Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,299
- 33,082
WAZANZIBARI KUFUNGUA KESI KATIKA MAHAKAMA ZA KIMATAIFA (UINGEREZA) DHIDI YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKIDAI UKIUKWAJI WA KATIBA.
Habari za kiuchunguzi zinadai kuwa wazanzibari kwa umoja wao bila kujali itikadi zao sasa kufungua kesi katika mahakama ya kimataifa Uingereza dhidi ya serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushinikiza ukiukwaji wa katiba ya Zanzibar na kuwanyima wazanzibar haki ya msingi ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Taarifa zinasema wazanzibari watadai mahakani kwamba Serikali ya Dk Magufuli inatumia nguvu za dola kukandamiza haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemtaka, hatua hiyo imekuja baada ya CUF chama kikuu cha upinzani Zanzibar kutokuwa na imani na mahakama za Zanzibar juu ya uvunjwaji wa katiba ya Zanzibar na sheria ya uchaguzi.
Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wameeleza kuwa hatua hiyo itaukuza mgogoro wa kikatiba wa Zanzibar na kuwa mgogoro wa kimataifa huku baadhi ya mataifa ya magharibi yakiotoa wataalamu waelekezi (consultants) kuwaelekeza kundi hilo la wazanzibari jinsi ya kufungua na kuendesha keshi hiyo kwa umahiri mkubwa.
Endapo wazanzibari hao watashinda madai yao na Serikali ya Tanzania ikashindwa kutekeleza madai amri ya mahakama ya kimataifa Tanzania itakabiliwa na vikwazo vya kimataifa hali ambayo itapelekea uchumi wa Tanzania kuporomoka na hali ya maisha ya watu wa kawaida kuwa ngumu zaidi (maarufu kama tutaisoma namba). Kutokana na hali hiyo baadhi ya wanasiasa wakongwe nchi wameshauri haki itendeke Zanzibar ili kuepusha Tanzania na aibu zaidi.
Chanzo: Mwandishi wetu