma zao za jadi na huku Wazungu wakionekana ni wenye miliki zote za Australia wakati ni wakeni wahamizi kutoka Ungereza.

Ni kwanini Wazanzibar tuna imani zenye kutuzuru na kutuwekea mazara?

Katika harakati za kujigomboa hakuna imani mbele ya wanafiki kama Kificho, Samia, Nohodha wala yoyote mwenye kuleta asari ktk jamii? lakini sisi Wzanzibar bado tuko na nongo za macho na hata mtu afuje vipi bado tunamkubati na kumuenzi. Dunia imebadilika tutakuwa wamwicho kujigomboa na maendeleo ya nchi yetu na watu wake hata tukishtuka tutashindwa kumjuwa Mzanzibar halisi ni yupi na asio kuwa ni yupi.

Lengo la Road map kwa Waisrail na vikao visivyo kwicha na Wapalestina ni kuimega na kuimaliza Palestina na Road map itakamilika kwa Waisrail pale wanapo fika ulingoni kuchaimaliza Palestina hapondio watawaita Wapalestina kuja kukaa na kuzungumza Amani huku kinacho Zungumzwa hakipo tena ardhi ya wazulumiwa wa Kipalestna imemalizwa.

Kwa hio na sisi Wazanzibar kama tutajiwashia basi kuna hatari yakuwa wageni katika ardhi, viongozi wa ccm/smz niwababaichaji na kecho na kecho kutwa Zanzibar ikichatiwa kisawa sawa makuchani kwa Watanganyika na wao kukosa utapia mloo watakuja kungana na sisi na kuanza kukoboa macho.

Wazanzibar tusikubali wajukuu zetu kuja kuwaegea mazingira magumu na mazito? usiwe na chakula lakini atlist uwe na kwenu hili ndio lakujivunia na kujifaharicha, kila mzaliwa wa Tanganyika ana kabila lake na mkoa anao toka.

Mungu ibariki Zanzibar na wazanzibar na uwatowe tongo za macho wanafki wetu Zanzibar nchi inakwenda. smz ziwezeni njaa zenu mukinusuru kizazi Muungano ni mzigo mzito muliotutuka wananchi bila ya kujali kuwa unatumiza na imefika wakati wakuutuwa.
 
Swali la kujiuliza kwa Wanzibari

1. Sisi ni Damu na Tanzania Bara na Tuwe wamoja au
2. Sisi ni tofauti na Tunatawaliwa

Kama jibu ni la kwanza basi tuwe na nchi moja na haki zote za Tanzania. Kama jibu ni la pili basi himizeni watu wapiganie uhuru kamili na Zanzibar kama nchi. Hii inaweza kuleta vita lakini kama mnaamini basi piganieni uhuru.

Tatizo ni kwamba hakuna jibu la tatu.
 
Makamo wa raisi Gharibu Bilali ametamka kuwa atalishulikia suala la kero za muungano mpaka zimalizike zote. Mganga mkuu amefariki sasa itakuwaje bila mganga. Hhahahahah.
Hakuna Bilali wala widadi wazanzibari hawataki muungano basi. Musijisumbue bure na pipi zenu sisi hatuna hamu nazo.
 
Shit, hilo la muungano kuvunjika ni ndoto tu, ni sawa na fisi anapofuatilia mkono wa binadam akizani utaanguka aule. Zaidi ya hayo hata kura ya maoni kuhusu kuvunja muungano hamna, nafasi iliyopo ni moja tu , kuujadili muungano kwa nia ya kuuboresha, yaani kuondoa kile kinachoitwa kero za muungano, kama kweli zipo, basi.
 
Si tunachotaka ni serikali yetu ya Tanganyika muungano ufe usife haituhusu Tanganyika Tanganyika tunakupenda
 
Shit, hilo la muungano kuvunjika ni ndoto tu, ni sawa na fisi anapofuatilia mkono wa binadam akizani utaanguka aule. Zaidi ya hayo hata kura ya maoni kuhusu kuvunja muungano hamna, nafasi iliyopo ni moja tu , kuujadili muungano kwa nia ya kuuboresha, yaani kuondoa kile kinachoitwa kero za muungano, kama kweli zipo, basi.


Roman Empire?

Ottoman Empire

British Empire?

Songhai Empire?

TANGANYIKA EMPIRE?

Nothing is impossible Mkuu, keep watching this page.

Zanzibar for Zanzibaris and we can't wait to see your backs.
 
Kwenye kura ya maoni ktk mchakato wa katiba hilo suala ni lazima liwepo.MUUNGANO CHINI:biggrin1:
 
Kwenye kura ya maoni ktk mchakato wa katiba hilo suala ni lazima liwepo.MUUNGANO CHINI:biggrin1:


Hatutaki kuulizwa kama tunataka UHURU wetu, Azimio la BLW linatosha Mkuu Kibakwe.

Tumechoka kutawaliwa na mfalme wa Tanganyika.

Zanzibar for Zanzibaris.
 
Muungano haukwepeki kujadiliwa, wanachofanya watawala wetu ni kupoza moto badala ya kuuzima kitu ambacho kinaashiria kuwa lazima kuwe na ama serikali tatu au kuuvunja kabisa, wa-Tanzania bara hakika hawanufaiki kabisa na muungano kama wazanzibari wenyewe, ila kwakuwa Zanzibar ni ndogo ndio maana wanafikiri wanaonewa na pia fikra zao za mafuta nk zinawahadaa kabisa.
 
Hatutaki kuulizwa kama tunataka UHURU wetu, Azimio la BLW linatosha Mkuu Kibakwe.

Tumechoka kutawaliwa na mfalme wa Tanganyika.

Zanzibar for Zanzibaris.
avatar40787_1.gif
:dance:
 
Hapa Tanzania kuna jamii hata wasome vipi uwezo wao wa kufikiri unaendelea kuwa mdogo tu. Kwa kuwa inawezekana wewe mtoa mada ukawa mmojawapo sina sababu ya kushangaa.

Ogopa sana mtu anayeamini kufa binadamu ni mipango ya Mungu lakini anakataa kutokea kifo cha Osama kwa kuamini si rahisi Osama akauawa kwa risasi za kimarekani, na kisha anadai aoneshwe maiti yake ili aamini. So stu...!
 
nsha choka mie muungano wa kulazimishana kwani hii imekuwa ndoa ya kwetu (Wakatoliki) tufike mahali tuelezene ukweli wazanzibar waende na sie tubaki na Tanganyika yetu( Ingawa mie napenda tubaki na jina la Tanzania hata kama hao machogo wataondoka)
0
 
Roman Empire?

Ottoman Empire

British Empire?

Songhai Empire?

TANGANYIKA EMPIRE?

Nothing is impossible Mkuu, keep watching this page.

Zanzibar for Zanzibaris and we can't wait to see your backs.
Kwa kweli uko sahihi. Tunahitaji Tanganyika yetu nanyi mbaki na Zanzibar Yenu
 
Back
Top Bottom