Wawili wafia mgodini kwa kukosa hewa

kingwipa1

JF-Expert Member
Jul 2, 2008
334
51
Habari nilizopata punde ni kwamba kuna watu wawili wamefia mgodini huko kwenye machimbo ya Merelani kwa kukosa hewa. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo tar 21/01/2010.
Watu hao walikuwa wameenda kufanya kazi kwenye mgodi mmoja wa wachimbaji wadogo wadogo uliopo kwenye kitalu B.
Maiti wamehifadhiwa wenye hospitali ya mkoa wa Arusha.

Chanzo cha kukosa hewa hakijajulikana na mimi nafuatilia kwa watu wa karibu ili kujua chanzo cha mauti iliyowakuta ndugu zetu.

Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amina
 
Habari zaidi zinadai maafa hayo yametokea kwenye mgodi uliowahi kuuwa watu kama 20 kwa mafuriko. Nadhani tukiohilo lilitokea mwaka juzi. Watu walio karibu watupe habari zaidi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom