Swali: Ni kwa namna gani Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano itatuondolea ufisadi, umaskini, maradhi, ujinga, kutujengea shule, kutujengea zahanati/hospitali, kutupunguzia vifo vya mama wajawazito, kutulindia raslimali zetu dhidi ya wageni, kupunguza division 0 za f4, etc? Just let me know, au tunataka tuheshimu Wajerumani walioianzisha Tanganyika ambayo hata hivyo ilijumuisha Rwanda na Burundi? Only that? Kwa nini tusiheshimu kile tulichokitengeneza wenyewe? Mbona Zanzibar ya 1600s ilijumuisha mikoa ya Pwani na Morogoro? Nini "faida" ya kutengana anyway? Au watz wanataka vyeo tu, eti mimi Rais wa Tanganyika! Dhambi ya ubaguzi itauua Muungano, Tanganyika itakayozaliwa na hata Zanzibar!
Ndugu yangu Urusi uliamuwa kutowa uhuru kwa mataifa iliyoyajumuisha kwake kwa hila ili ipate nafasi ya kujiendeleza. Nayo Tanganyika ifanye hivyo iache hila na kuiachia Zanzibar ijiendeshe na kama kuna mambo ya kujumuika basi na iwe hivyo huku kila mmoja akiwa huru. Kuungana ambako viongozi wetu wanatdanganya kuwa kunafanyika duniani sio mujumuiko ya kiutawala bali kwa mambo mnayoona yana faida kwa pamoja na ndio maana tunasikia kunaJumuiya ya Ulaya.