Wazanzibar walio kimbilia Somali warejea Nyumbani Zanzibar.

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=3]Picha: Watanzania waliokuwa wakimbizi nchini Somalia warudi Zanzibar[/h]

Watanzania waliokuwa wakimbizi katika kambi ya Mogadishu nchini Somalia wakielekea kupanda mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar jana










Baadhi ya Watanzania 38 waliokuwa wakimbizi Jijini Mogadishu wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kushuka katika ndege la Umoja wa Mataifa iliyowaleta nyumbani wakiwa na wake zao walioa nchini Somalia baada ya kuishi huko kwa miaka 11,walikimbia vurugu za Januari 26/27 mwaka 2001

Watoto ambao kwa sasa ni Raia wa Somalia wakiwa na wazazi wao Raia wa Tanzania waliokuwa wakimbizi nchini Somalia wakisubiri taratibu za Uhamiaji katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume jana baada ya kuwasili wakitokea Mogadishu na ndege ya Umoja wa Mataifa chini uangalizi wa UNHCR


Baadhi ya akinamama Raia wa Somalia ambao wameolewa na Watanzania waliokuwa ukimbizini Mogadishu wakifurahia jambo walipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,hapa walikuwa wakisubiri taratibu za Uhamiaji

Baadhi ya Watanzania waliokimbilia Mogadishu nchini Somalia mwaka 2001 wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Zanzibar jana. Wa kwanza ni Mohammed Adam(38) akiwa amembeba mwanawe mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume,wanaotazama kamera ni baadhi ya wake wa Watanzania hao ambao ni raia wa Somalia waliowasili jana wakitokea Mogadishu Somalia na ndege ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia huduma za kibinadamu

Source: ZanziNews




Posted by Roy Snr. at 23:57
 
Wakimbizi wa Tz warejea makwao,kumbe hata Tz kuliwahi kuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe?

Kisiwa cha amani!!???
 
Hawa watu wanajua mahala salama kweli? Yaani mtu ukimbie Tanzania uende kusaka amani Somalia!! Kweli tumeumbwa na utofauti wa ajabu! Anyway tunashukuru wamerejea salama tuendelee n a ujenzi wa taifa.
 
Duuuuuuh, kwisha habari yetu, wamerudi baada ya kupata full mafunzo ya AL-SHAABAB. Duuuh UAMSHO!
 
al shaabab; walienda ughaibuni kutafuta wanawake wazuri wa kisomalia; wanaipenda sana ccm
 
Back
Top Bottom